Mkakati maalumu wa kukiimarisha Chama cha Mapinduzi

Hapo kuna mambo mawili..
mleta mada hii hapa jf ametumwa ailete na amelipwa kiasi fulani..

pili aliyemtuma kaweka namba zake za simu akitegemea malipo ya uchawa wake!
 
Lakini Samia mwenyekiti halali wa CCM. Huo ujumbe anataka ufike kwa mwenyekiti wa CCM siyo raisi wa nchi.
Ukisoma maelezo yote yanalenga kuhimarisha CCM.
britanicca hajawahi kupinga uchaguzi au uteuzi wa Mwenyekiti Samia kuwa mwenyekiti wa CCM

Huwezi tenganisha Serikali na CCM kwenye hii nchi Mkuu.

Unapomtaja Samia unataja Rais wa nchi, na Mwenyekiti wa CCM.

Unasema britanicca hajawahi kumpinga Mwenyekiti wake?
 
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan

Nakusalimu kwa JMT,
Kidumu Chama Cha Mapinduzi,

Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema, uhai, amani na utulivu kwa ujumla katika Taifa letu.

Pia, nakupongeza pamoja na Serikali yako kwa ujumla kwa kazi nzuri na kubwa mnayoifanya ya kuleta maendeleo na mabadiliko katika maeneo yote.

Ndugu Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wetu, ni heshima kubwa kwangu kuwasilisha kwako mchango wangu huu utakaosaidia kuimarisha Chama. Naomba nitumie muda wako ,kuwasilisha MKAKATI MAALUMU WA KUKIIMARISHA CHAMA CHA MAPINDUZI kama ifuatavyo:

Kwanza, nashauri kuwe na maboresho makubwa ya TEHAMA katika michakato yote ndani ya CCM. TEHAMA iboreshwe katika namna ambayo michakato ya uchaguzi, uenezi, itikadi kampeni mafunzo na mingineyo ifanikishwe na irahishwe kupitia TEHAMA. Hii itatoa fursa kwa wengi kukifahamu Chama Cha Mapinduzi, kuondoa au kupunguza malalamiko na kukisaidia Chama kukabiliana vema na changamoto za mabadiliko ya teknolojia na akili mnembe ambayo yanaweza kuleta athari hasi katika uimara wa CCM miaka ya baadae.

Pili, Utunzaji wa Siri za Chama . Imekuwa ni jambo la kawaida taarifa za ndani na nyingine za siri za CCM kuvuja au kuvujishwa mitandaoni. Kwa ujumla, taarifa za ndani na zile za siri mara nyingi uwa ni mikakati ya ushindi hivyo kuvuja au kuvujishwa inafanya mikakati na mbinu za CCM kujulikana na kupelekea hatari ya kushindwa au kushinda chini ya kiwango Cha matarajio. Katika utunzaji wa Siri, nashauri idadi ya wajumbe wa vikao vinavyojadili siri ipunguzwe na wajumbe wa vikao hivyo wasaini waraka maalumu wa kulinda na kutunza Siri za Chama ,pia kuwe na kiapo Cha utiifu kwa Chama ambapo anayeapa kiapo hiko hatorudishiwa uanachama ikibainika ameshiriki katika kuvujisha siri za Chama. Pia, nashauri Chama kiondokane na mfumo wa kutoa nyaraka za siri katika " hard copies" na badala yake nyaraka za siri zipatikane kwenye " soft copies" na online tu, yeyote anatakiwa kuzifungua ni yule mwenye utambulisho maalumu.

Pia, Chama kijenge mfumo ambao ili usome nyaraka ya Siri ni lazima uwe kwenye mazingira ya ndani ya jengo la Chama ili kuzuia upatikanaji wa nyaraka hizo nje ya maeneo mengine na nyaraka za siri zote ziwe ni " read only" kwa namna yoyote isiwezekane kui- print au ku-screetshot au kuipiga picha. Pia ,utengenezwe mfumo ambao utasaidia kuchukua sura ya mtu anayeisoma au kuipitia nyaraka kwenye mfumo na mfumo ujifunge mara moja pale sura hiyo itakuwa sio Ile iliyosajiliwa kuniona nyaraka hiyo. Hii itasaidia siri za Chama kutunzwa kwa ukamilifu.

