Shukrani iende kwa 'Brother' wangu Muhammad Muhammad alinipa story hii miaka 19 iliyopita nikiwa Darasa la Kwanza lakini sitaisahau.
Wengi mmekuwa mkisikia kuhusu 'Ndoto za Alinacha' habari yake kamili hii hapa;
Alinacha alikuwa ni kijana mmoja maskini asiye na kitu aliyeishi zama hizo miaka kibao ilopita. Siku moja katika pitapita zake alitokea Mtu mmoja akampa pesa kadhaa. Pasipokuchelewa Alinacha akafikiria haraka cha kufanya na zile pesa akaamua akanunue vikombe atembeze auze ili hela iongezeke nyingine.
Basi Alinacha baada ya kununua vile vikombe alitembeza weee! mpaka jioni hakupata mteja yeyote, vumbi lilimjaa miguuni na alichoka sana.
Alinacha akaamua apumzike chini ya mti kidogo,chapo akapitiwa na usingizi sababu ya uchovu. Sasa akiwa usingizini ndoto ikaanza.
Aliota kauza vikombe vyote akanunua kuku. Kuku wakazaliana wakawa wengi akanunua Mbuzi, baadaye Mbuzi wakazaliana akanunua Ng'ombe.
Baada ya hapo Ng'ombe wakawa wengi akaamua fungu moja la Ng'ombe atume kama mahali ya kuolea Mke, Fungu la Pili akaona atumie kujenga na fungu la tatu atumie kuzalisha kupitia biashara.
Akiwa anaendelea kuota ndoto yake akaota yupo kwenye jumba kubwa ameshaoa sasa Mkewe alikua anamtengea chai. Kwa jeuri ya mali alizokuwa nazo akaipiga teke ile chai huku akisema
"SITAKI CHAI YA RANGI MIMI'.
Kumbe katika kurusha teke kwenye uhalisia alivunja vile vikombe alivyonunua siku ile alivyokuwa kavitenga miguuni. Kuamka kikombe kimebaki kimoja tu jamaa akaendelea kuwa maskini.
Sent using
Jamii Forums mobile app