Mjue TUNICATE.

Mjue TUNICATE.

The Dictator

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
4,323
Reaction score
11,762
tunicate_komodo-jpg.3343884

SEA SQUIRT (tunicate) ni mnyama/samaki wa baharini ambaye anapokuwa mchanga, anakuwa na ubongo wake kama tu ilivyo kwa viumbe wengine na huogelea akitafuta sehemu ya kudumu ya kujishikilia, kama vile mwamba.

Mara anapopata sehemu hiyo, hujishikilia hapo, kisha hufanya kitu cha ajabu:

humeza/hula au huvunjilia mbali mfumo wake wa neva za fahamu, ikiwa ni pamoja na ubongo wake.

Sababu? Haitaji tena kuhamia mahali pengine wala kuchambua mazingira mapya. Kwa ufupi anakuwa karidhika.

— chakula chake (planktoni) huingia kwa kufyonzwa tu kwa kupitia maji yanayopita mwilini mwake. Wala ahangaiki....

Kwa maneno mengine: ubongo wake ulimsaidia kumtafutia nyumba, na baada ya kuipata, hana tena haja ya kufikiri au kusogea.

Ni mfano wa kushangaza sana wa jinsi viumbe wanaweza kubadilika kutokana na mazingira yao.

Na pia, ni mafumbo mazuri ya kifalsafa yasemayo: ukishafika mahali pazuri kimaisha, je, utahitaji tena kuwa na ubunifu au fikra endelevu?
 
Attachments

  • Tunicate_komodo.jpg
    Tunicate_komodo.jpg
    2.1 MB · Views: 17

Duuh..hii Dunia Ina viumbe wengi sana.Huyu mwamba sasa nae hufa au? Vipi analiwa?wanazaanaje Hawa?
 
Back
Top Bottom