Tatu, udhibiti na usimamizi wa rasilimali. Chama imara ni lazima kiwe na rasilimali watu na vitu vya kutosha ili kukiwezesha Chama kufanya shughuli zake kwa umakini na ufasaha Nashauri kipaumbele kikubwa kiwekwe kwenye juhudi za kuongeza rasilimali watu na vitu, malengo na mikakati iwekwe kwa kila mkoa kuongeza idadi fulani ya wanachama wapya, ubunifu uongezwe kwenye kubuni miradi ya kuongeza mapato ya Chama, mashirika ya Chama yasimamiwe kikamilifu na vitega uchumi viongezewe tija, jumuiya za Chama zijiendeshe kwa ubunifu na tija, elimu ya ujasiriamali na uwekezaji itolewe kwa viongozi na wanachama na mafunzo ya uzalendo ,utiifu na uadilifu kwa Chama yatolewe mara kwa mara Hii itasaidia Chama kuwa na rasilimali za kutosha katika kujieneza na rasilimali watu bora sana yenye ufahamu wa miiko ya Chama.

Nne, ufanyikaji wa MIDAHALO na MIJADALA ya kitaifa. Nashauri Chama kianzishe utaratibu wa kufanya mijadala na midahalo kama njia ya kupata mawazo mbadala, kurekebisha na kujenga upya sehemu yenye kasoro. Hii itasaidia Chama kupata ufumbuzi wa haraka wa changamoto na kupata picha ya matarajio ya wengi kupitia midahalo na mijadala hiyo

Tano, ufanyikaji wa TAFITI . Chama kinatakiwa kichochee ufanyikaji wa TAFITI za mara kwa mara zenye kuchochea mabadiliko katika maisha ya watu. TAFITI zitasaidia mabadiliko makubwa ya haraka na Imani ya watu kwa CCM kuongezeka sana.

SITA, iundwe kamati ya ufuatiliaji na tathmini ndani ya CCM. Moja ya sababu kubwa ambayo huwa inasababisha CCM kupoteza imani ni kuona utekelezaji hakuna. Nashauri iundwe kamati ya ufuatiliaji na tathmini ndani ya CCM itakayokuwa na jukumu la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo , ahadi, ilani, sera za CCM na maagizo ya viongozi wa CCM na kutoa maoni na ushauri. Kamati hii pamoja na mambo mengine iwe ni jukumu la kuishauri kamati kuu au halmashauri kuu pale itakapoona inafaa ni hatua gani zichukuliwe ili utekelezaji uwe bora zaidi.

Saba, nashauri ianzishwe idara ya mipango, mikakati na strateji ili kiwe ni chombo rasmi cha kupanga, kuweka mikakati na strateji za kutimiza na kuiwasilisha kwenye vikao vya juu vya Chama kwa ajili ya utekelezaji.

Ahsante kwa kunipa muda wako ,

Naomba kuwasilisha

Wako katika ujenzi wa Taifa,
KARLO THOBIAS MWILAPWA
mwilapwakarlo@gmail.com
0715 804 254
Hiyo teknolojia haipo.
 
Pili, Utunzaji wa Siri za Chama . Imekuwa ni jambo la kawaida taarifa za ndani na nyingine za siri za CCM kuvuja au kuvujishwa mitandaoni. Kwa ujumla, taarifa za ndani na zile za siri mara nyingi uwa ni mikakati ya ushindi hivyo kuvuja au kuvujishwa inafanya mikakati na mbinu za CCM kujulikana na kupelekea hatari ya kushindwa au kushinda chini ya kiwango Cha matarajio.
Umri unaenda bado mnazeeka na tabia Chafu na huu ndio uhalisia wenu.

Weak link kwenye 0's & 1's ( taarifa )ni watu ..... Mtavujisha wenyewe mwisho mtekane na muuwane.
 
Naona unajipigia chapoo bwana Mwilapa..

Hii nchi kufikia nchi ya ahadi inataka wanaume waliokamilika kama Lissu na Heche wengine wachumia tumbo..!!
 
Hii inakupa picha members wengi humu tulivyo watupu kichwani.
Wengi tunakimbilia kusoma vichwa vya habari na kuangalia aliyeleta habari ni wa upande gani, inatakiwa kabla ya kumjibu mtu tunatakiwa tusome habari nzima na angalau kujaribu kuelewa kimeandikwa kitu gani je kimeandikwa kwa lengo gani?
 
Hili ni Bandiko la mtu si langu nimesoma nikaona niliweke hapa Kwakuwa Jana Samia kashinda JamiiForums siku nzima
 
CCM haihitaji kuimarika kwa sasa, inastahili kukaa pembeni na kupotea kabisa.

CCM ni kansa kwa watanganyika na wanaoitakia mema Tanganyika.
 
Naomba kuwasilisha

Wako katika ujenzi wa Taifa,
KARLO THOBIAS MWILAPWA
mwilapwakarlo@gmail.com
0715 804 254
Mtu na akili zako timamu, kweli unakaa chini kupoteza muda wako kuandika mambo kama haya juu ya chama ambacho tayari kinachungulia kaburi?

