Mjengoni: Nani aliyesema "Fungeni Milango Tupigane"? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjengoni: Nani aliyesema "Fungeni Milango Tupigane"?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanangwa, Apr 24, 2011.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Ninaomba kujuzwa.
   
 2. Architect E.M

  Architect E.M JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 813
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  ni mbunge wa arusha mjini kupitia CHADEMA, mheshimiwa GODLESS JONATHAN LEMA
   
 3. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,388
  Trophy Points: 280
  how much sure are u?
   
 4. Architect E.M

  Architect E.M JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 813
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  nilipata habari kutoka kwenye gazeti la raia mwema, the following day afta huyu mheshimiwa kuongea hivyo.. Halafu pia hiyo kauli ilishajadiliwa humu pia, na wwatu waliokua mjengoni wenyewe walituhabarisha kuwa ni lema,,,
   
 5. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,388
  Trophy Points: 280
  asante mkuu sikua na taarifa hizi
   
 6. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  inalazimu sometimes, hili bunge letu ovyo, ndo mana hata wakenya, waturuki, wakorea etc walizichapa. Itampa adabu yule mama la fisadi
   
 7. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  ujue bunge letu jinsi lilivyojaa mambumbumbu mkono lazima upigwa ili kuleta heshma na umakini kwa baadhi ya mazuzu hasa fr ccm
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mwanzo alimwaga ugali Lucinde a.k.a Bajaj - CCM Mtera bunge la January, then April Lema -cdm Arusha akamwaga mboga.
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hii kauli imeshatolewa na wabunge wawili tofauti Lema na Lusinde, funny enough ya mmoja (CDM) inaonekana uhuni, na ya yule tena aliyeitamka akiwa amesimama ilionekana ni ujasiri
   
 10. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni mbunge wa ccm kulingana na bandiko hili toleo la leo la Tanzania Daima
  _______________________________________________________
  Wabunge wa aina hii hawatufai-Prudence karugendo

  KWA mara ya kwanza tangu tuwe na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumemsikia mbunge akitoa kauli ya ajabu bungeni.
  Ni mbunge kijana aliyepaswa kuwa na fikra mpya za kuliingiza bunge letu kwenye karne ya 21 likiwa na mwonekano wa mabadiliko ya kisayansi na teknolojia.

  Lakini mbunge huyo kupitia chama tawala, CCM, bila shaka baada ya kuwa hana la kuchangia kwenye mjadala uliokuwa unaendelea, akaamua kupaza sauti akitaka milango ya Bunge ifungwe ili waheshimiwa wabunge waanze kutwangana baada ya kutofautiana kwa hoja.

  Dai lake la kutaka milango ifungwe sio la kutaka faragha ilivyoonekana, kwamba wabunge wasionekane wanapigana, sababu mbunge huyo anaelewa kwamba mkutano wa bunge unaonyeshwa moja kwa moja kwenye luninga na kutangazwa moja kwa moja kupitia kwenye redio.
  Lengo lake la kutaka milango ifungwe inawezekana lilikuwa ni kutaka kuwazuia wagombolezeaji ambao wangelazimika kuingia ndani ya ukumbi wa bunge ili kuinusuru hali ya mambo. Hapo kuna mambo ya kuyaangalia na kuyatafakari.

  Ni kwamba inawezekana mbunge huyo alikurupuka usingizini, kama ilivyo kawaida, na kutoa kauli hiyo tata kutokana na upande wa kambi yake kuelemewa na hoja za msingi zilizokuwa zinatoka upande wa pili, kwenye kambi ya upinzani.

  Sasa kwa fikra finyu mheshimiwa huyo akaona suluhisho la haraka haraka la kuzibomoa hoja za wapinzani ni kupigana akiwa ameegemea kwenye mambo mawili:
  La kwanza yeye ni kijana anayejiona bado anazo nguvu za kupigana, na la pili ni wingi wa wabunge wa chama chake, chama tawala.
  Ni kwamba wingi wa wabunge wa chama tawala hauwawezeshi wabunge hao kujenga hoja zenye nguvu, pengine ndiyo maana mbunge huyo akaona hili la pili, kupigana, lingeweza kuzaa matunda aliyoyategemea, matunda yanayofanana na wingi wao.

  Lakini hata hivyo siwezi kumlaumu mbunge mhusika kwa kituko hicho. Naamini alifanya kitu kilicho kwenye uwezo wake. Kama uwezo wake ni kupigana, tuseme huo ndio mchango wake anaoweza kuutoa bungeni kwa niaba ya wapiga kura wake.

  kumtegemea mbunge wa aina hiyo afanye kitu kilicho tofauti na hicho itakuwa ni kumuonea. Cha kuangalia ni mfumo uliomwezesha mpiganaji huyo kuipata fursa hiyo.

  Wabunge kwa hapa nchini wanapatikana kupitia kwenye vyama vya siasa. Na kila chama kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea nafasi hizo za ubunge.

