Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,608
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amewaonya Wakandarasi wanaochekelewesha ameonesha Miradi ya Maendeleo na kuonyesha kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa katika Wilaya za Wanging’ombe na Makambako, Mkoani Njombe.
Akizungumza katika ziara yake ya kikazi katika maeneo hayo leo, tarehe 22 Julai 2025, Aweso amebaini mapungufu mbalimbali hasa upande wa Mkandarasi, ikiwemo kuchelewesha mradi na kuwepo kwa
Aweso amesisitiza kuwa hatua za haraka lazima zichukuliwe dhidi ya wale wote wanaokwamisha utekelezaji wa mradi huo, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya Maji Safi na Salama kama ilivyokusudiwa. Waziri Aweso amewaagiza Watendaji wa Wizara ya Maji pamoja na Mkandarasi anayetekeleza Mradi huo kutoka Kampuni ya Larsen and Taubro Limited kuhakikisha kazi inafanyika kwa bidii, usiku na mchana.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Antony Mtaka, amewaasa Wakandarasi Wazawa, kwa kusema kwamba wanapopata fursa ya kutekeleza Miradi mikubwa kama hiyo wanapaswa kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na weledi ili kuendelea kuaminika katika utekelezaji wa miradi ya baadaye. Aidha, mradi wa maji wa Wanging’ombe na Makambako ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita Milioni 13 za Maji kwa siku, hatua ambayo itaboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji Safi na Salama katika maeneo hayo.