Zitto Kabwe: Vyama vingi vya siasa vimekufa Tanzania

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
348
666
"Uchaguzi wa Marekani umeisha, Wachambuzi rudini kuchambua uchaguzi wa Vijiji na Mitaa. Kuna mambo mengi ya kutazama. Sura ya siasa imebadilika kabisa.

1. Huu ni uchaguzi wa namba, ukubwa wa oganaizesheni ya chama unapimwa kwa idadi ya wagombea na namna wamesambaa nchini. Idadi ya wagombea mpaka sasa imechora ramani mpya ya siasa za Tanzania bara.

2. Uchaguzi huu unaonyesha ukubwa wa idadi ya wanachama wa chama
Cha siasa. Takwimu mpaka sasa inaonesha kuwa Tanzania ni nchi ya vyama 3 tu. Vyama vingine vimefutika kabisa katika ramani ya siasa.

Nataraji kuona wachambuzi mnafanya kazi hii ili sisi wanasiasa tupate kuona na kuwajibika kwenye uhalisia na sio hisia na tambo tu.
Uchaguzi wa marekani umeisha, rudini nyumbani sasa."

Soma pia: Zitto ashauri upinzani kuungana kwenye chaguzi kuing’oa CCM

Chanzo Jambo TV
 
Kwanza vyama 3 ni vingi vinatakiwa viwe 2 tu chama tawala na chama cha upinzani undumila kuwi ndio uliofanya vyama viwe 3.
 
Mimi sio mwana chama wa ccm na siipendi ccm...
Lakini kwa Tanzania, kwasasa hakuna chama kinacho weza kuing'oa ccm madarakani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom