Mjane aliyemwaga machozi mbele ya Rais Magufuli akabidhiwa nyumba yake

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Mjane Aliyemwaga Machozi Mbele ya Rais Magufuli Akabidhiwa Nyumba Yake

Hatimaye mjane aliyemwaga machozi mbele ya Rais John Magufuli akidai kudhulumiwa mali ya urithi, amepewa nyumba na shamba baada ya Mkuu wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Crispin Meela kusuluhisha mgogoro wa umiliki wa mali hizo.

Hivi karibuni akiwa mjini Babati, Rais Magufuli alimuagiza Meela ahakikishe mjane huyo, Mwanaidi Mussa anapewa mali zake ikiwamo nyumba na shamba zilizokuwa zinadaiwa kuchukuliwa na mke mdogo kinyume cha sheria.
Meela alimkabidhi nyumba na shamba la ekari 2.5 mjane huyo juzi na kuagiza mke mdogo kama hakuridhika na uamuzi, akakate rufaa mahakamani.
Meela pia aliwataka wananchi kuacha kurubuniwa na watu wachache wenye maslahi binafsi na badala yake wafuate maelekezo yanayotolewa na vyombo vya sheria.

“Migogoro ya mirathi imeendelea kukithiri katika maeneo mengi nchini kutokana na watu kutofuata sheria za mirathi na wengine wakitaka kunufaika na mali zinazoachwa na marehemu,” alisema Meela.

Mwanaidi ambaye amezeeka, alidai kwa muda mrefu amewaomba viongozi wa Serikali ya mtaa anaoishi wamsaidie, kutatua tatizo lake lakini walimpuuza.
Mke mdogo, Asia Musa alidai kuwa nyumba hiyo aliyokabidhiwa Mwanaidi, aliijenga na mumewe kauli ambayo ilikinzana na ya mke mkubwa aliyedai kuwa wakati Asia anaoelewa alikuta nyumba ameshaijenga na mumewe.

My Take;
MaDC na MaRC tunaomba msimamie haki katika maeneo yenu ninaamini kuna wajane,wanyonge na mayatima wengi wanateseka.
 
Kweli wajane na watoto wao wanateseka sana juu ya mali za urithi! Hata mimi naona na naogopa sana kwenye ukoo/familia yetu kwa sasa wapo kimya likitokea la kutokea utawaona wanajongea na kauli zao tata! Wakati wa ups and down hutawaona wakisaidia hata kwa ushauri! Ila mkubwa wa familia akilala....utawaona wamejaa waanze kuwawekea masharti ya kufuata!
 
Ampeleke mahakamani Meela siyo mahakama, ni siasa hizo tu!

Huo sio utawala wa sheria. Meela ametumia vigezo gani?

Meena amempa kutumia vigezo gani?
Watanzania tuna tabia ya unafik sana....
Huyo mjane alipo dondosha chozi kwa kudhulumiwa, mlisema sana na kutoa maneno taka kwa viongozi wa serikali kutoingilia swala la mama huyo.
Leo mama huyohuyo mjane amerudishiwa malizake kwa wasimamizi wa serikali kuingilia kati swala la kudhulimiwa mama huyo, tena bado mnaongeeeea.
Kwakweli inafika wakati nashindwa kujua waTanzania tunataka nini sababu kilakitu tunapingatuuu
 
Meela siyo mahakama! Ni kuvunja katiba, chombo cha kutoa haki ni mahakama na si Magufuli wala Meela! Take note of that! Unajuaje kama mama yule ndiye mwenye haki? Au kwa vile alitoa machozi!
 
Kwa vipi mgogoro wa mirathi uamuliwe na DC!!? Ninavyojua mimi mirathi ni suala la kimahakama, yaani mirathi ifunguliwe na uamuzi wa kugawa mali za marehemu ufanywe kwa usimamizi wa mahakama. Halafu hao kama ni waislamu nadhani siku hizi kuna kadhi court.
 
Meela siyo mahakama! Ni kuvunja katiba, chombo cha kutoa haki ni mahakama na si Magufuli wala Meela! Take note of that! Unajuaje kama mama yule ndiye mwenye haki? Au kwa vile alitoa machozi!
Sijui mgogoro huu ulianzia wapi....Je mke mdogo alimilikishwa hizo mali na mahakama au alijimilikisha kinguvu/fedha?
 
Yumkini akina mama hawa ni wa imani ya kiislamu; na uislamu una sharia zake katika suala la mirathi na wakf; na kwamba tayari kadhi yupo na anatimiza majukumu yake nchini. Kwa kuwa suala la mirathi na wakf ni suala la kiimani zaidi hususan katika uislam; Je, maamuzi haya ya serikali sio kuingilia dini? Itakuwaje endapo mke mdogo ataamua kufuata mkondo wa dini/kadhi kutafuta haki yake? Naona migongano isiyo ya lazima kati ya serikali na dini ikija kwa mbaali kwenye suala hili.

Kitu ambacho Serikali ilipaswa kufanya ni kuwashauri akina mama hawa hususan yule aliyelia kufuata taratibu stahiki katika kupata haki zao na kwa kumsaidia ingeweza kumwekea wakili au kumwomba Kadhi Mkuu kuingilia suala lile na kama ingeshindikana katika mkondo wa Kadhi basi mkondo wa sheria za nchi ufuatwe. Machozi yasiwe sababu au ishara kwamba aliyeyatoa ndiye mwenye haki. Huo ndio utawala wa sheria japo una machungu na gharama zake.
 
Meela siyo mahakama! Ni kuvunja katiba, chombo cha kutoa haki ni mahakama na si Magufuli wala Meela! Take note of that! Unajuaje kama mama yule ndiye mwenye haki? Au kwa vile alitoa machozi!
Huu Ni upumbavu haki haiobwi Na wala haitolewi Na mahakama haki inachukuliwa hata kwa gharama zozote
 
Sijui mgogoro huu ulianzia wapi....Je mke mdogo alimilikishwa hizo mali na mahakama au alijimilikisha kinguvu/fedha?

Hakuna ajuaye. Na ndio maana kuna vyombo vya kutoa haki kwa kufuata taratibu na sheria za nchi.
 
Back
Top Bottom