Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,634
- 46,276
1. Umoja wa Ulaya (EU)
Huu ndio mfano wa umoja wa nchi bora zaidi kuwahi kutokea duniani. Wana pesa yao yenye nguvu na heshima duniani. Wana vigezo thabiti vya kujiunga na umoja huo, hakuna vikwazo vya kusafiri na kufanya kazi/biashara. Kinachovutia zaidi ni nchi haiwi mwanachama tu kwa sababu iko Ulaya, Uturuki na nchi nyingine zimejaribu mara kadhaa kujiunga ila zimegonga mwamba.
2. NAFTA/USMCA
Umoja wa kiuchumi wa nchi tatu za Marekani, Canada na Mexico umerahisisha na kukuza biashara kati ya mataifa hayo kwa muda mrefu huku kila mmoja akifaidika nao.
3. OPEC
Umoja wa nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi duniani uko imara sana. Huenda sababu kubwa ajenda yao kubwa huwa ni moja tu, kuhakikisha bei ya mafuta inakuwa na faida kwao. Wakikutana ujue ni kicheko au kilio kwa watumiaji wa mafuta duniani na wakiamua jambo lao hakuna anayefanya udanganyifu au usaliti.
4. NATO
Huu ndio umoja imara zaidi katika kulinda maslahi ya ulinzi ya wanachama wake. Article 5 ya katiba ya Umoja huo imeweka comittement ya juu zaidi ya wanachama kwamba shambuli kwa mwanachama mmoja ni shambuliz kwa wote.
5. G7
Club ya nchi tajiri na zenye maendeleo makubwa zaidi ya viwanda(US, Canada, UK, Ufaransa, Japan, Ujerumani, Italia na EU kama mualikwa) ni ushirikiano wa mataifa saba tajiri kiviwanda na yenye mrengo mmoja hasa unaohusu "Western values". Wakiamua jambo linalohusu fedha huwa hawashindwi kitu au kurudi nyuma.
6. FIFA
Shirikisho la mpira duniani ni umoja imara sana. Wanachama wake wana nidhamu kwa kila kitu, iwe jambo lenye manufaa au vinginevyo. Viongozi na kamati zake zikishaamua jambo hakuna mwanachama anaweza kukengeuka.
Kimkakati kabisa waliweka kanuni ya mambo yanaohusu mpira kutopelekwa mahakamani ili wawe na utawala wao na mambo yote yaishie katika vyombo vyaka.