mjadala mpana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mjadala mpana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mchange, Aug 24, 2009.

 1. Mchange

  Mchange Verified User

  #1
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 156
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  HIVI MOROGORO TUMEKOSA NINI JAMANI SISI MBONA HIVI?
  MZERU NAOMBA MAJIBU TAFADHALI
  Na:Habibu Mchange

  Nikiutazama mkoa wangu jinsi ulivyobarikiwa namwenyezi Mungu kwa kuwa na kila aina ya mvuto,maliasili,baraka,nafaka tofauti tofauti,mito inayotiririka maji usiku na mchana pamoja na mandhari nzuri ya milima ya uruguru inayoonekana hata ukiwa ndani ya gari wakati unaungia maeneo ya msamvu,napatwa na furaha sana moyoni mwangu na kujihisi nami mwenye bahati kuishi katika mji wenye kila aina ya neema kama Morogoro.

  Morogoro hii ninayoisifia hapa ndio ile ambayo ilipendekezwa na mweshimiwa Rais wetu kuwa Ghala la Taifa la chakula,sio kwa sababu tu wakazi wa mkoa huu wanalima sana ndo mana Rais akautunuku cheo hiko bali kwa sababu mkoa huu una kila aina ya rutuba katika ardhi yake.

  Naizungumzia Morogoro inayosifika pia kwa uzalishaji wa ndizi hapa nchini lakini ukiwa pia ni mkoa pekee unaotoa magimbi kwa wingi..sio hayo tu lakini ukweli ni kwamba hakuna tunda wala zao ambalo haliwezi kupandwa katika mkoa huu likashindwa kustawi, ni lazima litastawi, ndugu zangu karibuni sana Morogoro mje mjionee.

  Kwa kuwa taswira ya nchi na mkoa wowote ule hujengwa na maeneo ya mjini ni lazima leo hii nijikite kuizungumzia Morogoro mjini kwa mapana yake na Changamoto zinazotukabili sisi wenyeji wa eneo hili.

  Ndugu zangu wakazi wa morogoro mjini na wote mnaolitakia heri taifa letu kwa ujumla,pamoja na sifa kemkem nilizozimwaga hapo juu,eneo letu hili hususani JIMBO la morogoro mjini limekosa kitu muhimu sana katika uratibu wa shughuri zake za kila siku za maendeleo.

  Mwaka 2005 wakazi wote wa jimbo hili walishuhudia wanasiasa mbali mbali wakijinadi kupitia vyama tofauti tofaut kuomba ubunge,kama ilivyo ada ,sheria zetu za nchi zinamruhusu mtu mmoja tu kwa jimbo moja kuwawakilisha wenzake bila kujali idadi yao bungeni katika jumba la kutunga sheria na la-kupangia maendeleo.

  Masikini ndugu zangu wa MORO tulidhani tumempata mwakilishi MZURI kumbe mwakilishi wetu ,MZERU ni MZERU kweli kweli.

  Wakati anachaguliwa kuwa MBUNGE alikuwa ni miongoni mwa waganga wa hospitali kuu ya mkoa na kuwafanya wakazi wa MORO hususani wanawake wawe na matumaini makubwa kwake kuwa pengine sasa zile shida za kila siku za kwenda hospitali na kuambiwa hakuna dawa tafadhali nenda kanunue dirishani angalau zitakuwa zimefika kikomo kwani mwakilishi wetu wa safari hii analifahamu fika


  tatizo hili na sio tu angeweza kulitolea ufafanuzi kwa kulikemea pale hospitali,bali pia hata

  kulisemea bungeni na angalau wakazi wa MORO tukamsikia waziri anasema nini kuhusu hili, lakini wapi!!,amakweli ukistaajabu ya mussa utayaona ya firahuni.

  MZERU hivi umesahau kama sisi wakazi wa MORO tunapata shida katika kila kona ya huduma muhimu?.

  Hivi haufahamu kama pale hospitali kuu ya mkoa wagonjwa wanalazwa wane wane kitanda kimoja?.

  Hivi ni kweli haujui kuwa wakinamama waliokutegemea kama ungewasaidia kama ulivyowaahidi kuwa watapata huduma safi za afya wanakufa kila leo pale hospitali kuu kwa kukosa huduma bora za afya?.

  Inamaana haufahamu kuwa hospitali yetu ya mkoa ina tatizo la kukatika umeme mara kwa mara?,na kila umeme unapokatika mamia ya wagonjwa wanapoteza maisha yao pale hospitali kuu?.

  Kama unayafahamu hayo mbona ulitudanganya sasa na JENERETA ulilotuletea siku mbili tatu na kujitangaza kwenye vyombo vya habari,sasa hivi mbona hutuambii umelipeleka wapi JENERETA LAKO?,,mbona umetuacha na kiza kinene?. Kwa nini ulitufanya kama watoto wadogo kwa kutudanganya na pipi ili tutulie?.

  Hivi unafahamu kuwa kila umeme unapokatika pale hospitali kuu ya mkoa wauguzi wanaokuwa zamu za usiku wanaanguka kwa kujikwaa kutokana na kiza?.
  Hivi kweli unafahamu kama pale hospitalini hakuna KORIDO zinazounganisha MOCHWARI na majengo mengine hivyo kuwafanya wauguzi waanguke usiku pindi wanapopeleka maiti MOCHWARI?..kama unafahamu sasa tueleze basi umelipeleka wapi lile JENERETA ulilotudanganya nalo?.

  Mbunge wangu MZERU hivi unafahamu kuwa wakina mama wajawazito wanakufa wakati wa kujifungua au hata kabla na baada kwa ajili ya upungufu wa huduma muhimu za afya ambazo zipo chini ya uwezo wako?.

  Hivi mzeru hebu tuambie unahitaji SHILINGI ngapi ili uweze kuzungumza shida zetu BUNGENI?,,,tuambie tuchangishane tukupatie ili utuwakilishe bungeni ipasavyo…

  Hayo ni maswala machache sana kuhusu afya, wacha nikuambie mengine yanayotukera sisi mabosi wako tuliokupa ajira hiyo inayokufanya utugeuke na usahau shida zako..
  Hivi MZERU ni kweli umeshindwa hata kushauri lolote kama sio kutilia mkazo katika vikao vya halmashauri kuhusiana na stendi kuu ya MSAMVU?.


  Hivi unafahamu kama pale stendi hakuna hata maeneo rasmi ambayo watu wanaweza waka kaa au kusimama wakisubiria gari au wageni zao?..hivi unafahamu kama binaadamu hawa wanapigwa na jua kila siku pale stendi


  kutokana na kukosekana na sehemu ya kujikinga na jua ndio hao hao waliokupigia kura mwaka 2005 hadi ukashinda?.
  Ina maana haufahamu kama siku mvua ikinyesha tu watu wanakimbizana kiasi cha kuvunjana miguu wakitafuta pa kujificha,mpaka wanajazana katika vibanda vya watu vya biashara.

  Tuambie basi kazi iliyokupeleka bungeni ni nini?.umeenda kulala au kuchukua posho inayotokana na kodi ya jasho letu?.
  Kama unafahamu kuwa kila gari kubwa moja linalonusisha pua yake tu pale msamvu stendi linalipia SHILINGI 1000/= na kila gari dogo linalofanya hivyo linalipia SHILLINGI 300/=sasa tuelezeni basi hizi pesa zote mnazo tuchuna zinapotelea wapi kama hata choo tunachokwendea haja tunalipia?.

