Mjamzito aibiwa mtoto temeke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjamzito aibiwa mtoto temeke

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kaitaba, Oct 28, 2009.

 1. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mwanamke mmoja (jina kapuni) amefika temeke hospitali jana na kudai kuwa mjamzito, na baada ya muda kidogo akampigia simu mme wake kuwa amejifungua mtoto, lakini daktari wake amemwamia kuwa mtoto kafariki na kaondoka na kichanga hicho kusikojulikana, (hisia ikatawala kuwa daktari kaiba kichanga hicho)

  Mme wake alipofika tmk hosp, aliwaeleza wauguzi kuwa mkewe alikuwa mja mzito, ktk kutafuta ukweli, huyo mwanamke alipimwa na vipimo vimeonesha kuwa hajawahi kushika mimba zaidi ya miezi 12 iliyopita,

  Unamshauri nini mme wake? na huyo mama yuko chini ya ulinzi sasa
   
 2. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ....Udaku! Jina kapuni kwa suala la kama hili? au ni wewe??
   
 3. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Tumsaidie huyu jamaa, kwa vile vijana wangu wanazunguka kutafuta habari na kuzisambaza, ebu nunua gazeti la darleo, watakuwa wameandika maana na wao wameichukua, ila wao wameandika kwa urefu zaidi ikiwa ni pamoja na majina
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Pale kwenye ukumbi wa Hoja pangefaa zaidi kwa bandiko hili...
   
 5. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  unaandikia magazeti yale ya kombora? risasi? au? ushauri gani hapa, na tittle ya kidaku
   
 6. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yakiwafika haya, mtanikumbuka
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duh yaani mwanaume alikuwa anahumia tambala bila yeye kujijua au?
   
 8. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Habari ndo hiyo, je akiachiwa huru mme ampokee au amwache?
   
 9. M

  Msindima JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mmhh jamani hii nayo kali,mbona tena napata maswali mengi ya kuuliza,ntampata kweli mtu wa kujibu haya maswali? habari inasema huyo mama baada ya kupimwa imeonekana kuwa hajabeba mimba katika kipindi cha miezi 12,sasa huyo mume wake nae ina maana katika kipindi cha huo ujauzito hakuwahi hata kula chakula cha usiku? mbona hii habari inatia shaka?
   
 10. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kwa wanawake wajanja na wana lengo baya, wanahama na chumba miezi yote 9, kwa madai kuwa daktari au mganga wa kienyeji kakataza kufanya/kulala na mme wake,

  na mme kwa vile anataka mtoto inabidi akubali
   
 11. M

  Msindima JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Jamani bado nakua na maswali sana anyways let me leave this issue as it is.
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Anaswa akijidai amejifungua [​IMG] [​IMG] [​IMG] Written by Administrator Wednesday, 28 October 2009 11:31 Na Waandishi Wetu, Temeke/ Polisi

  MWANAMKE Maua Ally (29), mkazi wa jijini, amejikuta akiangukia mikononi mwa Polisi baada ya kupiga mayowe akilalamika kuwa mtoto wake aliyemzaa katika Hospitali ya Temeke ameibwa na watu wasiofahamika.

  Akizungumza na gazeti hili leo asubuhi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Liberatus Sabasi, amesema mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma za kutoa taarifa za uongo.

  Akizungumzia sakata hilo, Kamanda Sabasi amesema Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo Nusura Simba (49), kuwa kuna mwanamke analalamika kuwa ameibiwa mtoto.

  Amesema mwanamke huyo alidai kuwa alifika katika hospitali hiyo akiwa anaumwa uchungu na alipokewa na daktari kisha kupelekwa chumba cha kuzalisha, ambapo alijifungua mtoto na kupokelewa na madaktari.

  Amedai kuwa mwanamke huyo alidai kuwa cha kushangaza baada ya kutoka chumba hicho hakumuona mtoto wake na ndipo alipoamua kutoa taarifa kwa uongozi wa hospitali.

  Baada ya jeshi la polisi kupokea taarifa hizo walifika hospitalini hapo na kumhoji mwanamke huyo ambaye alikiri hakujifungua wala hakuwahi kuwa mjamzito.

  Alidai kuwa aliamua kutoa taarifa za uongo kwa sababu mume wake amekuwa akimshinikiza kubeba mimba.

  Kamanda Sabasi amesema kutokana na taarifa hizo, uchunguzi wa kitaalamu ulifanyika dhidi ya mwanamke huyo na walibaini kuwa taarifa anazozitoa ni za uongo.

  Amesema kuwa mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

  Wakati huo huo, kibaka maarufu anayetamba kwa uporaji wa pochi za wanawake katika mataa ya Nyerere, Kawawa na Chang'ombe, Hamad Mohamed (24), hatimaye amenaswa na Jeshi la Polisi.

  Kamanda Sabasi amesema mtuhumiwa huyo anasifika kwa uporaji wa pochi na simu za mikononi, jambo ambalo limekuwa kero hasa kwa abiria wanaopita maeneo hayo.

  Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.


  Source Dar leo.
   
Loading...