Mjue Miguna aliyemuapisha Raila Odinga

mbari

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
509
421
UNAMJUA MIGUNA WA NCHINI KENYA

Aligombea Ugavana wa Jiji la Nairobi huko Kenya na akapata kura zaidi ya elfu tisa. Baadae akajitangaza kama Jenerali wa vuguvugu la kuipinga Serikali ya Kenya kupitia Chama kiitwacho (NRM) National Resistance Movement of Kenya.

Ndiye aliyemuapisha Raila Odinga kuwa Rais wa Watu wa Kenya. Kesho yake baada ya kiapo cha Raila Odinga akatangaza Picha zote za Uhuru Kenyatta zishushwe popote zilipo na akapanga kuzichoma moto hadharani.

Usiku wa siku hiyo hiyo, Polisi wakazingira Nyumbani kwake na silaha nzito, wakavunja mlango kwa kuulipua na wakamkamata.

Badala ya kumpeleka Kituo cha Polisi cha kilichopo jirani wakamsafirisha usiku huo huo na kumpeleka Mikoani yaani ni kama wamtoe Dar Es Salaam wampeleke Dodoma halafu wakatae kumpeleka Mahakamani.

Sio hilo tu, pia wakazuia mtu yeyote asimuone wala kuongea naye licha ya Mahakama kutaka afikishwe Mahakamani, mpaka pale Jaji alipotoa Amri kwa Mkuu wa Polisi na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai ndipo wakampeleka Mahakamani wenyewe.

Badala ya kumpeleka mfano Mahakama ya Dar Es Salaam alikotakiwa kupelekwa kwa mujibu wa order ya Mahakama, wakampeleka mfano Mahakama ya Serengeti Mkoani Mara.

Mahakama ya Serengeti ikasema, mrudisheni huyu Miguna Mahakama Kuu ya Dar Es Salaam, kabla hajapelekwa huko, Mahakama kwa mujibu wa malalamiko mengine ya waleta maombi, ikatoa uamuzi aachiwe kwa dhamana ya elfu hamsini.

Polisi badala ya kumuachia Miguna kwa dhamana ili kutii order ya Mahakama, waliendelea kukaidi order hiyo ya Mahakama na usiku wa kuamkia leo inasemekana Miguna amesafirishwa kwa ndege ya Serikali kupelekwa nchini Canada, nchi ambayo ana uraia pacha pia.

Binafsi najiuliza, Miguna alikamatwa na Polisi kwa sababu za makosa ya kijinai au Miguna alikamatwa na watu wa Idara ya Uhamiaji kwa sababu ya kuwa na uraia pacha wa Canada?

Bado najiuliza, Polisi na Dola ya Kenya wanamhofia huyu Miguna kuliko Raila Odinga aliyemuapisha. Huyo (pichani) ndiye Miguna Miguna wa (NRM) National Resistance Movement Of Kenya anayemuunga mkono Rais wa Watu wa Kenya Raila Odinga.
FB_IMG_1518060980658.jpg
 
Dola katika ubora wake....ukicheza nayo utaijua...ulete uchoko watu wakuache who are you?
 
Ongezea: Muda wote aliowekwa kusikojulikana alilazimishwa kusimama tu walipomuonea huruma aliambiwa alale sakafuni...pia alipewa chakula Mara mbili tu!

Hajakamatwa kwa uhaini kwakua katiba yao ime state mpaka muda Wa kiapo cha Rais na ataapishwa na Jaji mkuu au Naibu wake na ikiwa hayupo/hawapo bunge litaitishwa kuweka utaratibu! kimsingi Hata Raila hana kosa kwakua aliapa kua rais Wa watu na si Jamhuri! Tena saa sita mchana! hahah na hata hati ya kiapo iliandaliwa kiufundi sana!

In short jamaa ni critic Wa Uhuru! na Uhuru hampendi kaakua jamaa anajiita political commentator na kingereza chake chenye ma vocabulary tata..Uhuru alisema baada ya uchaguzi iwe marufuku kwa watu wanao jiita wachambuzi kwa media! Miguna ndiye Lissu wao!
 
Huyu na Odinga ni wa kuweka ndani wanacheza na maisha ya watu hasa Kenya ambapo kitu kidogo tu watu wanaweza kuchinjana.

UK aendelee kuwaminya hivyo hivyo haya mambo ya sijui democracy isiyo na mipaka ni upuuuzi.
 
hapo ndo naikumbuka ile movie ya olympia is fallen apart,ha ha ha!leo tunaweza sema,kenya is fallen apart.lol!very shame
 
Nimekumbuka enzi Daniel Arap Moi alipokua Rais, huu upuuzi haukuwa ukifanyika na Kenya ilikua ni moja ya Nchi zenye nidhamu ya hali ya juu....
Gademmit....
Haikuwa nchi ya nidhamu bali Moi alikuwa dikteta aliwapiga na kuwakamata wapinzani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom