Mjue Donald Trump

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,280


Donald Trump alizaliwa June 14, 1946, Mmarekani mfanyabiashara ambae sura yake si ngeni kwenye TV, pia ni mwanasiasa na mfanyabiashara.
Trump alizaliwa katika jiji la New York na alipata shahada yake ya uchumi mwaka 1968 kutoka Chuo Kikuu cha Pennyslavania. Akiwa mwanafunzi alifanya kazi kwenye kampuni ya baba yake iliyojihusisha na ujenzi, na mwaka 1971 alikabidhiwa hati miliki za kampuni hiyo.

Trump ni mtoto wa pili kutoka mwisho kuzaliwa katika watoto wanne wa Fred na Mary Tramp, wamebaki watoto watatu baada ya kaka yao mkubwa Fred Jnr. kufariki kutokana na matatatizo ya ulevi wa kupitiliza, hii ni sababu iliyomfanya Donald kujiepusha kabisa na matumizi ya pombe na sigara.

Kutokana na matatizo ya tabia Donald aliacha shule ya Kew-Forest School akiwa na umri wa miaka 13 na kujiunga na New York Military Academy ambako alimaliza darasa la nane na elimu ya masomo ya juu (High School). Baba yake alipowahi kuhojiwa, baba yake Trump akisema Trump alikuwa mtukutu sana akiwa mdogo.

Akiwa NYMA, Trump alicheza kwata, alivaa uniform na alifikia cheo cha Captain, mwenyewe aliwahi kumumelezea mwandishi wa habari zake kuwa, NYMA ilimpa mafunzo mengi ya kivita kuliko waliowahi kwenda vitani.

1964 Donald Trump akiwa New York Military Academy.
 
Kujisifu kote kumbe alirithishwa kampuni. Marekani hawana rais kwa staili hii
 
Trump ana mbagua nani? Mtu mweusi? Sasa kule ni Marekani ni nchi yao weupe.

Tukisema Trump hatashinda kisa ubaguzi, population ya US itatuumbua. Ratio Kati ya blacks na whites.

Watu wengi saivi dunia, nchi kibao zinaingia kwenye Neo-nationalism, ndio kutokea kwa brexit etc...kwa mfumo huo wa sasa, watu kuweka nchi zao mbele kwanza inatosha kuleta picha kuwa Trump atashinda tho media zinambana na kumwekea bad coverage ila box la kura halitadanganya.
 
 
Mike Tyson kwao wapi
 
Jazia nyama,yaani kwa hayo maandishi matatu,ndio umemuelezea trump...mbona Amini ulimwelezea vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…