Mjadala Upi ni muhimu kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii?

Makusudically

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
2,203
1,235
Naomba kujulishwa kwa undani juu ya haya yafuatayo:

Mitandao imekuwa ikiongelea zaidi juu ya RC Makonda na muda mwingi unatumika kuongelea matukio tu badala ya issue relevant to development.

Kwanini mitandao isiongelee zaidi kuhusu Matukio muhimu kama yale ya Wabunge kuwagonga na gari wananchi na kuwaua tena kwenye Zebra crossing na wananchi hao ni watoto yatima? Mfano huko Katoro mkoani Geita kuna mbunge mmoja (jina limehifadhiwa) alimgonga mwananchi na kumsababishia ulemavu wa kudumu lakini hayo hayaongelewi.

Kuna kiongozi mmoja alikwepa kodi hadi Bil.1 nzima na kuwasababishia Wananchi kukosa huduma za kiafya, maji safi na salama, huduma za kielimu. Watu kama hawa mitandao ingewalaumu sana. Lakini mitandao inahangaika na kumbatiza RC Makonda jina la Bashite.

Inashangaza!!
 
Tujadili Nchi ya Botswana wanawezaje kuchimba wenyewe Madini yao!!!!!!! ,,,,GDP ya botswana more than 50% government revenue driven by Mining & Mineral Processing Je hapa kwetu wanabeba mchanga na kwenda Ku process kwao,tusiwe MAPOYOYO. IF Aikud a Presidaaaa.
 
Tujadili jinsi gani kijana wa kitanzania anaweza kujiongezea kipato na kujinasua kiuchumi bila ya kutegemea wanasiasa. [HASHTAG]#siasa[/HASHTAG] tupa kuleee tujitafutie maendeleo yetu wenyewe!!
 
Jaman kuna vitu vinasononesha kama kuna watumishi walitimuliwa kwa kuwa na vyeti feki kwani ni iwe kwao tu hili linafanya mjadala uwe mrefu maana tunasota mitaani wakati MTU analindwa kwa kodi zetu huku analalamikiwa ana vyeti feki
 
Mambo ya mahusiano katika jamii yamekuwa ndio kinara mitandaoni kwa sababu ndio yanamgusa mtumiaji moja kwa moja....Hayo mengine mbwembwe Tu.
 
Back
Top Bottom