Mjadala - Kitabu cha unyama wa Paul Kagame: Behind the Presidential Curtain: Inside Out of real Paul Kagame

Mkuu umeni quote vibaya. Ninachosema ni kwamba tum block Kagame asije Magogoni kwani anaweza kumuambukiza JPM udikteta (au kwa lugha nyingine, wanaweza kuambukizana udikteta) ikawa hatari kwa raia wasiokuwa na hatia.
Maana yangu ni kuwa Kagame ni kijana mdogo sana kwa TZ hivyo hawezi leta ushawishi wowote wa hali hiyo coz nae ameshikiliwa maskio tuu
 
Asante mkuu,ni muhimu tujue haya yote sababu system ya awamu ya tano ilivyomkumbatia huyu mtu inasikitisha sana haswa ukichukulia awamu hii imejaa wachumia tumbo,hawaangalii mbele future ya watoto wetu,naogopa sana Tanzania ya mbele nina hakika mr slim anatujua hadi chupi yetu sasa hivi.TUKIMALIZA HUU MJADALA NITAWEKA LINK NYINGINE YA KITABU CHA DAVID HIMBARA ALIYEKUWA MSHAURI MKUU WA KAGAME KINAITWA KAGAME'S KILLING FIELDS
Mkui tafadhali Sana Weka Link ya Hiki Kitabu "THE KAGAME KILLING FIELDS."
 
Jana nilitoa link ya ku download hiki kitabu, kwa ambao hawaja download ingia JF Store, wandugu naomba msome vizuri hicho kitabu baadaye turudi kwenye mjadala hapa maana niliyoyasoma yanasikitisha.

View attachment 1072722View attachment 1072723

Kumbe ndiyo maaana Museveni kamchoka,wanajuana nje ndani, na Kagame hizo tabia zake ni za hatari siye yule tunayemuona sisi, SO SAD.

Kitabu kina pages 110(hard copy)ila kwenye pc hapa inaniambia ni pages 302 ,kwenye page ya 71 tunaona kitu fulani kuhusu tabia ya Kagame(familiar )

--
--It was President Kagame himself who briefed his senior intelligence commanders to use the tactic of being friendly to those they were planning to kill, at some point they gave out sugar and salt, cooking oil and soap to the locals that our soldiers had looted from shops just to make them come out of the hiding only to be killed in the end.----

Ni kwamba mwaka 1992 katika mazungumzo ya amani Arusha,Rais Juvenal Habryimana alisema wakimbizi wa Rwanda walioko nje kurudi ni ngumu sababu hakuna ardhi ya kutosha kwa hiyo akawasambaza wahutu mipakani huko na kuwapa ardhi ili ionekane kweli pamejaa na pia sababu nyingine ilikuwa ni kuwapeleleza RPF waliokuwa wanavamia kutokea Uganda

So,trick ya Kagame ikawa ni kwenda kwenye vile vijiji na wanajeshi wake kujifanya marafiki zao wakiwapa sukari,chumvi,nguo,siku moja katika kijiji cha Kagitumba wakaitisha mkutano mkubwa wahutu wakajaa wake,waume kwa watoto,katikati ya mkutano askari wa RPF wakarusha risasi na mabomu ya kutosha wakaua maelfu ya wahutu.

Niko page ya 72 ila dah hadi hapo nilipofika jamaa aliua marafiki zake waliomsaidia kupindua nchi karibu 10 tena wenye vyeo vya juu jeshini akiwemo FRED RWIGEMA swahiba mkuu wa Museveni kiasi cha kusababisha mdogo wake Museveni meja Salim Salehe kwenda kuua mameja wawili wasio na hatia waliosingiziwa na Kagame kwa Musevni kwamba walimuua Rwigema

Jamaa alikuwa anawaogopa makamanda wa ukweli waliomtoa dikteta Habrayimana , walikuwa hawamkubali sababu hakupigana vita muda mwingi alikuwa masomoni Marekani alipopelekwa na Museveni.

Mwandishi anasema jamaa ana tabia ya kujifanya rafiki yako huku akikutafutia muda sahihi wa kufanya yake(does that sound familiar?
nimesoma chote
 
Wawe waangalifu kweli kwani huyu bwana ni highly trained commando of the highest order na kwa vile anaelewa kinacho endelea, anakuwa mwangalifu sana na pia nadhani wale waliompa hifadhi ya ukimbizi nao watasaidia kumpa ulinzi.
UNAMPA SIFA ASIZOKUWA NAZO
 
Hii makala lazima niifuatilie yote. Jf ni sehemu sahihi pa kujifunza vitu
 
Waovu hua hawapendi mambo yao yajukikane. Usishangae akaanza kuwatafuta mnaomchambua humu. Au akaomba jf wafute huu uzi
 
Back
Top Bottom