Mkuu, ni hivi: Tanzania Mpya haina nafasi hata ndogo ya takataka kama hii ya CCM.

Tanzania haiwezi kamwe kupona bila ya hili zimwi la CCM kuangamizwa.

Umeandika kama hujui CCM ina maana gani kwa waTanzania wakati huu.
 
Hii akaunti itakuwa "HACKED" .
Hapana.

Mwandishi siyo yeye,; yeye katumiwa tu kwa umaarufu wa jina lake hapa JF, na kwamba anajulikana kuwa mwanachama wa chama hicho.

Tatizo la mwandishi ni kama yeye hajui kabisa CCM iliyopo na hiyo anayoshauri ifanyiwe marekebisho.

Sasa sijui anataka marekebisho ya nini wakati CCM wenyewe hawana hofu yoyote ya kupoteza kura; maanake kura haziwaweki madarakani miaka yote..
Hata bila kushangaa, hajazungumzia lolote kuhusu uovu unaofanywa na chama chake, na wala haoni matatizo na ufisadi ndani yake.
Yeye anapiga tu, mradi ujumbe ufike, na kwa vile kaweka na namba ya simu, akumbukwe kuingizwa kwenye ulaji.
 
Hapo kuna mambo mawili..
mleta mada hii hapa jf ametumwa ailete na amelipwa kiasi fulani..

pili aliyemtuma kaweka namba zake za simu akitegemea malipo ya uchawa wake!
Sijalipwa na siwezi penda kulipwa

a0a603d9-f6c9-461e-9318-92c2ae95b676.jpeg
1c758dfd-12da-4c5a-a050-8d6ed684a556.jpeg
 
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan

Nakusalimu kwa JMT,
Kidumu Chama Cha Mapinduzi,

Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema, uhai, amani na utulivu kwa ujumla katika Taifa letu.

Pia, nakupongeza pamoja na Serikali yako kwa ujumla kwa kazi nzuri na kubwa mnayoifanya ya kuleta maendeleo na mabadiliko katika maeneo yote.

Ndugu Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wetu, ni heshima kubwa kwangu kuwasilisha kwako mchango wangu huu utakaosaidia kuimarisha Chama. Naomba nitumie muda wako ,kuwasilisha MKAKATI MAALUMU WA KUKIIMARISHA CHAMA CHA MAPINDUZI kama ifuatavyo:

Kwanza, nashauri kuwe na maboresho makubwa ya TEHAMA katika michakato yote ndani ya CCM. TEHAMA iboreshwe katika namna ambayo michakato ya uchaguzi, uenezi, itikadi kampeni mafunzo na mingineyo ifanikishwe na irahishwe kupitia TEHAMA. Hii itatoa fursa kwa wengi kukifahamu Chama Cha Mapinduzi, kuondoa au kupunguza malalamiko na kukisaidia Chama kukabiliana vema na changamoto za mabadiliko ya teknolojia na akili mnembe ambayo yanaweza kuleta athari hasi katika uimara wa CCM miaka ya baadae.

Pili, Utunzaji wa Siri za Chama . Imekuwa ni jambo la kawaida taarifa za ndani na nyingine za siri za CCM kuvuja au kuvujishwa mitandaoni. Kwa ujumla, taarifa za ndani na zile za siri mara nyingi uwa ni mikakati ya ushindi hivyo kuvuja au kuvujishwa inafanya mikakati na mbinu za CCM kujulikana na kupelekea hatari ya kushindwa au kushinda chini ya kiwango Cha matarajio. Katika utunzaji wa Siri, nashauri idadi ya wajumbe wa vikao vinavyojadili siri ipunguzwe na wajumbe wa vikao hivyo wasaini waraka maalumu wa kulinda na kutunza Siri za Chama ,pia kuwe na kiapo Cha utiifu kwa Chama ambapo anayeapa kiapo hiko hatorudishiwa uanachama ikibainika ameshiriki katika kuvujisha siri za Chama. Pia, nashauri Chama kiondokane na mfumo wa kutoa nyaraka za siri katika " hard copies" na badala yake nyaraka za siri zipatikane kwenye " soft copies" na online tu, yeyote anatakiwa kuzifungua ni yule mwenye utambulisho maalumu.

Pia, Chama kijenge mfumo ambao ili usome nyaraka ya Siri ni lazima uwe kwenye mazingira ya ndani ya jengo la Chama ili kuzuia upatikanaji wa nyaraka hizo nje ya maeneo mengine na nyaraka za siri zote ziwe ni " read only" kwa namna yoyote isiwezekane kui- print au ku-screetshot au kuipiga picha. Pia ,utengenezwe mfumo ambao utasaidia kuchukua sura ya mtu anayeisoma au kuipitia nyaraka kwenye mfumo na mfumo ujifunge mara moja pale sura hiyo itakuwa sio Ile iliyosajiliwa kuniona nyaraka hiyo. Hii itasaidia siri za Chama kutunzwa kwa ukamilifu.

Tatu, udhibiti na usimamizi wa rasilimali. Chama imara ni lazima kiwe na rasilimali watu na vitu vya kutosha ili kukiwezesha Chama kufanya shughuli zake kwa umakini na ufasaha Nashauri kipaumbele kikubwa kiwekwe kwenye juhudi za kuongeza rasilimali watu na vitu, malengo na mikakati iwekwe kwa kila mkoa kuongeza idadi fulani ya wanachama wapya, ubunifu uongezwe kwenye kubuni miradi ya kuongeza mapato ya Chama, mashirika ya Chama yasimamiwe kikamilifu na vitega uchumi viongezewe tija, jumuiya za Chama zijiendeshe kwa ubunifu na tija, elimu ya ujasiriamali na uwekezaji itolewe kwa viongozi na wanachama na mafunzo ya uzalendo ,utiifu na uadilifu kwa Chama yatolewe mara kwa mara Hii itasaidia Chama kuwa na rasilimali za kutosha katika kujieneza na rasilimali watu bora sana yenye ufahamu wa miiko ya Chama.

Nne, ufanyikaji wa MIDAHALO na MIJADALA ya kitaifa. Nashauri Chama kianzishe utaratibu wa kufanya mijadala na midahalo kama njia ya kupata mawazo mbadala, kurekebisha na kujenga upya sehemu yenye kasoro. Hii itasaidia Chama kupata ufumbuzi wa haraka wa changamoto na kupata picha ya matarajio ya wengi kupitia midahalo na mijadala hiyo

Tano, ufanyikaji wa TAFITI . Chama kinatakiwa kichochee ufanyikaji wa TAFITI za mara kwa mara zenye kuchochea mabadiliko katika maisha ya watu. TAFITI zitasaidia mabadiliko makubwa ya haraka na Imani ya watu kwa CCM kuongezeka sana.

SITA, iundwe kamati ya ufuatiliaji na tathmini ndani ya CCM. Moja ya sababu kubwa ambayo huwa inasababisha CCM kupoteza imani ni kuona utekelezaji hakuna. Nashauri iundwe kamati ya ufuatiliaji na tathmini ndani ya CCM itakayokuwa na jukumu la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo , ahadi, ilani, sera za CCM na maagizo ya viongozi wa CCM na kutoa maoni na ushauri. Kamati hii pamoja na mambo mengine iwe ni jukumu la kuishauri kamati kuu au halmashauri kuu pale itakapoona inafaa ni hatua gani zichukuliwe ili utekelezaji uwe bora zaidi.

Saba, nashauri ianzishwe idara ya mipango, mikakati na strateji ili kiwe ni chombo rasmi cha kupanga, kuweka mikakati na strateji za kutimiza na kuiwasilisha kwenye vikao vya juu vya Chama kwa ajili ya utekelezaji.

Ahsante kwa kunipa muda wako ,

Naomba kuwasilisha

Wako katika ujenzi wa Taifa,
KARLO THOBIAS MWILAPWA
mwilapwakarlo@gmail.com
0715 804 254
Ushauri mzuri sana, ila naimani hayo yote CCM wanayafahamu na kutotekeleza sio kwa bahati mbaya. Ni hilo tu!
 
Hapana.

Mwandishi siyo yeye,; yeye katumiwa tu kwa umaarufu wa jina lake hapa JF, na kwamba anajulikana kuwa mwanachama wa chama hicho.

Tatizo la mwandishi ni kama yeye hajui kabisa CCM iliyopo na hiyo anayoshauri ifanyiwe marekebisho.

Sasa sijui anataka marekebisho ya nini wakati CCM wenyewe hawana hofu yoyote ya kupoteza kura; maanake kura haziwaweki madarakani miaka yote..
Hata bila kushangaa, hajazungumzia lolote kuhusu uovu unaofanywa na chama chake, na wala haoni matatizo na ufisadi ndani yake.
Yeye anapiga tu, mradi ujumbe ufike, na kwa vile kaweka na namba ya simu, akumbukwe kuingizwa kwenye ulaji.
Ngoja niseme nimekurupuka, sijasoma hadi mwisho, nilipitia tittle tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom