Waminepo
JF-Expert Member
- Feb 3, 2019
- 374
- 255
Bro Pascal, wewe ni mwandishi mzuri na nguli ! Mimi nashauri uandike kitabu (riwaya) kama vya akina Shafi Adam Shafi au Shaaban Robert , prof. Ngugi wa Thion'go au prof. Wole Soyinka na uuze mtandaoni bro ! Utapiga hela sana ! Yaani mafumbo yako ni hatari sana bro, uko vizuri mno !!! Ushauri tuu ! Tafuta theme moja iandikie kaka yangu, yawezekana labda umeanza. Au hata uwe columnist kwenye magazeti makubwa kama alivyo kuwa marehemu prof. Abdulrahman Mohamed Babu kwenye Africa Now magazine enzi hizo !Wanabodi
Hapa mimi ni mjumbe tuu na mjumbe hauwawi, hizi ni Salaam bona-fide na genuine za mahabusu kwa rais Magufuli.
Baada ya tangazo la Rais Magufuli la msamaha kwa watuhumiwa wa ufisadi la juzi Jumapili, jana asubuhi nimetembelea gereza fulani kuwasalamia jamaa zangu fulani ambao wako ndani huu mwaka wa 4 kwa kesi ya utakatishaji fedha, ili kwenda kuwapa habari njema ya Rais Magufuli kuwasamehe kwa lengo la kuwashauri wakiri tuu makosa hata kama wamesingiziwa tuu, na wakubali tuu kulipa hayo mabilioni hata kama hawana, ndugu tutachangishana na kama ni kuuza nyumba zetu, mashamba yetu na mali zetu alimradi wapendwa wetu wawe huru.
Kufika tuu ile kuwaona, japo hata msamaha bado, lakini tayari sura zimeanza kutabasamu kwa tabasamu la matumaini ya kuwa huru tena, kwa sababu kikawaida ziara za magerezani ni ziara za huzuni huzuni, this time ilikuwa ni ziara ya furaha na matumaini. Kiukweli Rais Magufuli atabarikiwa sana kuleta tumaini kwa watu kama hawa kwa sababu wengine tayari walikuwa na sura za kukata tamaa kabisa.
Kwa vile ni mwanahabari, nikajiona mjanja kuwahi kupeleka habari hiyo njema kwa watu wote, ile kukaa, badala ya mimi kutoa habari, mimi sasa ndio napewa habari!.
"Bwana Paskali, najua umekuja leo mapema hivi asubuhi kwa sababu ya lile tangazo la jana la rais Magufuli, hapa sisi wenyewe tumelisikia na kutazama live TBC, baada tuu ya Tangazo lile, geraza zima lililipuka kwa shangwe, vifijo na vigelegele kumshangilia rais Magufuli kwa huruma yake"
Nilielezwa.
Ndipo nikauliza kumbe magerezani siku hizi kuna mpaka TV!. Kumbe siku hizi wafungwa na mahabusu wanaruhusiwa kuangalia TV?. Kiukweli tumepiga hatua, japo sikuuliza mahabusu wanalala wapi, maana najua tuu watakuwa bado wanalala chini, au sikuuliza wanajisaidia wapi, maana najua watakuwa bado wana... debe.
Kumbe maboresho ya jela zetu sio tuu kutoka karandinga hadi mabasi ya hadhi, na nguo za madurufu hadi cotton za orange, bali magerezani kumbe siku hizi ni hadi TV!. Haya ni maendeleo makubwa.
Nikafanya majadiliano na jamaa yangu kuhusu taking advantage of this golden opportunity, akanimbia kiukweli yeye amesingiziwa tuu, kuukubali msamaha wa rais Magufuli, ni kukubali kosa ambalo sio la kweli, na after all the amount anayotuhumiwa nayo ni too substantial ambayo hawezi kui raise in his remaining life time, hivyo bora aendelee kuvumilia tuu mateso hadi haki itendeke, na isipotendeka, yuko tayari kufia jela halafu karma itamlipia.
Kiukweli nilimshauri, such an opportunity ni golden opportunity, comes once in blue moon, what is haki compared freedom, or what is money compared to his liberty?.
Nikamtolea mfano wa January Makamba, kwenye ile sauti kwa mlioisikia, ametukana wapi?. Kama waziri mzima, mbunge mzima, amekosewa kwa kudukuliwa na hajatukana chochote lakini kutumbuliwa na kuomba msamaha, what about him?. Nimemshauri, na huu ni ushauri kwa wana jf wote wenye ndugu watuhumiwa, washaurini ndugu zenu waandike barua za kuomba msamaha hata kama hawajakosa au wamesingiziwa, waombe tuu msamaha na kuahidi kulipa, kwani pesa ni nini compared, tutachangishana kulipa, barua iandikwe, msamaha uombwe, kwa sababu usipoandika barua, kutake advantage ya msamaha huu, kwa hoja ya kutafuta haki, huwezi kujua itachukua muda gani kuipata hiyo haki, nikitolea mfano yule wakili Medium Mwale wa Arusha, amekaa mahabusu miaka 8 hadi uchunguzi kukamilika, kesi ikasikilizwa kwa siku moja tuu, akakiri makosa na kuhukumiwa kulipa faini, akalipa, akatoka, unaweza kulinganisha angekubali kosa, hiyo miaka 8 gerezani angefanya mambo mangapi tena fani yenyewe ni uwakili?.
Pia mahabusu wengine ambao siwajui ila kwa kuniona zamani nilikuwa Mtangazaji wa TV hivyo wao wananijua, wakanituma niwafikishie salaam zao kwa rais Magufuli kuwa wanamshukuru sana, wanampenda sana, na kuna mmoja akaahidi siku ya kutoka, breki ya kwanza ni geti la Ikulu kumshukuru kwanza rais Magufuli, ndipo aende nyumbani kujiunga na familia yake.
Mahabusu wengine nao wakatuma maombi yao kwa rais Magufuli kuomba msamaha huo uwe extended kwa mahabusu wote wa kesi zote hadi mwizi wa kuku kuwa yuko tayari hata kulipa kuku wawili kwa hoja kuwa watuhumiwa wote ni Watanzania na binadamu wote ni sawa, hivyo kama sasa haki
inanunuliwa kwa pesa, na msamaha huo ni watuhumiwa wa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ambazo ni watu wazito na kiwango cha fedha ni fedha nyingi, wanaomba jicho la huruma ya rais Magufuli pia lielekezwe kwa watuhumiwa masikini na wa makosa yote ikiwemo makosa ya wizi, warudishe kile walichoiba akiwemo mwizi wa kuku, nao pia waununua uhuru wao wawe huru kuja kulijenga taifa, tena you can just imagine, baada ya msamaha huu wa rais Magufuli, unajua kabisa kura zao watampigia nani!.
Salaam kutoka kwa mahabusu wa kesi za ukwepaji kodi, wao wameomba huruma ya rais Magufuli, wasemehewe tuu hilo deni la kodi na hawatakwepa tena. Mahabusu mmoja akasema "kama serikali yetu imeweza kuwasamehe wale wazungu wa Acacia lile deni la kodi ya dola bilioni 190 ya Noah zetu, serikali hii inashindwaje kuwasamehe Watanzania wazawa na wazalendo wa kweli wa taifa hili ambao walikwepa kodi kutokana na kubana kwa vyuma?".
Mjumbe hauwawi, kama rais Magufuli, kufuatia upendo wake kwa raia wake, na huruma yake kwa Watanzania wanaoteseka magerezan kwa kusubiria kutendewa haki, then haki hiyo itendeke kwa wote, sio mafisadi tuu, wahujumu na watakatishaji fedha, bali watuhumiwa wote bila ubaguzi, hata wenye tuhuma za mauaji, tuwapelekee pale wale wazee wa Gambosh, jamaa wakiri waliua na kuahidi kurudisha uhai wa waliokufa kwa msaada wa wazee wa Gambosh, nao wafutiwe kesi, mwizi wa kuku arudishe kuku, etc, Binadamu wote ni sawa na Tanzania ni moja.
Mungu Mbariki Rais Magufuli huruma yake pia iwaangazie watuhumiwa wengine.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali