Mjadala waDowans(ITV) na Audi alteram partem

Mjadala ulikuwa mzuri. Kuna mambo muhimu yalijitokeza pia. Sheria za uandishi wa habari zilikiukwa. Ili habari iwe habari mwandishi utetezi in au ukweli au maslahi ya umma. Kuna tatizo la maadili katika nchi. Matokeo yake ni uandishi usiojali sana ukweli bali maslahi ya umma. Mfano. Mwanahalisi alivyotaja mafisadi 11 akiwemo mh. Rais kwa kuwaanika hadharini kwa kuwasikia kwa Mh. Slaa, alifanya makosa. Kilichomlinda ni maslahi ya jamii. Jana kulifanyika makosa. Kuwataja Mh. Lowasa, Rostam, Chenge, na wengine kwa namna walivyotajwa wananchi wanaweza kubeba mawe.

Kitakachoweza kuisaidia itv na mtajaji pamoja na mmiliki wa itv wasishitakiwe ni maslahi ya umma. Hili inaruhusi maslahi ya umma yavunje maadili ya uandishi. Hilo sio jamba jema.

Ni kama kauli ya Wah. samweli sita/Mwakyembe. Ukiiangalia kwa undani (kwani kufikiri ni kugumu) wanapashwa wajiuzulu. Lakini kutokana na tatizo la kiutawala (Gavernance) watalindwa na maslahi ya umma. Umma katika suala hili litawalinda na kuwalazimisha kujiuzulu ni kuweka mafuta katika moto. Hali ndo hiyo.

Nitakuja na mapendekezo baadaye siwezi andika mengi. Watanzania wengi ni wavivu kusoma.

 
Asante sana nyambala ni ukweli usiokwepeka mchawi lazima atafute na wanatakiwa wajulikane na hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi yao haiwezekani eti tulipe na maisha yaendelee tu no way..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…