🚨 Mitsubishi Outlander a.k.a Kenge kwenye msafara wa Mamba

Samatime Magari

Senior Member
Feb 10, 2017
103
388
1655870940155.png

.
Mitsubishi Outlander ni compact crossover [medium sized] SUV inayotengenezwa na kampuni ya kijapan ya Mitsubishi Motors, Mwanzoni ilikua inajulikana kama Mitsubishi Airtrek ilipokua introduced Japan mwaka 2001..
.
Mpaka sasa Outlander ina generation 4, Generation ya 1 ikianza [2001-2005], Generation ya 2 [2006-2012], Generation ya 3 2013-2021 na Generation ya 4 [2021- Present]. Umaarufu wa Outlander umekua kwa kasi miaka michache iliyopita na watu wengi wametokea kuipenda hii gari..
.
1655870988862.png
1655871004161.png
1655871025602.png
1655871044667.png

.
Wengi wamezipenda kutokana na muonekano wake na uwezo wa kubeba watu saba na kupita njia mbovu vizuri [ziko juu], Sasa Leo kipekee nitaenda kumgusa Generation ya Pili huyu ambae wabongo wengi wamenunua kwa sasa na wewe unayetarajia kununua...
.
Outlander generation ya pili[2006-2012] amekuja akiwa na engine option 6, Petrol Engine 2.0L 4B11 DOHC MIVEC I4 (kwa Japan na New Zealand), 2.4L 4B12 DOHC MIVEC I4, 3.0L 6B31 SOHC MIVEC V6 na Diesel Engine 2.0L VW TDI I4, 2.2L PSA DW12 HDI I4 na 2.3L 4N14 Di-D MIVEC I4...
.
hili neno MIVEC ni kama VVT-i isikuchanganye, Engine zimekuja zikiwa linked na Gear box [Transmission] za 5-speed manual na 6-speed manual INVECS-III CVT na 6-speed automatic na 6-speed twin-clutch SST AT..
.
1655871084468.png
1655871107538.png

.
Hizi gear Box za CVT tumia recommended oil zake tu usije weka Rubex humu utalia, na niwakumbushe tu ukiona engine imekua recommended kutumika Japan mara nyingi hizo ndo engine rafiki kwa mazingira ya huku kwetu Changanyikeni..
.
Kwa hii case ya Mitsubishi Outlander Engine 2.0L 4B11 DOHC MIVEC I4 na 2.4L 4B12 DOHC MIVEC I4 ndo ziko poa zaidi Kibongo bongo, Nikisema hivi simaanishi kwamba zingine sio nzuri hapana ziko poa ila inayotufaa zaidi watoto wa Chief Hangaya ni hizo tajwa hapo juu..
.
Mafuta gari inatumia vizuri tu ukilinganisha na ukubwa wake na engine iliyofungwa kwa Engine za Petrol inaenda wasitani wa km 10.9-12.4 Km/L, Wakati kwa Diesel Kuna turbo engine moja inaenda mpaka 14.9Km/L..
.
Hii waliichukua kwa Volkswagen ni Engine nzuri sema imekaa kizungu sana Maji machafu kidogo tu inapata kichocho, Na hii gari hasa engine ya 2.4L kama wewe ni muoga wa kununua mafuta nakushauri achana nayo..
.
1655871197573.png
1655871211143.png

.
Gari ndani iko very stylish [well laid interior] ikiwa na space ya kutosha, Dashboard yake imepangika vizuri [neatly arranged] ikikupa uwezo kama dereva wa kuitumia kiurahisi na inavutia, Ukija kwenye seat First row sehemu ya miguu ni kubwa kwa dereva na abiria wake Yani Hata mtu uwe na miguu mirefu au bonge unakaa vizuri tu..
.
Second row seat pia ziko poa wamezinyanyua kidogo ili zikufanye uwe confortable kwenye safari ndefu, Zile seat za nyuma ni ndogo hamna space achia watoto tu au kwa safari fupi kwa watu wazima zinaweza faa. Zile seat za nyuma ni ndogo hamna space achia watoto tu au kwa safari fupi kwa watu wazima zinaweza faa..
.
1655871312719.png
1655871396502.png
1655871433184.png

.
Zile seat za nyuma ni ndogo hamna space achia watoto tu au kwa safari fupi kwa watu wazima zinaweza faa..
.
Gari iko na cabin storages za kutosha zilizopangiliwa vizuri, Yani hapa vitu vyako kama Simu, Mkoba, Mawani nk vinahifadhiwa vizuri tu..
.
Ina cup holders 4 [Sio zile gari ukishika brake unakuta simu iko Miguuni au Kama bibie ana kifursana mkononi hajakifunga kinam-mwagikia]..
.
Pia ina glovebox na centre box ya kuhifadhia vitu vidogo dogo, iko na built in subwoofers kama unapenda music usio na fujo hapa ndo mahali pake pia na camera za kutosha nafikiri 6..
.
1655871509803.png
1655871535866.png

.
Ukija kwenye Boot kama 7 seats ziko active boot ni kama haipo tu, Inabaki space ndogo sana..
.
Ukilaza zile seat 2 za nyuma zikabaki seat 5 nafasi kwenye boot inapatikana ya kubeba mzigo wa kutosha wa kifamilia..
.
Iko na option pia ya Kulaza seat za katikati pia na hapa ndo space inakua kubwa zaidi sema tu hazilali chini kabisa kuwa level sawa na floor kama gari zingine..
.
Outlander nae ana grades kutokana na mwaka waliotengeneza na Grades zake zimetofautishwa kwa kiasi kikubwa na engine iliyofunga ila ukiangalia features nyingi ziko sawa..
.
Kuna grade M G na Did sasa hizi ukiangalia M ina 2.0L G ina 2.4L na Did ina 2.0L Turbo diesel Engine, Kwa Grade M na G zote zinapatikana zikiwa 4WD au 2WD na 5 or 7 seater na kwa 2.0 Did ndo inapatikana na 4WD na 7 Seater tu..
.
1655871658245.png
1655871678695.png

.
Gari barabarani in terms of Stability na handling iko vizuri sana, Ikishika barabara vizuri ni kama samaki anaogelea hivi, Ina kitu moja inaitwa multi-link strut coil springs inaifanya gari kuwa na control hata kwenye kona kali..
.
Inasemekana jamaa waliodesign hii gari ndo wanahusika pia na Mitsubishi Evo, Kama ni mtu wa rally nafikiri balaa la Evo unalijua unawaza pata picha flani kichwani. Ukija kwenye rough roads gari iko juu ina ground clearance ya 8.5 Inches bumps na mashimo unapita vizuri tu..
.
1655872157144.png
1655872170765.png

.
Upatikanaji wa spare parts zake sio rahisi kama Toyota ila zinapatikana, kama haujui machimbo ya spare unaweza pata tabu kidogo..
.
Service parts na suspension bei zake ziko juu kidogo ila ni himilivu ukija kq Body parts kama taa au side mirros ni gharama sana..
.
Nakushauri kama unategemea au unamiliki hii gari uikatie bima comprehensive ili ikitokea tatizo isikupasue sana..
.
1655872261153.png
1655872298346.png

.
Ukiongelea uadimu wa spare kuna wasee wanapenda kusema ohoo dunia imekua Kijiji hakuna haja ya Kuogopa, Nikukumbushe tu kuagiza spare Nje sio sawa na Kununua pale Ilala kwa Shayo.
.
Ni kama upate tatizo la kiafya badala ya kutibiwa pale Amana na bima yako ya NHIF uende India lazima uwe vizuri, nvm tuendelee.
.
Gari ndogo za Mitsubishi miaka ya nyuma hazikua na sifa nzuri Tanzania. Kuna time unaweza kutana na kigari kidogo cha Mitsubishi kimechoka engine inapiga kelele body iko kama imetapikwa hivi mpaka unaionea huruma..
.
1655872369984.png
1655872433165.png

.
Huyu Outlander ni kama amekuja kufuta hizo kumbu kumbu yale maumivi waliyopata wamiliki wa Mitsubishi siku za nyuma yametibiwa hapa..
.
Mitsubish Outlander kama ukimu maintain vizuri ni gari nzuri na very reliable akiwa mechanical issue ndogo ndogo sana za kawaida. Fanya service on time tumia vilainishi genuine haitakusumbua..
.
Outlander kwa sasa mpaka unaishika mkononi inaweza kukugharimu kati ya 18-22M, Kama unahitaji kuagiza au kununua Mitsubishi Outlander hapa nchini [showroom au ya mkononi] tunaweza kukusadia..
.
Tuko na network nzuri ya trusted dealers kwa hapa Tanzania na Japan, Dealers wanaotupa gari nzuri na salama kwa bei nzuri kwa ajili yako..
.
Simply tupigie simu, njoo WhatsApp au Ofisini Posta Mpya Phoenix House Mkabala na Mkapa tower na tutakupa kitu smart kama wewe ulivyo smart kwa bei nzuri..
.
Asante..
Samatime Car Dealers Co Ltd
0714547598
 
Hizi gari zipo nyingi Sana sikuhizi Kwa kifupi mitsubishi na Subaru huwa wanaigana Sana technology (kitu ambacho ni kawaida Kwa manufacturers)..
Mitsubishi Outlander zinafanana na Subaru forester 2008-2012 hata serikalini wanatumia Sana zile za diesel zenye six cylinder
 
Hizi gari zipo nyingi Sana sikuhizi Kwa kifupi mitsubishi na Subaru huwa wanaigana Sana technology (kitu ambacho ni kawaida Kwa manufacturers)..
Mitsubishi Outlander zinafanana na Subaru forester 2008-2012 hata serikalini wanatumia Sana zile za diesel zenye six cylinder
Hapo umemaanisha 4 cylinders!!?
Maana hakuna gari ya kawaida from Mitsubishi yenye diesel engine ya six..
Six zao wanafunga kwenye gari kubwa..!
 
Back
Top Bottom