Mjane aeleza alivyotishiwa maisha na watendaji wa serikali akidai haki yake ya ardhi Muleba

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
mjane.png

Mama mjane Bi.Modesta Mukurasi anayemiliki shamba la urithi lililonunuliwa na wazazi wake shilingi tano mwaka 1937 ameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi kati yake na watendaji wa serikali ya kijiji cha Bushumba wilaya ya muleba mkoa wa Kagera wanaotishia usalama wa maisha yake kwa vitisho kuwa watamuua endapo ataendelea kudai shamba lenye ukubwa wa hekari 30 ambalo limeuzwa kwa wawekezaji kinyemela.

Amebainisha hayo katika kikao cha viongozi wa Chama cha Mapinduzi, watendaji wa serikali wilaya ya Muleba katika ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa Alhaj Abdallah Bulembo iliyolenga kufafanua mabadiliko ya katiba ya chama cha mapinduzi na kutoa shukrani kwa wananchi kwa kumchagua Rais Dkt John Pombe Magufuli kuiongoza nchi.

Kutokana na malalamiko hayo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa Chama cha mapinduzi Mhe.Alhaj Abdallah Bulembo amelazimika kumkabidhi kwa uongozi wa serikali ya wilaya ya Muleba mama huyo ili asaidiwe kupata haki yake.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom