Aristolicius
Senior Member
- Mar 3, 2012
- 110
- 39
Habari kwa wote!
Kufuatia matatizo yanayoendelea nchini hasa katika swala la uchinjaji wa vitoweo na kukua kwa chuki baina ya Wakristu na waislamu ni dhahiri sasa ni wakati muafaka wa serikali kuchukua hatua thabiti kumaliza haya matatizo.
Kwa upande wangu naona serikali imekua ikiyachukilia ki uwepesi matatizo haya huku ikiwa ni dhahiri hayakuanza leo,kuna vurugu za mwembechai wote tunazikumbuka,zamani wakati mimi nipo shule wanafunzi wote tulikuwa tunavaa sare sawa ila kuna kipindi serikali ikaona hii haifai shule moja sare ni tofauti waislamu wakaruhisiwa kuvaa sare zinazowatambulisha huku wa RC wakiacha rozari zao nje waliambiwa zificheni ndani shule sio sehemu ya kuonyesha dini zenu wote mnatakiwa kuwa sawa,utofauti huu wa mavazi ukaendelea vyuoni wanafunzi wakakatazwa kuvaa mavazi fulani wakiambiwa yanapingana na maadili(sijui maadili gani)chuo cha Mwl.Nyerere ikafika hadi dada zetu wakilazimishwa na wananchi kuvaa hijabu bila kujali dini zao,serikali ikawa kimya wengine wakachukulia kama chuki za wavisiwani kwa wabara kumbe ni fujo za kidini zinamea.
Hayo yote yalijenga nafasi(gap) kati ya dini hizi mbili na kila kukicha yakazaa kitu kipya na sasa kilichozaliwa ni mgogoro wa uchinjaji wa kitoweo na viongozi wetu wanalichukulia kiuwepesi wepesi vyama vya siasa navyo kimya vingine vinashindwa kutoa kauli vikiogopa kuitwa vya kidini,vingine vinatoa kauli za lawama baada ya kutoa suluhu,vingine vinaogopa kupotezea umaarufu miongoni mwa wanachama wa dini fulani?
Kwangu mimi nijadili suluhu kadhaa na ugumu wake
1.kufuata katiba:kikatiba hakuna dini iliyooidhinishwa kuchinja wala iliyokatazwa hivyo tukiamua kufuata katiba wote tutaruhusiwa kuchinja ila tatizo linakuja je tutakuwa tumesolve tatizo?sidhani ,kimtazamo watu watakubali kwa shingo upande sababu hili suala si la kidini pekee linaendeshwa na maslahi ya kibiashara zaidi na pia kuna chuki baina ya waumini wa dini tajwa swala kuchinja sidhani ni jambo kubwa hapo swala ni kuchoka kupelekeshwa.
2.Kuundwa kwa nembo ya uhalal(halal sticker) kwenye nchi za wenzetu kumekuwa na nembo ambazo zimekuwa zikiwekwa kwenye vyakula vilivyoaandaliwa kwa desturi na ibada ya kiislamu ili kuwawezesha waweza kufuata ibada yao hivi kwanini hili lisifatwe kwetu?ila hili pia ni linaweza likawa gumu ikiwa kisa cha yote haya ni chuki baina ya watu.
3.Mjadala wa kitaifa:nadhani ni wakat taifa liandaa mjadala wa kujadili tofauti hizi kabla hazijatufikisha mbali kama tuliweza kwa vurugu za visiwani je tutashindwa katika hili?
Wito wangu:ifike wakati watanzania tunapojadili matatizo yetu tupendekeze suluhu na sio kuishia kutoa lawama au ku practise party politics(kufanya siasa za vyama) katika matatizo yetu ,wewe kama mtanzania unashauri nini kifanyike?ni wapi tulipokosea?je ni kweli tatizo ni hili tunaliona au kuna ajenda nyuma yake?maswali kama haya yatatusaidia kutafuta suluhu ya kweli.
NB.samahanini kama nitakuwa sijafuta taratibu za uandishi mimi sio mwandishi mtaalamu(professional).