Mkakati wa kuiboresha tanesco – je unataka tanesco mpya iweje?

mimi pekee

Member
Sep 25, 2012
9
0
SHIRIKA LA UMEME TANZANIATAARIFA KWA UMMA

Shirika la umeme Tanzania TANESCO lipo katika mchakato wa kufanya mabadiliko ya kimuundo na kiutendaji ili kuboresha huduma zake kwako mteja wetu. Kwa kutambua umuhimu wako wewe kama mdau mkubwa katika sekta ya nishati ya umeme, shirika linakuomba kushiriki katika kutoa maoni yako ya namna ambavyo ungependa TANESCO mpya iwe, ili kusaidia kuleta mabadiliko yatakayoboresha kutekeleza majukumu yake ya kukuhudumia wewe mteja wetu kwa ufanisi mkubwa.
Unaweza kutuma maoni yako kupitia barua pepe tanesco.iweje@tanesco.co.tz au communications.manager@tanesco.co.tz au piga simu kwenye namba +255 222451185. Pia unaweza kutuma maoni yako kupitia facebook yetu chini ya tangazo hili kwa kutafuta neno ‘TANESCO iweje’ au kupitia blog yetu iitwayo umemeforum.blogspot.com.Unaombwa pia kutoa ushirikiano wako pindi wafanyakazi wa TANESCO watakapopita wakigawa dodoso fupi kama njia ya kukusanya maoni yako.
“Pamoja Tujenge TANESCO Yenye Ufanisi”

Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano
TANESCO MAKAO MAKUU


 
Back
Top Bottom