Mjadala: Gharama za road license vs uhalisia

Mangi flani hivi

JF-Expert Member
Jan 2, 2016
2,026
3,100
Salaam,
Nawapongeza sana kina mama kwa kusherekea siku Yao hapo jana.

Niweke bayana kuwa sina nia mbaya ya kuwatoa kwenye mjadala wa muhimu na wa kitaifa unaendelea sasa kuhusu MAKONDA vs BASHITE. Bali ni nataka kuonyesha maumivu ambayo nayavumilia kwa miaka mitatu ya umiliki wa kibaby walker changu hapa tz bara.

Nimefanikiwa kuishi Bara na visiwani katika vipindi tofauti vya kutafuta maisha. Nianze kwa kusema kuwa Gharama za kumiliki gari kwa Tanzania bara ni kubwa mnoooo... Ukikoswakoswa bandarini, utapigwa na insurance. wakikukosa utapigwa na traffic police. Hao wote cha mtoto ROAD-LICENSE ndo funga kazi.
Hivi jamani hii sheria Wakati wanapitisha tulikuwa wapi???? Mbona haya maumivu yatatuua??? Ngoja niwape mfano:
Mimi ninamiliki kibaby walker kidogo kwa umbo ila kina cc 1790.
Kwa mwaka natakiwa nikilipie 230000 bila kuchelewa hata sekunde. Ku delay kwa aina yeyote kutanigarimu penalt ya 75000. Sasa waungwana ikitokea insurance na roadlicense zinaisha pamoja, watoto watendaji Shule kweli???

Sasa unifanye mjanja uache kulipa kwa miaka kadhaa... Hapo ndo utajua kuwa ulikuwa unamiliki silaha ya maangamizi.
Kuna magari sasa hivi hayauziki.... Gari linadaiwa milioni 3 utauza sh.ngapi??
Mbona zenji garama za roadlicense zipo kwenye mafuta na maisha yanaendelea fresh tu.....

Nimeona nisije nikadakwa na maumivu, Kama wadau wa sheria wanaweza kubadili sheria hii tafwadhali tusaidieni.
Karibuni kwa nyongeza.....
 
Tatizo mkuu mapato yetu yanategemea sana mifuko ya wananchi, hasa wale wanaojikwamua kiuchumi. Kibaya zaidi kukaa kwetu kimya kunatafsiriwa kuwa tumekubalina na hali.
 
Mangi. Nilichokifanya mimi ni kutofautisha miezi ya kulipa insurance na motor license.

Iwe na utofauti wa miezi minne au mitatu. Unanua insurance third party, halafu baada ya huo muda una upgrade kwenda comprehensive. Kwa maana hiyo unaanza upya. (Ila omba Mungu usipate ajali ukiwa na third party)

Ukiwa na gari kwenye nchi zetu za kiafrika ni sawa na kuwa na ng'ombe, utakamuliwa tu.
 
Ndugu walishabadiri sheria siyo road license bali ni motor vehicle license (leseni ya kumiliki gari) iwe barabarani au imepaki nyumbani au mbovu lazima uilipie kama wamiliki bunduki wanavyolipia iwe wameitumia ama la.
 
tunakamuliwa vinawekwa kwenye kapu la Tanzania VINAGAWIWA MPAKA ZANZIBAR wasiotozwa...
 
Uzuri hata hao wanaokumbatia dhuruma hii inakuja kuwatafuna pia. Wanapostaafu ndiyo hugundua mkosa yao, wanapo anza kukabiliana hizi tozo wakiwa uraiani..Ni walalamikaji sana.
 
Back
Top Bottom