Mjadala: Je, ni siku zipi ambazo mwanamke huweza kupata ujauzito katika mzunguko wake wa kila mwezi?

Wakuu ningependa kujua ni siku gani hatar kwa mwanamke kupata mimba kuanzia siku ya kwanza ya kubleed,.Mfano: kama ameingia hedhi mwez wa 5 tarehe 26, na mwezi wa 6 tarehe 25,Je siku yake/zake hatari za kushika mimba ni zipi/lini? Naomba Msaada wenu Wakuu?


Siku anayokasirika na kumpania mumewe.
 
Hapo huwezi kujua ni siku gani ukigusa kwa sababu hapo bado hujajua mzunguko wake ukoje, ili ujue siku gani safe ni lazima ujue her complete menstrual cycle. Mfano mwenye mzunguko wa siku 22, siku ya 8 ndio ovulation hivyo kuanzia siku ya 6-11 unatakiwa usiende peku peku unless labda unatafuta mtoto. While mwenye mzunguko wa siku 28 hiyo siku ya 8 ni safe day kwa sababu ovulation ni siku ya 14 hivyo siku zake za hatari zita range 11-17. Pia ukiangalia mwenye mzunguko wa siku 35 siku ya ovulation ni ya 21 hivyo balaa lita range 18-24, wakati kwa mwenye mzunguko wa 28 hizi ni safe days kwake. Ni kweli haya mambo yanachanganya lakini ili ujue siku safe za mwenza wako ni lazima ujue mzunguko wake vizuri ni wa siku ngapi. Kama cycle yake haiko constant ni changamoto sana
Asante sana Mr Google hapa ndo majibu tosha kama nikijitahid kujua mzunguko majibu ndo haya nakopy nakupest Tu!
 
Hili suala linachanganya wengi sana, wengi wana focus kwenye tarehe lakini hawajui mizunguko yao, Mzunguko wako ndio utakaokufanya ujue hasa siku za mimba ni zipi kinyume na hapo utakua unatwanga maji kwenye kinu,

Kujua mzunguko unafanyaje?
Mf: umengia hedhi tarehe 26.05 anza kuhesabu kuanzia siku ya kwanza uliyoona hedhi mpaka siku ya mwisho kabla ya hedhi nyingine kama hapo umeona tena tarehe 25.06 hivyo utahesabu kuanzi tarehe 26.05 mpaka tarehe 24.05 utapata siku 29, huu ndio mzunguko wako yaan wa siku 29.

Kujua siku za Mimba ni zipi?
chukua mzunguko wako toa siku 14.
Mf: 29-14=15
Upevushaji itakua siku ya 15 tangu uone hedhi hapo utaongeza siku mbili kabla na siku mbili baada ya upevushaji kwa maana utalenga kuanzia siku ya 13,14,15,16,17.

Muhimu: kujua mzunguko wako na kutoa kwa 14 utapata jibu la siku za hatari hata kama mzunguko utabadilika tayari unakua umejua jinsi ya kuhesabu mzunguko wako.
 
Kwa nyongeza ili usipate tabu nenda playstore tafuta apps za period tracker kama vile FLO, hapo utaingiza details zako basi utakua unaelekezwa kila mwezi siku za mimba ni zipi,

Easy tu.
 
Ni hivi... Chukua mzunguko wako toa 14 then znazo baki toa 4,hapo hutakiwi kushiriki tendo.

Then chukua zilizobaki baada ya kutoa 14 jumlisha 3 hapo unaruhusiwa kufanya mapenzi

Mfano

Mwenye siku 28 fanya hivi...

28-14=14
Hiyo ndo cku ya ovulation kwake,

So
14-4=10
Tarh hiyo hatakiwi kufanya mapenzi bila kinga kwani atapata ujauzito

Then,

14+3=17
kuanzia tarehe 18 ndo anaweza fanya mapenzi bila kupata ujauzito mpaka tena mwez unaofuatia.

Na mwenye tareh 30 pia vile vile...

NB.

Tarehe huwa zinaongezeka kila mwezi Yaan.
Kama ulianza na 28 ,

Mwezi unaofuata waweza kuwa na 30

Na

Mwez mwingne 35

Na hii hutofautiana kutoka mwanamke mmoja na mwingne.

Chunguza tarhe zako kwa makini, kisha tumia hiyo formula hapo juu itakusaidia.

Nawasilisha.
Naomba kuuliza kwa mfano nimeingia tarh 21 nikafanya tendo tareh 14 nikapumzika then nikafanya tena tarh 16 halafu nikanasa mimba hiyo mimba itakua ya tar 14 au ya 16 na mzunguko wangu niwa siku 28
 
Habar wadau mie Nina swali kwamafano nimeingia bleed tar 21 nikafanya sex siku ya 14 nikatulia nikarudia sex siku ya 16 halafu mimba ikatunga hiyo mimba itakua imeingia siku ya 14 au siku ya 16 mzunguko wangu niwa siku 28
Ulichepuka ,, tulieni Dada zangu umeona sasa unajitatiza mwenyewe hapo
 
Hiyo imeingia tar 14... ilaa sasa why uwe na wasiwasi kama ni mtu mmoja alikufokonyoaa??? Au ndo kubadilisha ladhaa oohoo angalia usijekuuza mechi mzee mama
Msaada mie niliingia tar 21 nikafanya tendo siku ya 14 nikatulia nikarudia siku ya 16 je kama mimba ikitunga itakua ya siku 14 au ya siku ya 16
 
Habar wadau mie Nina swali kwamafano nimeingia bleed tar 21 nikafanya sex siku ya 14 nikatulia nikarudia sex siku ya 16 halafu mimba ikatunga hiyo mimba itakua imeingia siku ya 14 au siku ya 16 mzunguko wangu niwa siku 28
Amisa umepata mimba jiandae kulea, maana nimeona umereply nyuzi zaidi ya nne zinazohusu mimba.
 
Back
Top Bottom