Mji kama Kahama ukitoa ule mgodi kinabakia nini pale?

Watanzania kuna nyakati tuambizane ukweli, mji kama Kahama ukitoa ule mgodi wa Buzwagi nini kinabaki pale Kahama? Kuna raia humu watataja car wash, guest house, bajaji, frame, saloon, maduka ya nguo na kadhalika, na sio Kahama tu nenda Geita then ondoa ule mgodi hakuna kinacho bakia pale Geita, kwamba ni kitu strong kwa uchumi. Kahama kidogo sana vile viwanda vya mpunga vile ndio unaweza sema kuna kitu pale ila sio zile hoteli na frame.

Hii iko kwenye miji mingi nchi hii, uwekezaji mwingi ni wa vitu kama hotel, car wash, frame na maduka ya nguo. Je, hizi tunaweza shindanisha na biashara za wachina?
Du pole sana inaonekana ulianza hii mada bila tafiti ya kutosha kuhusu kahama, kwanza kahama ni Hub ya biashara inaunganisha Shinyanga, Mwanza, Kagera, Geita, Kigoma, Tabora, Rwanda na Burundi. Soko kubwa hapa ni watu by then katika halmashauri zilizokuwa zinaongoza kwa mapato ilikuwa Ilala, Makambako na Kahama. Mji huu ni maarufu kwa uchimbaji wa dhahabu. Pia ni mji wa pili kwa mapato kati ya halmashauri za wilaya, ikitanguliwa na Kinondoni na kufuatiwa na Mufindi.

Buzwagi ni mgodi mdogo na ulifungwa kitambo, Kuna Giant Kahama Mining (Bulyanhulu) Kakola huko. Wilaya ya Kahama imevunjwa na kupatikana Msalala, Kahama na Ushetu. Vile viwanda na stores mpunga usizipuuzie hata kidogo pale unachakatwa mpunga kutoka Tabora, Kigoma, mpanda, Sumbawanga na Mbeya. Sekta hiyo imeajiri watu wengi na kuuza mchele mwingi Moshi, Arusha, Nairobi, Kigali, Kampala mpaka Sudan.

Hotel zilikuwepo kabla ya huo mgodi, wachimbaji wadogo wako wengi mno kahama kuliko sehemu yeyote TZ kama sio Afrika, Hata bus za kwenda mbali zinalalia huko
 
kukuwa kwa kahama na kutanuka haraka baada kuanzishwa kwa mgodi buzwagi na ule wa kakola ambako wafanyakazi wengi waliitaji maitaji kama guest,starehee na chakula .

chanzo ndipo kilianzia hapo kuvutia wafanya biashara wengi wakila aina kufanya biashara na wote wakajikuta wanamuingiliano wa biashara kwenye mzunguko.

hata ukija kuchunguza matajiri wengi walianza kuja kwa wingi baada ya migodi kufanya kazi kama buzwagi.

kwa kahama sasa kutokana na chanzo hiki imekuwa sehemu ya biashara si sehemu tena inayotegemea mgodi kwa sababu watu wamekuwa wengi na maitaji yamebadilika.

kahama kila kukicha idadi ya watu inaongezeka kutoka sehemu mbali mbali na nje ya nchi !

mpaka sasa kuna raia kutoka nigeria wapo hapa kahama,rwanda ndio sehemu yao kubwa kuhemea maitaji kama center yao,uganda imejikitka sana kununua karanga na mchele pamoja na wakenya wengi .

kahama imekuwa sehemu kubwa ya watu kuja kupata maitaji yao leo tabora anakuja kupata maitaji na shinyanga japo ni makao ya mkoa [emoji23].

kahama hakuna biashara utakayofanya usifanikiwe kwa sababu hakun ushindani mkubwa mfano dar yani mnafanya biashara aina moja mpo 10 na wateja watakao kuja kununua wapo wa 4 tu hapo kimbebe.

kahama kinachorudishwa nyumwa ni kutokana na shinganya kupoteza idadi na watu sana wanaokimbilia kahama japo kuwekeza sana miondo mbinu mikubwa na kuinyima kahama .

hata kipindi cha nyuma waliivunja sehemu nyingi maeneo ili ikose nguvu .

kahama ni wilaya yenye benki zote na zengine zinataka kuingia.
 
Kuna Tamthilia ya South Africa ilikuwa inarushwa ITV kwa jina la EGOLI, chini yake kulikuwa na maandishi ya kuchombeza A PLACE MADE OF GOLD
Nilikuwa sijui maana hasa ya hilo chombezo mpaka nilipofika South Africa na kwa bahati sana nikafikia hotel inayoitwa Egoli ndani ya jiji la Johannesburg

Hili jiji limejengwa na dhahabu inayopatikana hapo, Jburg haina chanzo asili cha maji maji yake yanatoka Zimbabwe
Miundombinu yake
Umeme wa uhakika
Uwekezaji wake nknk
Vyote hivi vimetokana na matumizi sahihi ya mapato yatokanayo na dhahabu yao na ndio maana likazaliwa jina la A place made of gold
Je kule Mwadui Shinyanga hali ikoje
Hapo Kahama je
Vipi kule Mirerani kwenye Tanzanite?

