Mizania ya dhana ya kubeba Gundu au Kismati kutoka kwa Uliengonoka nae Punde.

dalalitz

JF-Expert Member
Sep 6, 2013
3,421
1,985
Waungwana,

Habari.

Inapeperuka dhana mitaani ya kuwa wapo Watu Wanawake kwa wanaume,
Ambao inaaminika ikitokea Punde tu umeshirikiana nae 'Kingono' basi kama una MIPANGO yoyote yakimaendeleo au kutafuta mafanikio fulani inakuwa Unafanikiwa, Ni-kama unapata 'Kismati' kutoka kwa uliejamiiana nae.

Wakati huo huo,
Wapo wengine ukishirikiana nao 'Ngono' Ukitoka hapo ndugu ni majanga juu ya majanga yaani hata Likidondoshwa fuko la Almasi ukifanikiwa kuliokota wewe,
Ile Almasi yote inageuka Kokoto yaani wewe unakuwa umebeba 'Gundu'.
Mambo hayaendi kabisa.


Binasfi, nimezisikia kauli za Jamaa zangu kadhaa wakilaani juu ya 'Gundu' wanalohisi kulibeba kutokana na kungonoka na watu fulani au wakati mwingine 'Kismati' walichokipata kutoka kwa 'Walioshirikiana nao Kingono'

Kinachofurahisha au kustaajabisha zaidi mara nyingi,
Wale wanaodhaniwa kuwa na Gundu mara nyingi ni wale ambao kwa Wanawake Mtu anaweza kusema ni Mrembo na nampenda,
Tatizo Lake ana gundu.
Na kwa wale wenzangu na mimi ambao pengine hawana mvuto kinyume chake wamekuwa na Kismati ajabu.

Sijatafiti,
Ila, kwa kuamini Uwingi wa wenye
U- weledi na Ufahamu ikiwemo uwanda mpana tulionao kwa wachangiaji hapa tunaweza kupata ufafanuzi, ushuhuda, ushahidi na pengine Upotoshaji pia.

Ila vyote kwa lengo la kupanuana uelewa katika Somo hili.

Tufahamishane kama ni ukweli,
Nini Mizania yake?
Na kama si kweli kwa Vigezo gani?

Naomba kuwasilisha.
 
Hizo ni imani kama zilivyo imani nyingine hazina ukweli wowote.
 
Ni kweli kabisa ilinitokea mimi,
Niliingia katika mahusiano na mdada flani,
Kiukweli hadi leo bado ananipensa ila huwa namkimbia,
KWANINI??
Kwa sababu nilipoanza kutembea nae nilianza kupata mabalaa mengi nambo yangu yakawa hayaendi ,
Nikaja kugundua baadae sana ,
Nlipo muacha mambo yakakaa kwenye mstari,
NI MWAKA UMEPITA BUT HACHOKKI KUNITAFUTA NA HUWA SOKEI SIMU ZAKE NA WALA HAKOMI KUPIGA.
 
Ni kweli kabisa ilinitokea mimi,
Niliingia katika mahusiano na mdada flani,
Kiukweli hadi leo bado ananipensa ila huwa namkimbia,
KWANINI??
Kwa sababu nilipoanza kutembea nae nilianza kupata mabalaa mengi nambo yangu yakawa hayaendi ,
Nikaja kugundua baadae sana ,
Nlipo muacha mambo yakakaa kwenye mstari,
NI MWAKA UMEPITA BUT HACHOKKI KUNITAFUTA NA HUWA SOKEI SIMU ZAKE NA WALA HAKOMI KUPIGA.
Kuwa muungwana.
Mfahamishe kuwa huna mpango nae,
Sio kuendelea kumtesa.
 
Nazungumzia kwa mwanamke wengine mtazungumzia kwa mwanaume...gundu la mwanamke linakuja pale anapozidisha kero yaan gubu,kushindana ndani ya nyumba,kiburi,ukimpa mpango wako wa biashara utasikia unanishirikisha ila ukifanikiwa unanisahau yaan mna wote ana kufeed negative charges tu ukikuta na yeye ndo malaya wa kurithi yaan baba ake au mama ake alikua malaya na ndugu zake wana maneno mengi km wazaramo#hutoboi ng'oooo and vice versa is very truee,manake atakupa mipango ya maisha utabadilika utakua smart utaanza kua na akili za kufanya mambo ya msingi zaidi..kampani za kutumia pesa utapunguza mwenyewe unajisikia ht kumtambulisha kwa watu
 
Back
Top Bottom