makao makuu ya ccm
makao makuu ya ccm
Kama wewe ni mpenzi wa kinywa kitakatifu (mbege) karibia meneo ya Kitandu...Roho yako itasuuzika..
Mkuu kama wewe ni Mpenzi wa kujirusha viwanja vipo vingi tuu Moshi,kuanzia Pub Alberto,Malindi,La liga,Avencha,Glaciers nk.Na kama ni Mpenzi wa mvurugo nenda zako pale mitaa ya Kiusa stand ya Maili sita ukale mvurugo wa uhakika. Na kama ni mpenzi wa Mbuzi Katoliki panda zako KCMC au Kibolironi,na kama unapenda mambo yetu yaleeeeeee,ukiweka kambi mitaa ya Malindi na Pub Alberto utang'oa mpaka wazungu kirahisi kabisa but make sure salio linasoma mfukoni kwa ajili ya Savanah,maana hapo kuna watoto wa MUCCoBS,KCMC,Mwenge na Masoka.
Malindi imetajwa sana, panafaa kufika hapo angalau kwa kuanzia Kuburudisha macho kwanza, taratibu mengine yatajipa.
Aika meku mbe. Umenichekesha sana.Kama wewe ni mpenzi wa kinywa kitakatifu (mbege) karibia meneo ya Kitandu...Roho yako itasuuzika..
Nami nimefika leo naona mzee wa Fresh Coach anaboresha pale round about mkabala na kahawa house. Juice matunda saafi,milo nk
Wakuu shukrani wote kwa maelekezo mazuri, sasa hivi nipo Makumba bay nimepata mchemsho wa kuku. Kwa mtu ambaye anaelekeza kwenye ofisi za vyama, itabidi kumsamehe kwani lengo langu si kuchukua kadi ya uanachama, labda kama alimaanisha vinginevyo. Wengi 99.99% michango yenu nimeipokea na nitaifanyia kazi. JF ni uwanja wa elimu, tuzidi kuelimishana.