Madini sio mimea kwamba yakiisha utaotesha mengine la hasha yakiisha yameisha.. Je yakiisha tutabaki na nini cha kujivunia kama wenzetu?
Shinyanga a place made of Diamond?
Kahama a place made of Gold?
Mirerani a place made of Tanzanite ?

Naomba niishie hapa[emoji24]
Johannesburg wanaita nickname yake Golden City, Cape Town, Mother City.

Tanzania bila kuuteketeza ule mwenge wa kishirikina tutaangaija sana bila kujuwa tatizo ni nini kumbe ni laana.
 
Uzuri wa Kahama na Katoro ni hakuna kulala yaani hadi liamba watu wanakula Bata

Videmu unavikuta macho yamekuwa mekunduu halafu yamelegea kwa usingizi.
 
Watanzania kuna nyakati tuambizane ukweli, mji kama Kahama ukitoa ule mgodi wa Buzwagi nini kinabaki pale Kahama? Kuna raia humu watataja car wash, guest house, bajaji, frame, saloon, maduka ya nguo na kadhalika, na sio Kahama tu nenda Geita then ondoa ule mgodi hakuna kinacho bakia pale Geita, kwamba ni kitu strong kwa uchumi. Kahama kidogo sana vile viwanda vya mpunga vile ndio unaweza sema kuna kitu pale ila sio zile hoteli na frame.

Hii iko kwenye miji mingi nchi hii, uwekezaji mwingi ni wa vitu kama hotel, car wash, frame na maduka ya nguo. Je, hizi tunaweza shindanisha na biashara za wachina?
Shida wawekezaji wazawa wanachowaza ni frame na maduka. Akijitahidi ni lodge. Hakuna wazawa wengi wanaowaza kuwekeza kwenye viwanda vikubwa kama wanavyofanya wahindi au wageni wengine
 
Itabaki tu kama NZEGA ilivyo bakia baada ya Mgodi wa LUSU kuondoka....
 
Shida wawekezaji wazawa wanachowaza ni frame na maduka. Akijitahidi ni lodge. Hakuna wazawa wengi wanaowaza kuwekeza kwenye viwanda vikubwa kama wanavyofanya wahindi au wageni wengine
Mama Rehema mmiliki wa kiwanda kikubwa cha kukoboa mpunga na kupaki
mchele Pale Kahama ni wa nchi gani?.
 
kukuwa kwa kahama na kutanuka haraka baada kuanzishwa kwa mgodi buzwagi na ule wa kakola ambako wafanyakazi wengi waliitaji maitaji kama guest,starehee na chakula .

chanzo ndipo kilianzia hapo kuvutia wafanya biashara wengi wakila aina kufanya biashara na wote wakajikuta wanamuingiliano wa biashara kwenye mzunguko.

hata ukija kuchunguza matajiri wengi walianza kuja kwa wingi baada ya migodi kufanya kazi kama buzwagi.

kwa kahama sasa kutokana na chanzo hiki imekuwa sehemu ya biashara si sehemu tena inayotegemea mgodi kwa sababu watu wamekuwa wengi na maitaji yamebadilika.

kahama kila kukicha idadi ya watu inaongezeka kutoka sehemu mbali mbali na nje ya nchi !

mpaka sasa kuna raia kutoka nigeria wapo hapa kahama,rwanda ndio sehemu yao kubwa kuhemea maitaji kama center yao,uganda imejikitka sana kununua karanga na mchele pamoja na wakenya wengi .

kahama imekuwa sehemu kubwa ya watu kuja kupata maitaji yao leo tabora anakuja kupata maitaji na shinyanga japo ni makao ya mkoa [emoji23].

kahama hakuna biashara utakayofanya usifanikiwe kwa sababu hakun ushindani mkubwa mfano dar yani mnafanya biashara aina moja mpo 10 na wateja watakao kuja kununua wapo wa 4 tu hapo kimbebe.

kahama kinachorudishwa nyumwa ni kutokana na shinganya kupoteza idadi na watu sana wanaokimbilia kahama japo kuwekeza sana miondo mbinu mikubwa na kuinyima kahama .

hata kipindi cha nyuma waliivunja sehemu nyingi maeneo ili ikose nguvu .

kahama ni wilaya yenye benki zote na zengine zinataka kuingia.
wewe upo.kahama
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom