Mizengo Pinda anafaa kuwa rais wa nchi hii

Mizengo Pinda anafaa kuwa rais wa nchi hii

Joined
Jan 31, 2014
Posts
50
Reaction score
9
Ana sifa za kutosha sana ambazo sitazitaja kwanza mpaka wale wenye damu ya ubishi na chuki waanze kumponda ndipo nitakapo tumia sabuni safi iliyotengenezwa na matendo safi na uoni wenye kuonyesha dira ya kumkomboa mtanzania na umasikini.
 
Pinda hauziki Mkuu,naona alichofaulu ni uadilifu tu Ila mengine yote zero mpk sura jinsi gani tutatundika picha zake kwenye kuta maofisini kwetu......ni shidaa.....halafu nasikia juzi alikuwa mwanza anaunda kikosi kazi chake kwa njia zile zile za wengine......mwisho na uadilifu pia tutaanza kuuhoji.
 
kama tutaamua kwa pamoja kufikiri kwa uhuru kwa pamoja tutakubaliana mwaka 2015 tunahitaji Rais mwenye sifa kubwa ya uadilifu,ni dhahiri kabisa Mizengo Pinda anayo sifa ya uadilifu katika kipindi chake chote cha uongozi serikalini.
Ni lazima tutambue rasilimali kama gesi zilizogunduliwa nchini kwetu hazihitaji kusimamiwa na Rais mwenye sifa za ufisadi na tukifanya mchezo katika hili tutaishia kujuta.
Katika kipindi chake cha uongozi akiwa kama waziri mkuu ameonyesha kuwa kiongozi mzuri mwenye kutoa uhuru kwa mawaziri wake kutekeleza majukumu yao bila kuwaingilia katika majukumu yao na hii ikachochea kasi ya maendeleo nchini,hii ni sifa kubwa ya kiongozi kwa kuwa inaruhusu ubunifu kutoka kwa viongozi wa chini na huyo ndie Rais tumtakae.
kwa pamoja tutakubaliana Mizengo Pinda sio kiongozi wa kukurupuka katika utendaji wake na hivyo ndivyo Rais anavyostahili kuwa,tunahitaji rais anaejua kutafakari kila nalofanya ili kuliepusha taifa na maamuzi yasiyo sahihi.
hakika hiki sio kipindi cha kuchagua mgombea mzuri wa urais bali ni kipindi cha kutafakari rais mzuri,kwangu mimi siku ambayo Mizengo Pinda atatangaza kugombea urais nitamuunga mkono bila kusita.
 
Huyu mheshimiwa Mizengo Pinda ninaye mjua mimi ndio unampa hizi sifa zote, kweli tuna mawazo tofauti, naheshim mawazo yako mkuu lakini mi naona Pinda hata kuwa mkuu wa mkoa hawezi.
 
Tatizo kubwa ndugu yangu upo kiushabiki zaidi,mtu ambaye ni waziri mkuu unasemaje hana hata uwezo wa kuwa Mkuu wa mkoa? nakushauri kuwa na mawazo huru na sio kufwata upepo,lete hoja nzito ya kumpinga Pinda labda naweza kukuelewa.
 
Watu wengi wa na sifa za kuwa Rais akiwemo Pinda, wewe uliyeleta thread hata mimi. Lakini si Pinda wala wewe wala mimi atayekuwamkazi wa Magogoni. Atakayekuwa Rais hazungumzwi kabisa sasa lakini utashangaa atakavyoibuka mwishoni.
 
Ikulu sio mahali pa kupeleka mtu anayelia lia hadharani
 
Ikulu sio mahali pa kupeleka mtu anayelia lia hadharani

kama wewe uliguswa na mauaji ya albino Pinda ni nani hadi hasiguswe? na yeye pia ni binadamu kama walivyo binadamu wengine,aliwahurumia albino ndio maana machozi yalimtoka,na baada ya pale alichukua hatua dhidi ya mauaji yaliokuwa yakiendelea na kufanikiwa kuyadhibiti kwa kiwango kikubwa,hadi siku hizi za karibuni ndio yakaanza tena kutokea nayo yatakomeshwa chini ya uongozi wake.
 
Ukweli usiofichika kua pinda anaweza na wanaopinga wamekosa sera za maana au wanataka mzee wa richmond nini? Kweli waswahili walisema nyani haoni kundule. Mchafu anaona hata wasafi ni wachafu kama yeye hamna jema hata akija malaika gablieli hapa bongo bado mtamkosoa ni unafki tu hapa.. Tangaza nia mzee pinda uchukue nchii unakubalika sana tu.;
 
Ana sifa za kutosha sana ambazo sitazitaja kwanza mpaka wale wenye damu ya ubishi na chuki waanze kumponda ndipo nitakapo tumia sabuni safi iliyotengenezwa na matendo safi na uoni wenye kuonyesha dira ya kumkomboa mtanzania na umasikini.

Anafaa kuwa waziri wa kilimo, chakula na maendeleo ya ushirika ama waziri wa mifugo na uvuvi coz anapenda kilimo na ufugaji wa nyuki ila sio urahisi coz historia yake sio nzuri. Akiwa watu watapigwa sana ataruhusu askari kupiga watu na uvunjivu wa amani.
 
njaa hizi,pinda mda wake unaisha mwakani ili afanye mambo mengine
 
Back
Top Bottom