Mjadala mpana: Kazi ya vyama vya upinzani ni ipi katika siasa za nchi?

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,357
6,422
Wadau nadhani kuna swali muhimu halijawahi jibiwa au (it has escaped the attention of the many) kulipa uzito wake.

Hivi kazi ya upinzani katika siasa za nchi ni pi? Nadhani tukikubaliana kazi za vyama vya upinzania ( na wote tukakubaliana na definition hiyo), chuki zinazoanza kujengeka katika jamii yetu na polisi zitaisha.

Maana tutaelewa na kukubaliana kwa kauli moja malengo mazuri ya kila mdau wa siasa.
 
Mkuu kazi ya upinzani kwa jibu rahisi ni kukosoa, kushauri, kuelekeza na kutoa njia mbadala za namna ya kufikia kilele cha maendeleo katika nchi au taasisi husika.
Tukikaa kama nchi tukakubaliana na definition hiyo, na IKAWEKWA KATIKA KATIBA, ugomvi au matendo ya polisi na upinzani tunayoyaona leo hayatakuwepo. Mimi kwa mtazamo wangu hatujaafikiana kama taifa majukumu/kazi/wajibu wa vyama vya upinzani KIKATIBA. Kazi za vyama vya upinzania tukishazianisha, zitambuliwe KIKATIBA
 
Mkuu kiuhalisia naamini viongozi wetu wanayajua haya unayosema tuyaainishe, ili yawe kama muongozo lakini nachokiona ni kufumba macho, kuziba masikio na kupotezea kile wanachokiona, kusikia na kushauriwa. Lakini tusikate tamaa.
 
ESCROW
IPTL
RADAR
MEREMETA
MELI MBOVU
UZWAJI WA NYUMBA ZA SERIKALI
RICHMOND
MIKATABA MIBOVU.
Vyote hivi vimeibuliwa na UPINZANI wakati ccm wakitetea na kufisadi nchi.
dowans
lugumi
operation tokomeza ujangili
mfuko wa commudity import support
kiwira
kagoda
twiga
deep green
buzwagi
mabehewa mabovu
meno ya tembo
mamilioni ya J.k
ununuzi wa nyumba ya ubalozi wa tanzania nchini italy
ununuzi wa majengo pacha ya B.O.T
loliondo gate
chavda na mashamba ya mkonge
pembe za ndovu kwenye ndege ya raisi wa china
uda
 
ni kioo cha gvt kama iko safi au chafu ama na kuinyoosha ktk mstali wa kiutendaji. kila mmoja anatambua umuhim wa kioo kwani kisipo kuwepo utaenenda kwa upofu
 
Mkuu kazi ya upinzani kwa jibu rahisi ni kukosoa, kushauri, kuelekeza na kutoa njia mbadala za namna ya kufikia kilele cha maendeleo katika nchi au taasisi husika.
Ila kwa hapa tz kazi yao ni kususa susa tu.
 
upload_2016-6-20_8-9-30.png

http://www.orpp.go.tz/sw/news_files/file_27.pdf
 
Mkuu kazi ya upinzani kwa jibu rahisi ni kukosoa, kushauri, kuelekeza na kutoa njia mbadala za namna ya kufikia kilele cha maendeleo katika nchi au taasisi husika.
Sasa mkuu hawa wa hapa Tz kazi kubwa ni kususa hawana nguvu ya kushawishi, wakikosoa hawatoi njia mbadala, kazi yao kubwa ni kupinga na kupinga kila kitu, na ndiyo maana hata serikali haiwathamini
 
Ila kwa hapa tz kazi yao ni kususa susa tu.
Sasa mkuu hawa wa hapa Tz kazi kubwa ni kususa hawana nguvu ya kushawishi, wakikosoa hawatoi njia mbadala, kazi yao kubwa ni kupinga na kupinga kila kitu, na ndiyo maana hata serikali haiwathamini
Red tea na Barafu ya moto, Mawazo yenu ni mazuri lakini hebu tuaangalie kwanini wanasusa, nimesema kazi yao in kukosoa na kuelekeza njia sahihi lakini sio serikali iseme tukosoeni hivi.
 
Vyama vyote in vya siasa. Na vina kaz ,Kutunga Sera za kuongoza nchi ,na kuzinad kwa wananchi ,kushika hatam ya nchi na kuongoza nchi kwa Sera zake

Sasa tunakuwa na vyama vya upinzani sababu kinachofanikiwa kuongoza nchi ni kimoja,

Neno upinzani linaweza kuwa baya ,lakin nadhan neno sahihi ni vyama ambavyo kura zake hazikutosha kushika hatamu,

So kama kura hazikutosha kushika hatamu,na nchi kujiendesha kwa Sera yao kwa asilimia 100 na wote tunajua kuwa kwenye Sera yao kulikuwa na mambo mengi mazuri ndo maana tunataka na wao wasiwe kimnya, watoe mawazo yao, pale yanapoungana na ya chama kinachoongoza nchi basi waunge mkono lakin pale ambapo mawazo yao yanapingana na ya chama kinachoongoza nchi basi wakosoe na kama mawazo yao yana mantiki basi serikali inayoongozwa na chama kinachoshika hatamu iyachukue na kuyafanyia kazi
 
Mkuu kiuhalisia naamini viongozi wetu wanayajua haya unayosema tuyaainishe, ili yawe kama muongozo lakini nachokiona ni kufumba macho, kuziba masikio na kupotezea kile wanachokiona, kusikia na kushauriwa. Lakini tusikate tamaa.
Tufanyeje ili wakione na wakikubali katika njia za amani. Tutafute third party awe kati yetu
 
Sasa mkuu hawa wa hapa Tz kazi kubwa ni kususa hawana nguvu ya kushawishi, wakikosoa hawatoi njia mbadala, kazi yao kubwa ni kupinga na kupinga kila kitu, na ndiyo maana hata serikali haiwathamini
Kama wanatoa hoja hawasikilizi unafanyaje
 
Mkuu kazi ya upinzani kwa jibu rahisi ni kukosoa, kushauri, kuelekeza na kutoa njia mbadala za namna ya kufikia kilele cha maendeleo katika nchi au taasisi husika.
Ni kweli kabisa kama serikali ingekuwa tayari pamoja na chama tawala kukubali kuwa upinzani siyo uadui.Na ukitaka kummaliza mpinzani wako fuata na yafanyie kazi anayokwambia.

Tuone wenzetu wamarekani wanavyofanya kwao.Taifa kwanza vyama baadaye.
 
Tufanyeje ili wakione na wakikubali katika njia za amani. Tutafute third party awe kati yetu
Yes, kutafuta third party ni muhimu, lakini pia ieleweke tu kuwa demokrasia ni gharama hata nchi zilizoendelea zilikumbana na vikwazo kama hivi, na ndo maana nikasema tusikate tamaa na tujue hakuna mtawala anayeachia madaraka kirahisi.
 
Ni kutokata tamaa, madaraka particularly kwa madikteita wa kiafrika ni matamu for personal gain. Ingelikuwa ni kuwatumikia wanachi wasingelingagania madarakani kama alivyosema Nyerere
 
Chama cha siasa ni kundi la watu lililoundwa kisheria kwa lengo la kuchukua uongozi wa nchi/dola. Kwa kuwa chama cha upinzani ni chama "kinachosubiri", lengo la kushika dola litafikiwa ikiwa chama kitafanikiwa kuonyesha udhaifu wa chama tawala wa wananchi na hivyo kupata ridhaa ya wananchi kupitia sanduku la kura.

Kwa hiyo "indirectly" kazi ya upinzani ni kuimarisha chama tawala kwa kuziondoa "usingizi". Yaani kutoa ujumbe kwamba "ukiteleza unaondoka na mimi nachukua".
 
Back
Top Bottom