Mkapa ainanga serikali ya Kikwete


Mkuu dawa ya haya yote ni M4C. Tuwape nafasi na muda maana hawa waliopo wameshajikita mfano wa ruba. Sasa hawa ruba wakipuliziwa M4C lazima walegee
 
Mkapa ni hopeless. Amesahau uhuni alioufanya ikulu. Kufanya biashara akiwa ikulu yeye na mke wake. Akae kimya asitukumbushe uhuni alioufanya yeye na Mramba.

"Mtakula nyasi ili dege bovu la raisi linunuliwe". Mnata raisi apande PUNDA??
 
upeo wa kujadili ISSUES humu jf ni wa kutia shaka,kumbe mkapa hakukosea kusema kwamba WATANZANIA NI WAVIVU WA KUFIKIRI,,tutakufa maskini kwa mtindo huu,,waliokuwepo kwenye kigoda cha mwl nyerere udsm walielewa mkapa alkuwa na maana gani,,tusichangie kwa ushabiki,jengeni hoja mnapayuka tu.Kipindi chake nchi ilikua kiuchumi,akalpa maden sugu,wafadhili wakasamehe maden mengine,miradi mingi ya maendeleo ilitegemea pesa ya ndani,MLITAKA AFANYEJE?NYIE NDO HAMNAZO
 
Hata mkapa aache unafiki kwani ana mchango mkubwa ktk hilo,yeye ndo aliongoza sera yake ya hovyo ya ubinafsishaji holela wa mashirika ya umma na kuiingiza nchi katika mikataba ya kimangungo.hata hivyo KIKWETE NI DHAIFU HAWEZI KUUKABILI UOVU ULIOPANDWA NA MWINYI,UKAKUZIWA NA KUIMARISHWA NA MKAPA NA SASA TUMEANZA KULA MAFAO YAKE YAKE,utamu wenyewe bado
 
Hapa tuseme tu ukweli tu, Mkapa alikosea aana wakati yupo Madarakani, lakini pia hiyo haimfungi mdomo kusema anachoamini ni makosa au kuna tatizo fulani! Ukweli pia ni kwamba kipindi cha mkapa uchumi ulikua sana! Hivi sasa hali yetu ni duni na ni aibu sana, sijui ****** atajivunia nini baada ya ngwe yake kuisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…