  Kila chama kinajua namna ya kuwapata baadhi ya wanachama wake kinaowaona wanafaa kuwa wawakilishi wa wananchi kabla ya kuwapambanisha na wagombea wa vyama vingine. Kwahiyo tunachokiona bungeni kwa sasa ndiyo matokeo ya umakini wa kila chama.
  Wapo wanaoshangaa kumuona mcheza tunguli, kwa mfano, akiwa bungeni kama mwakilishi wa wananchi katika karne hii ya 21. Lakini kwa upande wangu namtetea sana mtu huyo maana umakini wa chama chake ndiko ulikofikia.

  Kapitishwa na chama chake na kafanyiwa kampeni ya nguvu na chama chake, kashinda, iwe kwa uhalali au kwa kuchakachua, na sasa ni mbunge!

  Upungufu wowote atakaouonyesha bungeni sioni kama anastahili lawama, kwa sababu ni lazima yeye afanye kilicho ndani ya uwezo wake. Akiamua kuzomea sawa, akiamua kupiga mayowe sawa, maadamu chama chake kilimuamini kwahiyo kumhukumu kwa hilo tutakuwa hatumtendei haki hata kidogo.

  Kwa sasa hivi bunge limechangamka kutokana na kugawanyika katika sehemu mbalimbali. Kama Spika alivyowaasa wabunge jumamosi iliyopita, bahati nzuri au mbaya, yanayotendeka ndani ya ukumbi wa bunge kwa sasa tunayaona na kuyasikia moja kwa moja bila kusubiri kuletewa taarifa.

  Wanaosinzia tunawaona, wanaochangia hoja tunawaona, wanaoshangilia tunawaona, wanaozomea tunawaona na wengine kazi yao ni kugonga tu meza muda wote wa vikao vya bunge hasa wakisikia anayechangia ni wa kambi yao. Hiyo haijalishi kama kilichosemwa na mtu wa kambi yao kina mashiko au la.

  Hayo yote yamechangiwa na chama tawala kilichojivua uzalendo na kuvaa gamba gumu ambalo kwa sasa kinaanza kuliona kuwa halifai.
  Ni gamba hilo lililokuwa linakishawishi chama hicho kijaze watu bungeni bila kujali watu hao watakuwa na mchango gani katika ustawi wa nchi yetu.

  Kwa upande wa chama hicho kilichokuwa kinatiliwa maanani ni idadi ya wabunge. Nina mashaka kama hekima na uadilifu pamoja na uwezo wa mtu, weledi, wa kukokotoa masuala mbalimbali ya kijamii, kitaifa na kimataifa, ili kupata uwiano wa jamii yetu katika dunia hii tuliyomo vilikuwa ni vitu vinavyopewa kipaumbele.

  Naweza kusema kwamba CCM hii iliyovaa gamba ni tofauti na CCM ya miaka 16 iliyopita, sababu nakumbuka mwaka 1995, wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huo, muasisi wa chama hicho, Mwalimu Nyerere, alidiriki kumfanyia kampeni mgombea ubunge wa chama cha upinzani.

  Alifanya hivyo katika jimbo mojawapo la mkoani Mara baada ya kuutilia shaka uadilifu wa mgombea wa chama chake. Mwalimu alijali zaidi uwezo na uadilifu kuliko ushabiki wa chama. Alikuwa na uzalendo zaidi kwa nchi kuliko uzalendo wa chama.
  Lakini baada ya CCM kuvaa gamba tukamshuhudia mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete akiwanadi kwa wapiga kura watuhumiwa waliokuwa na kesi za kujibu mahakamani!

  Bila haya mwanyekiti wa CCM akawa anawashawishi wapiga kura wawachague watuhumiwa hao na wakati mwingine akifikia hata kuziponda kesi zao zilizokuwa zinawakabili mahakamani!

  Hapo ndipo tuamini kwamba gamba hilo, ambalo kwa sasa CCM inadai kuwa imeamua kulivua, lilikuwa limekifikisha mahala pabaya chama hicho.

  Kama Nyerere alikataa kumnadi mwana CCM kwa hisia tu kwamba uadilifu wake ulikuwa na walakini, je, ingekuwaje kama angekuwa anaelewa kwamba mhusika ana kesi ya kujibu mahakamani? Kweli gamba hili lilikuwa chafu sana.

  Fikiria matatizo yanayoikabili nchi yetu kwa wakati huu, tena matatizo yanayotokana na ukosefu wa mpangilio wa kutoelewa ni wapi tuweke vipaumbele vyetu kutokana na rasilimali tele za nchi yetu.

  Wawakilishi wetu badala ya kukaa kwa hekima na kujadiliana nini kifanyike anajitokeza mmoja wao na hoja ya kwamba wafunge milango ili wakapigane!

  Huyo ni mbunge wa chama tawala, chama kilichokuwa kimevaa gamba gumu. Sitaki kumtaja mbunge huyo, anajielewa na wabunge wenzake wanamuelewa.

  Ni namna gani mtu wa aina hiyo amepata fursa ya kuingia bungeni kama mwakilishi wa wananchi? Hilo ni swali linaloweza kujibiwa na chama chake. Sababu inaonekana ni mwendelezo uleule wa ukosefu wa mpangilio na kushindwa kuelewa sehemu gani ipewe kipaumbele gani.
  Kama tulivyo na rasilmali tele lakini tukishindwa kuzitumia huku tukilia na umasikini, wakati huo huo watu kutoka nje ya nchi wakipigana vikumbo kuja kuzoa utajiri wetu huo, ndivyo ilivyokuwa kwa huyo mheshimiwa aliyetaka kupigana bungeni wakati pale si mahala pake.
  Mpiganaji anaingizwa bungeni badala ya kuwekwa sehemu ambayo angepigana na kuliletea heshima taifa letu badala ya fedheha aliyotaka kuifanya.

  Mara nyingi wanamichezo wetu wamekuwa wakienda kwenye mashindano ya kimataifa na kurudi mikono mitupu wakati wenzao wa nchi jirani wakiwa wameelemewa na uzito wa medali wanazokuwa wamezizoa kwenye mashindano hayo.

  Sisi hilo tunaliona la kawaida kwa vile tunaamini kwamba hata kupigana hatuwezi. Kumbe wale ambao tungewapeleka wakapigane kwenye mashindano ya kimataifa na kutuzolea medali.

  watu wa aina hii hatupaswi kuwapeleka bungeni ambako hawana la kuchangia zaidi ya kuonyesha kwamba wao ni wapiganaji mahiri. Ukosefu wa mpangilio na utoaji wa vipaumbele.

  Funga milango tukapigane! Hiyo ndiyo kauli ya mbunge aliyetumwa na wananchi wenzake ili akawasemee kero zinazowakwaza katika kupambana na maisha.

  Wanahitaji huduma bora za mawasiliano, huduma bora za afya, maji safi na salama ya matumizi ya ndani, elimu bora kwa watoto nakadhalika nakadhalika.

  Waliyemtuma kasahau kil kitu ila kipaumbele chake ni kutaka kupigana bungeni! Hilo ni jambo tunalohitaji kulitafakari, si la kuacha likapita hivihivi kama tulivyozoea Watanzania.

  Tunapaswa tujiulize mbunge akipigana bungeni wapiga kura wake wananufaikaje?
  Kitendo hicho cha kishujaa, bila shaka, kulingana na imani ya mhusika inavyojionyesha, kingewafanya wapiga kura wake wasahau matatizo ya barabara?

  Kingewafanya wasahau ukosefu wa huduma bora za afya? Kingewaondolea matatizo yote yanayowakabili katika mzunguko mzima wa maisha? Kama jibu ni hapana kwa nini mbunge huyo wa CCM alikifikiri kitu hicho cha aibu kwa Bunge letu?
  Sidhani kama ni rahisi kuamini kwamba yule ni mtu wa kiwango cha kufanya mambo bila kufikiri.

  Au lengo lake lilikuwa ni kuwatisha wabunge wenzake, hasa wa upinzani, wasiweze kujadili masuala nyeti ya nchi kwa weledi ulio wazi na badala yake wakubali kuburuzwa na wenzao wanaotegemea wingi wao kufanikisha mambo yasiyo na tija kwa nchi na wananchi?

  Mwisho niseme kwamba kama kweli CCM imedhamiria kujivua gamba basi ihakikishe inajisafisha kabisa kwa kujivua hata hivi vijigamba vidogo vidogo ambavyo vikiachwa ni lazima viendelee kuifanya ionekane ina madoadoa kama vile imeugua ukurutu.
  Kwa mantiki hiyo nisingetegemea mbunge huyo aendelee kushiriki vikao vya Bunge letu, sababu wabunge wetu tunawapenda, hatukuwatuma wakapigane.
  Hatutaki warudi na ngeu au chongo, ila tumewatuma wakayajadili mahitaji yetu kwa weledi na wazi. Anayetaka kupigana ni bora tukamtafutie nafasi kwenye timu yetu ya olimpiki. Wasalaam.
   
 11. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli iko siku si nyingi ngumi zitaibuka,Speaker wetu ni kihiyo wa sheria hivyo inamuwia ngumu sana kubaini makosa ya kisheria,na wabunge wa CCM hasa wanasheria hawamsaidii hata kidogo kutafsiri sheria,angalia kama suala la uhuru wa mahakama sasa wapo wanasiasa wakuu wa mikoa,wanafuata nini humo,mswada ulipokuwa unapitishwa CCM walishabikia na kudharau hoja ya Lissu ambaye aliungwa mkono na mtoto wa mkulima mpaka mwisho na kuzidiwa kwa kura za wingi wa CCM,hii imefika mahala ambapo sasa ni ngumi tu zinahitajika.
  Msekwa aliposema Speaker anatakiwa kuwa mwanasheria ndio kilichotakiwa,wao CCM na Msekwa waliamua kufunika kombe sasa wanaaibika kwa kupitisha mishwada iliyo hovyo kuliko yote katika maisha ya Tanzania.
   
 12. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Bata akinya kaharisha
   
Loading...