Mkakati: Lowassa kuhamia UKAWA

Wakikata jina lake, hata kama hatahamia UKAWA wafuasi wake watahamia huko na itakuwa pigo kwa magamba!
 
Mtoa mada una majungu leta story za ukweli kuhusu comrade lowasa..
 
Karibu ila tabia za ccm za wizi uzusfshi uongo udini kufumaniwa Na wake za watu hatutAki
keza
 
Lowasa ana uchungu sana na umaskini Wa watanzania kuliko kiongozi yeyeto kwa sasa. Ndiye atafaa kutuvusha mwakani kwenye mkwamo Wa kiuchumi.
 

SUPU YA MAWE: Huko kwetu supu ya mawe ni pombe haramu ya chang'aa!

On a serious note, tafuta thread yangu yenye title "Ndoto ya matumaini ya Lowassa kuishia CC ya CCM"

Mpaka sasa hivi mikakati ya CCM ni kukata jina la Lowassa kwenye CC ya CCM. Vigunge wa CCM na hasa Mwenyekiti wao hawataki kabisa Lowassa awe next Rais wa JMT, kwasababu hawajui Lowassa atamfanya nini JK na Ridhwani baada ya kumtosa kwenye sakata la Richmond.

Mkulu alikwisha mwambia Lowassa aachane na ndoto ya Urais, lakini Lowassa akamwambia kwamba ni haki yake ya kikatiba hivyo amuache demokrasia ichukue mkondo wake ndani ya CCM, halafu Watanzania tutaamua.

Lakini pia baada ya muungano wa UKAWA kwa wale wachache wanaoipenda CCM, wanaona itakuwa ni mlima mkubwa kumnadi Lowassa mbele ya UKAWA kutokana na kashifa za ufisadi zinazo mzunguka. Zile zama ambapo mgombea wa CCM alipokuwa anapitishwa na mkutano mkuu wa CCM tayari ni Rais wa JMT zimepita.

Aidha pia kuna swala la afya ya Lowassa. It is un deniable true, kwamba afya ya Lowassa sio "NZURI" sana. Je, kama Lowassa atachaguliwa kupeperusha bendera ya CCM ataweza about four months grueling za kampeni? Na hasa wana CCM hao wakirejea matukio ya kuanguka kwa JK, ambaye relatively ana afya "nzuri" kulinganisha na Lowassa, tena mbaya zaidi kwenye kampeni zenye ushindani mkubwa katika historia ya nchi hii, ambapo sasa vyama vya upinzani vyenye nguvu vimeungana kuunda UKAWA.

CCM is now on DILEMA, wanataka kum contain Lowassa kwani akitoka CCM is a double edged sword to CCM, hata kama hatagombea URAIS kupitia UKAWA, lakini Lowassa akitoka CCM ndiyo hivyo CCM wanakipa a kiss good bye kiti cha URAIS wa JMT. Lowassa anafahamu hilo, CCM wanafahamu hivyo.

Mpaka sasa CCM wametegeneza mkakati mmoja, watapandikiza wagombea mamuluki wa nafasi ya rais, ili CC ya CCM itakapokata majina, yawe mengi including jina la Lowassa. Ili kama baadaye Lowassa atalalamika, ionekane hoja yake haina mashiko bali uroho wa madaraka, kwani CCM watakuja na propaganda mbona majina yaliyokatwa ni mengi tu, kwanini yeye Lowassa tu ndiye alalamike kama sio uroho wa madaraka. Akina Nape tayari wameshaandaliwa kwa kazi hiyo.

Kulingana na Katiba ya CCM, CC ya CCM itapendekeza majina yasiyozidi matano kwenda NEC ya CCM kupigiwa kura kwa waombaji wa nafasi ya URAIS. Majina matatu ya kwanza yatakayoshika nafasi ya juu kwenye kura za NEC yatapelekwa mkutano mkuu kupigiwa kura, kumpata mgombea mmoja atakaye peperusha bendera ya CCM.

Hakuna vigezo vya wazi vinavyofahamika ambavyo CC ya CCM hutumia kupendekeza majina yasiyo zidi matano kwenda NEC kupigiwa kura. CC ya CCM ndiyo litakuwa the last nail on the coffin of Lowassa, kwani jina lake na majina mengine ya wana CCM wengi wao wakiwa waliopandikizwa yatapokatwa.

Mpaka sasa hivi majina yatakayopendekezwa na CC ya CCM ili priority order ni kama ifuatavyo
  1. Mizengo Kayanza Pinda (sitting PM)
  2. Prof Mark Mwandosya (alifanya Vizuri nyuma ya JK kwenye uchaguzi wa 2005)
  3. Jina moja la Mzanzibari (kudumisha muungano, bado jina hilo halijakubaliwa yapo 3 yanayotajwa)
  4. Dr. Asha Rose Migiro (gender balance, Prof Tibaijuka alikuwa awe mmojawapo lakini nafikiri sasa sakata la escrow limemtupa nje)
  5. ........................... (??) Hili bado ni kitendawili linajumuisha wana CCM wengi eg, Mwakyembe, Sitta, Membe, Magufuri, Nahodha, Karume Jnr,Wassira, Makamba Jnr etc lakini Lowassa si miongoni mwao. Hili jina litachaguliwa kutokana na upepo wa kisiasa wakati huo.

Naomba kuwasilisha
 

Kundi la mwigulu naona mpo kazini. Unafanya sweeping analysis kwa kuleta fallacy of irrelevance kwa Mzee wetu lowasa.

Lowasa still the leading political figure in Tanzania.
 

labda awe waziri mkuu wa ukawa
 
Last edited by a moderator:
Kundi la mwigulu naona mpo kazini. Unafanya sweeping analysis kwa kuleta fallacy of irrelevance kwa Mzee wetu lowasa.

Lowasa still the leading political figure in Tanzania.

If this is fallacy utawatendea haki JF kama basi ukiwaeleza ukweli, lakini kusema fallacy of irrelevance kuishia mitini unakuwa hajamusaidia huyo MZEE WAKO LOWASSA.

BTW, mimi nilikuwa nakuanda KISAIKOLOJIA siku CC ya CCM itakapokata jina la MZEE WAKO LOWASSA usife kwa KISEBUSEBU NA KIROHO PAPO!
 
Lowasa naye sijui anachokitafuta japo na wewe mleta mada ni mzushi wa kutupa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…