Mkakati wa kuinyofoa CCM madarakani 2015: Ushauri kwa vyama vya upinzani

THE GREAT CAMP

JF-Expert Member
Jun 29, 2012
765
194
Salamu zangu kwenu vyama vya upinzani: Mimi si mwanasiasa, ila ni mkereketwa wa Mabadiliko ya kweli katika maisha ya Mtanzania anaye nyanyasika ndani ya nchi yake: Kwa kuangalia historia za chaguzi mbalimbali barani Africa, demokrasia imekuwa ikihujumiwa na serikali nyingi zilizo madarakani. Hivyo Mwaka 2015 nashauri vyama vya upinzani kufanya yafuatayo:

1. Vyama vya upinzani kwa nia moja viungane na visimamishe mgombea mmoja wa Urais
2. Kwenye majimbo ya uchaguzi, vyama vigawane ili mgombea mmoja wa ubunge anaye kubalika kutoka upinzani asimamishwe
3. Kila kura 1 ya Mtanzania ina thamani kubwa, Hivyo muungano wa vyama utapunguza mtawanyiko wa Kura
4. Muungano wa vyama vya upinzani UWAKUMBUSHE watumishi serikalini ile kauli ya Serikali ya CCM kuwa "HATUHITAJI KURA ZA WAFANYAKAZI". Hivyo tafuteni idadi kamili ya watumishi wa serikali mjue ni wangapi maana huo ndiyo mtaji wa kura za kunzia.
5. Hakikisheni kwa umoja huohuo mnalinda kura zenu kuanzia mwanzo hadi mwisho (HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE)
6. Mkubaliane kuunda serikali ya pamoja bila kuwa na uroho wa madaraka/Wizara za kuungoza
7. Umoja wenu usiangalie usipendelee dini wala kabila la mtu Tanzania

NB: Mkifanya hivyo kwa nia thabiti CCM haita ambulia kitu 2015.

Bandugu JF huo ni ushari wangu tu, Na wewe unaweza kuongezea ushauri wa kwako.

MUNGU
IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE WOTE.
 
bila elimu ya uraia ni kazi bure kuungana, angalia kenya kura zilizoharibika ni kutokana na ukosefu wa elimu kwa wapiga kura.CDM kwa kuanzisha majimbo basi kazi kubwa iwe kutoa elimu na si kumshambulia NEPI itakula kwenu.toeni elimu ya umuhimu wa;
  • kujiunga na cdm
  • kujiandikisha kupiga kura
  • kupiga kura
  • kulinda kura hadi matokeo yatangazwe
kilichompata Raila na wafuasi ni kupiga kura na kukimbia kujificha wakamuachia fisi bucha bila ajizi ameji-sevia kura 600,000
 
Mawazo yako sio mabaya, lakini chama cha CCM sasa hivi hakina watu.

Kwa mambo yanayofanywa na serikali ya CCM; waislam wote walioko CCM ni CUF wakristo wapenda haki CHEDEMA, watakaobaki ni mafisadi wachache, CCM watashangaa 2015 wala hakitokuwa chama cha tatu. Wakipata sana watakuwa nafasi ya nne.

Kama wanabisha wajaribu kuitisha uchaguzi wa kuziba nafasi za udiwani zilizo wazi za ARUsha lazima wawe wa nne nyuma ya chadema CUF na NCCR, wanatakiwa wajue hilo na hawawezi kuchomoa,mwenye masikio na asikie
 
Kuungana kwa vyama vya upinzani ni muhali sababu wameshindwa kuungana bungeni kuunda Serikali kivuli seuze waungane kuunda Serikali kuu? kila chama kinamtuhumu mwenzie! Chadema ambacho ni chama kikuu cha upinzani kinamuita CUF nyumba ndogo ya CCM! huku wote wawili wakirushiana lawama za udini na ukabila! Chadema na Nccr maelewano ni madogo sana sasa wataungana vipi kuiondoa CCM wakati hawapiki chungu kimoja?

Kabla ya kuungana, nilazima wajenge mazingira ya kuaminiana ili wapate daraja la kupitia kwenda ktk Muungano! mimi sijui sera za vyama vya upinzani kama zinafanana lakini kama wanasera tofauti nilazima Muungano wao uzingatie kukubaliana kutokukubaliana! la sivyo wakiungana kibubusa mwisho nchi itawashinda wakibaki kugombea madaraka! yametokea Kenya, Zimbabwe, Italy nk.
 
mawazo yzko sio mabaya,lakini chama cha ccm sasa hivi hakina watu,kwa mambo yanayofanywa na serikali ya ccm; waislam wote walioko ccm ni CUF wakristo wapenda haki CHEDEMA, watakaobaki ni mafisadi wachache,ccm watashangaa 2015 wala hakitokuwa chama cha tatu,wakipata sana watakuwa nafasi ya nne.kama wanabisha wajaribu kuitisha uchaguzi wa kuziba nafasi za udiwani zilizo wazi za ARUsha lazima wawe wa nne nyuma ya chadema CUF na NCCR, wanatakiwa wajue hilo na hawawezi kuchomoa,mwenye masikio na asikie

Unamaana gani kusema Wakristo wapenda haki wako Chadema? una maana Wakristo wasiopenda haki wako CCM? na unaushahidi gani kuwa Wakristo wako Chadema na Waislamu wako CUF? jee, NCCR nao kuna dini ipi? TLP nadhani amebaki Mrema pekee na yeye alishakuwa Mlokole tangu zamani!
 
Ushauri wako murua kabisa, lakini wahakikishe pia inakuwepo TUME HURU YA UCHAGUZI, bila hivyo watapigwa bao kali sana la kisigino.
 
Bila ya muungano wa wapinzani ni vigumu kushinda, hata ikiwa hoja ya kuweka mgombea mmoja wa rais haiwezekani basi at least muungane katika majimbo na uchaguzi wa wabunge, kuhakikisha majority ijayo ya bunge liwe kwa wapinzani, kuhakikisha balance ya power inarudi kwa wananchi, na upendeleo mkubwa unaonekana bungeni uliolishusha heshima bunge unaondoka kwa nguvu za upinzani. Rais na serikali nzima itakuwa accountable kwa bunge huru lenye nguvu..
 
Muungano wa vyama vya upinzani ni ngumu, sheria zetu haziruhusu,labda ushirikiano wa kivyama, lakini huo ushirikiano utasikia kina mrema wanaanza sema yeye ndo awe mgombea wa urais. Ccm itapenyeza mapandikizi wengi sana kwenye ushirikiano huo!
 
mawazo yzko sio mabaya,lakini chama cha ccm sasa hivi hakina watu,kwa mambo yanayofanywa na serikali ya ccm; waislam wote walioko ccm ni CUF wakristo wapenda haki CHEDEMA, watakaobaki ni mafisadi wachache,ccm watashangaa 2015 wala hakitokuwa chama cha tatu,wakipata sana watakuwa nafasi ya nne.kama wanabisha wajaribu kuitisha uchaguzi wa kuziba nafasi za udiwani zilizo wazi za ARUsha lazima wawe wa nne nyuma ya chadema CUF na NCCR, wanatakiwa wajue hilo na hawawezi kuchomoa,mwenye masikio na asikie
Please mode hii kitu mbona hakina abuse report button? nataka kukifuta nisaidie
 
mawazo yzko sio mabaya,lakini chama cha ccm sasa hivi hakina watu,kwa mambo yanayofanywa na serikali ya ccm; waislam wote walioko ccm ni CUF wakristo wapenda haki CHEDEMA, watakaobaki ni mafisadi wachache,ccm watashangaa 2015 wala hakitokuwa chama cha tatu,wakipata sana watakuwa nafasi ya nne.kama wanabisha wajaribu kuitisha uchaguzi wa kuziba nafasi za udiwani zilizo wazi za ARUsha lazima wawe wa nne nyuma ya chadema CUF na NCCR, wanatakiwa wajue hilo na hawawezi kuchomoa,mwenye masikio na asikie

Kwa hiyo mkuu sisi WAISLAMU tulokuwa chadema ni sawa na kusindikiza msalaba sio? poa ni mawazo yako ila kwa nijuavyo mimi chadema hatuna udini kihivyo ndio maana hata padre wetu tunategemea aongoze nchi hapo 2015.
 
chadema wao wanajiona ndo kila kitu. waache waende peke yao.

Hapana tukiacha Chadema waende peke yao inawezekana lengo letu tunalolitaka lisitimie. Hivyo CHadema ihakikishe ina washawishi wapinzani wengine kuunda Umoja, ili hii mimtu CCM isilambe kitu 2015 .
 
Kweli hoja ya mtoa thread. Ina mashiko kwa kuangalia kenyata na ruto walivyoungana bila kujali wako katika nafasi gani na matunda ya kuungana wameyaona,embu tujiulize kama ruto na kenyata wangebaki katika vyama vyao kwa kudhani wana population ya watu wengi leo hii nani angekua rais kati yao? Ni lazima uongozi wa cdm pamoja na vyama vingine wajue wanachi wanataka nini? Tena ikiwezekana zoezi hilo lianze hv sasa isije ikafika 2015 wakaanza kupigana vikumbo vya urais!
 
Kweli hoja ya mtoa thread. Ina mashiko kwa kuangalia kenyata na ruto walivyoungana bila kujali wako katika nafasi gani na matunda ya kuungana wameyaona,embu tujiulize kama Ruto na Kenyata wangebaki katika vyama vyao kwa kudhani wana population ya watu wengi leo hii nani angekua rais kati yao?

Ni lazima uongozi wa cdm pamoja na vyama vingine wajue wanachi wanataka nini? Tena ikiwezekana zoezi hilo lianze hv sasa isije ikafika 2015 wakaanza kupigana vikumbo vya urais!


.......

Unafahamu, watu wanadhani umaarufu unasaidia. Kujaza umati wa watu haimaanishi kuwa wote ni wafuasi wako.

Mimi naogopa sana vigeugeu vya Watanzania. Umoja tuu ndiyo utakao saidia kuikomboa hii nchi. CCM inatakiwa kupotezwa kabisa, ibaki Historia tu.

Hilo litawezekana tu kama vyama vya Upinzani vitaungana. Nasema hivi kwasababu nao CCM wanatambua kuwa wamechuja machoni na masikioni mwa wa Tanzania, hivyo lazima watakuwa na mkakati madhubuti wa kulinda himaya yao.

Chonde chonde UPINZANI msipuuze haya tunayo yasema humu JF.
 
Hilo ndio suluhisho la kuitupa nje CCM,shughuli ni kwamba wanasiasa wetu wengi wana njaa na hawana nia ya dhati ya mabadiliko wanahangaikia matumbo yao hivyo wananunulika kiurahisi na kufanya kazi ya propaganda za ccm na kuleta misuguano wakiwa ndani ya muungano huo.
 
Back
Top Bottom