Mjadala wa sera mpya ya vijana tushiriki

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Ndugu Makamaradi,

Napenda kuwaalika katika mjadala mpana na makini wa kujadili sera mpya ya vijana ambayo imezinduliwa mwaka huu 2008 ikiwa ni maboresho ya sera ya mwaka 1996! Kwa wale magwiji wa kujadili tunawaomba waje na hoja zao nzuri kwa manufaa ya vijana wa Tanzania .Mjadala huu ikiwa ni mfululizo wa mijadala ya DIRA inayoendeshwa na asasi ya TYVA kupitia idara yake ya Lobby, Advocacy and Networking-LAN utafanyika mnamo tarehe 29.08.2008 katika ukumbi wa Rombo Green View Hotel saa 2.30 asu mpaka 7 mchana!Mada itatolewa na mchokoza mjadala Ndg. Chambi Chachage mtafiti na mchambuzi wa sera wa kujitegemea.Napenda kuwaomba kwa wenye kupenda kuhudhuria mjadala huu kutuma udhibitisho wao wa kushiriki mapema kabla ya saa 12:00 jioni siku ya 27.08.2008 jumatano kupitia 0755-45 97 83 ama 0732- 36 13 37 ama barua pepe: tyvavijana@yahoo. com. Hii ni muhimu sana kwa kutuwezesha maandalizi ya tukio.Kumbuka nafasi zimebaki chache! Hatutahusika na wanachama ambao hawajatoa uthibitisho wa kushiriki kwao.Natumai tutashirikiana vyema kama tunavyoshirikiana siku zote!Wenu,

Michael Dalali
 
Back
Top Bottom