Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 31,139
- 88,800
Mfumo wa Injini
Outlander PHEV inatumia injini ya petrol ya cc 2,000 ikiwa na 4-cylinders, pamoja na mfumo wa umeme unaotoa jumla ya 197 hp.
Matairi ya mbele na nyuma yanatumia electric motors mbili zenye 60 kW kila moja.
Engine ya petrol yenyewe kuna muda inatumika kama generator au kuendesha gari moja kwa moja kwahiyo una option ya Parallel au Series hybrid.
Engine hupeleka power kwenye tyres za mbele tu coz hakuna driveshaft kwenda tyres za nyuma.
Betri na Uwezo wa Umeme
Outlander PHEV ina battery pack ya 12 kWh, iliyowekwa chini ya floor ya seat za, ipo flat kiasi kwamba pale seat za nyuma hamna ata ile uvimbe unaotokana na battery au drive shaft.
Range ya EV ni 60 km tokea full charge, ila utaishia kuendesha 120 km/h tu. Mwaka 2019 waliupgrade battery na kufikisha range kubwa zaidi na speed max hadi 135 km/h.
Fuel and Electric Efficiency
Kwenye EV Drive Mode, kiwango cha matumizi ni hadi 7.5 km/kWh. Yaani unit moja ya umeme (Tsh 350) unaenda zaidi ya 7.5 km.
Kwenye hybrid mode, efficiency ni approximately 18.9 km/L.
Muda wa Kuchaji
Outlander PHEV ina options tatu za kuchaji:
- Standard plug (3 pin) – kuchaji mpaka full kwa masaa 5
- Dedicated EV charger (nyumbani au public) – kuchaji full kwa ~ masaa 3.
- CHAdeMO DC fast charging – kufikia 80% ndani ya dakika 25.
Driving Modes
Outlander PHEV ina modes mbalimbali kwa dereva:
- EV Drive Mode – gari linaendeshwa na umeme pekee
- Series Hybrid Mode – injini ya petrol huzalisha umeme wa kuendesha motors
- Parallel Hybrid Mode – injini na motors zote zinatoa nguvu kwa gari.
- ECO Mode
- Battery Save Mode
- Battery Charge Mode
Wakati wa kupunguza speed (kushuka mteremko au braking), motors za mbele na nyuma zinafanya kazi kama generators, yaani kuconvert ile lost energy na kua umeme na kupeleka kwenye betri.
Tukio la Betri la 2013
Mwaka 2013, betri ya Outlander PHEV moja ilipata moto kwenye dealership huko Yokohama, baada ya kuchajiwa kwa muda mrefu.
Betri zilitengenezwa na GS Yuasa, sawa na wale wa Boeing 787.
Mitsubishi haikufanya recall, lakini ilisitisha uzalishaji hadi ilipogundua chanzo na kusolve. Baada ya kusolve mwaka huo huo matengenezo yakaendelea.
Bei CIF na kodi TRA?
CIF ya Outlander PHEV imechangamka kidogo. Na ushuru nao sio rafiki sana, kwa mfano tukisema leo tunanunua la mwaka 2014.
CIF $4800 na kuendelea kutegemea na hali.
TRA wanataka Mil 16.5 kwa huo mwaka., kwahiyo total ukiwa na 30 Mil unamiliki gari.
Mi naona ni gari zuri kwa mtu anaetaka SUV cheap kuiendesha especially kwenye mafuta na kua na feel ya EV.