  Eti mweshimiwa mbunge wangu unafahamu pia kama wanafunzi wetu wa hapa MORO wanasoma katika mazingira magumu sana?..kwani unajua kuwa shule zetu hizi tulizochangishwa kuzijenga hazina hadhi ya kuitwa shule?,unafahamu kuwa hizi shule zetu hazina walimu, maabara, maktaba wala vifaa sanifu vya kufundishia?.
  Hivi unalijua jina ambalo hizi shule zetu hivi sasa zimebatizwa? .zinaitwa ‘SAKA MIMBA’..hivi ni kweli watoto wako wanasoma shule hizi?,nasikia siku hizi hata udiwani dili na wao wala hawasomeshi watoto zao katika hizi ‘SAKA MIMBA’

  Kaka yangu MZERU hivi unafahamu kama wafanyabiashara wadogo wadogo masokoni wanalipishwa ushuru kila leo lakini huduma zao za msingi haziboreshwi wala haziboreshwi?. Unaweza sasa ukawaambia ni kwa nini wanalipishwa ushuru wakati masoko mengine hayana hata huduma za choo?..kwa nini walipishwe ushuru wakati baadhi ya masoko mvua ikinyesha inakuwa ni kasheshe?..
  Lakini kwa nini hawa wafanyabiashara wadogo kazi yao wao iwe kulipa ushuru tu huku hamuwaambii ushuru huo unakwenda wapi?..
  Hivi unafahamu kuwa kuna maeneo huku kwetu maji ya bomba yakitoka wakinamama wanalala wakiyaota siku nzima?..sasa kitu gani kinakufanya uwe bubu bungeni?..
  Ndugu zangu mnakumbuka wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu MZERU alinadiwa kuwa ni ‘MWALI’ na alikuwa anatetewa asiongee kwenye mikutano ya hadhara badala yake wapambe wake ndo walikuwa wanakausha makoo yao kumbe


  maana yao ilikuwa ndo hii?..kumbe walikuwa wanatuuzia MBUZI kwenye KIROBA
  Ndugu zangu MZERU ni miongoni mwa wabunge wachache ambao majimbo yao yapo karibu sana na DODOMA yaani akianza safari ya kuelekea BUNGENI saa nne kasorobo saa sita na robo anakuwa ameshafika.. sasa inakuwaje hii fimbo

  iliyoko karibu kabisa na BUNGENI lakini Haiui Nyoka na kuziacha fimbo za mbali zinatamba BUNGENI
  Hivi unafahamu kuwa WABUNGE wakina ZITTO KABWE, DR SLAA, DR MWAKYEMBE,na ANNE KILANGO MALECELA wanatoka mikoa ya Mbali(mwisho kabisa) karibu na mipaka ya nchi jirani yaani kwa lugha ya mjini unaweza ukasema kuwa wanatokea ‘SHAMBA’ na wewe unatokea mjini sasa mbona MAJOGOO haya ya shamba yanawikia mjini na wewe JOGOO la mjini upo palele..
  Hivi umesahau kama Treni ikipita hapa kwetu MORO mpaka ifike KIGOMA kwa Mh.ZITTO inahitaji siku 2 na nusu..
  Inasikitisha sana..ndugu zangu taswira anayotuletea huyu MBUNGE wetu hatuna budi tuikemee, kama haiwezi kuifanya kazi tuliyomtuma ni vema ang’atuke na asigombee tena awaache majemedari wengine waende wakawatetee wakazi wa MORO..
  Hivi nikikuuliza kuwa tangu umeingia bungeni umewafanyia nini wakazi wako utajibu nini au utasema nakuonea?..

  Mweshimiwa Mbunge wetu hatuitaji utujengee Barabara,Hatuhitaji utununulie magari wala hatuhitaji utuletee zawadi kutoka DODOMA,,tunahitaji UACHE UVIVU BUNGENI,UACHE KULALA, usimame na ututee kama wenzako wanavyofanya HIYO NDO KAZI TULIYOKUTUMA.
  Sifa yetu kuu ya utani ni MOROGORO MJI, KASORO BAHARI..lakini kumbe pia MOROGORO MJI KASORO MBUNGE HODARI….kama wewe pia ni mkazi unayeitakia mema MOROGORO YETU CHUKUA HATUA SASA.

  Habibu Mchange

  0717178678
  Mchangehabibu@yahoo.com
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  POLE KWA KUTOA RUSHWA.... I hope Hosea will do you right!!
   
Loading...