Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 601
- 2,508
JAJI MTUNGI NA MKAKATI MBAYA DHIDI UPINZANI.
(mchambuzi huru)
Tangu serikali hii ianze kuongoza, nchi ni kama imerejeshwa kwenye mfumo wa chama kimoja. Shughuli za vyama vya siasa zimepigwa maarufuku. Wananchi, wanasiasa na viongozi wa vyama vya siasa hawana Uhuru katika taifa lao.
Mutungi anajua hili, lakini amekuwa kimya.
Jaji Mutungi, msajili wa vyama vya siasa, hajali. Yuko bize kutishia kufuta Chadema.
Ukimya wa Mutungi unadhirisha kuwa yeye ni sehemu ya mpango haramu wa kuzuia Uhuru wa vyama vya siasa katika taifa. Anatumwa au anajituma kwa maslahi yake ya sasa na baadaye.
Mutungi alianza kutumika kutengeneza, kuimarisha na kuendeleza mgogoro ndani ya chama cha wananchi-CUF. Mutungi alijua kabisa Lipumba hana uhalali wa kisheria kwa kurejea kuwa mwenyekiti baada ya kujiuzulu 2015. Anajua migogoro ndani ya CUF ungemalizwa kwa utashi wa vikao vya uongozi wa CUF. Ofisi yake ilingia kwenye mgogoro ili kuiangamiza CUF.
Alihakikisha ofisi yake inamtambua Lipumba kinyume na utaratibu huku akijua si kazi ya ofisi yake kumtambua au kumrejesha ofisini kiongozi wa chama cha siasa tena aliyejiuzuru.
Mkakati huu ovu wa Mutungi ulipanua mgogoro na sasa umeiacha CUF Vipande vipande-CUF ya Lipumba na CUF ya Maalim Seif. Ndivyo alivyotaka Mutungi, anajiita mlezi wa vyama vya siasa. Kwa ilivyo CUF sasa ni kama vile imekufa. CUF haiko kama ilivyo zamani. Hii ndio raha ya Mutungi.
Sasa Mutungi amemaliza kazi yake kwa upande wa CUF, amehamia rasmi kuendeleza kazi yake, anatamani kufuta Chadema kwa sababu ni Chama kikuu cha upinzani kinachoogopwa na chama tawala.
Mkt wa chama tawala ametumia kofia ya urais kufuta shughuli mikutano ya vyama vya siasa kinyume na Katiba. Msajili wa vyama siasa naye anatishia kufuta vyama vya siasa.
Mutungi alianza kujiingiza taratibu kwenye mgogoro wa CUF, akafanikiwa. Sasa ameanza kuifuatilia Chadema. Anakoenda Mutungi kunajulikana. Anaharibu.
Kazi anayofanya Mutungi, haina tija kwa taifa Bali inaweza kuliingiza taifa kwenye matatizo makubwa sana. Mutungi azuiliwe, yupo kwa ajili ya kuvuruga taifa. Amepoteza sifa ya kuwa mlezi wa vyama vya siasa.
Katika zama hizi za demokrasia ukiona mtu mzee aina ya Mutungi anafikiria kufuta vyama vya siasa, anazeeka vibaya au amepitwa na wakati.