Mitihani ya Suprementary

Mitihani ya Suprementary

Mzee mwenzangu juzi wa kwangu alikuwa anaongea na simu eti ana supu mbili kufuatilia anasema ni supplementary ila hajasema nimpe pesa... Hawa vijana bila kuuliza hivi watatufilisi...
 
ku sup si mwisho wa chuo ila ukicheza utalud chuo 2020
 
Acha uzuzu! Wewe ulilipia rufaa ya kutaka sap yako ipitiwe upya ili kama kulikuwa na makosa ya usahishaji itolewe. HUKULIPIA MTIHANI WA SAP ZAKO.
Acha kukariri kila chuo na utaratibu wake,,,,, wew ndio zuzu sasa
 
Heshima nyingi na za dhati kwa wanajukwaa wote!

Nina kijana wangu anasoma Mzumbe Chuo kikuu (Anasomea Sheria)
Naomba kujua hii mitihani ya Supplementary je inalipiwa pesa na kama inalipiwa ni kiasi gani?

Naomba kujua maana hawa vijana wa siku hizi mizinga mingi bila kujali hali ya mdororo wa uchumi kwa watanzania wengi.

Asanteni.
Niko mzumbe. Ni kweli tunalipia ,ni 20000 bila kujali idadi ya sup ulizonazo.
 
U

Usikate kiuno kushangilia kitu usichokijua!
Mzumbe hawalipishi mitihani ya sup, kinacholipiwa ni rufaa dhidi ya sap.
Unaongea nini wewe niko MU third year wanalipa supp vizuri sanaaaa....
Na hapa metoka kuwakopesha watu kama 5 hiviiiii.....
 
Hiyo inategemea chuo unachosoma kuna ambao chuo kinahitaji kulipia hiyo mitihani ya marudio na kuna baadhi ya vyuo hawahitaji malipo kwa ajili ya hiyo mitihani, lakini huyo kijana wako hadi anapata supp alikuwa mgonjwa au ndio ukilaza wenyewe mkulu aliyosema?
Unajikuta unaakili sanaaaaa!!!!!
Hupishani na anaemcheka kilema
 
Shida ya madenti wengi mnatumia pesa za kupewa vibaya,Fiesta Dar iliudhuriwa na madenti kibao japokuwa kiingilio kilikuwa kikubwa,wengine wanahonga/tongozea pesa za wazazi wao au boom,ndio maana wazazi wengi tumeamka hakuna "free lunch"
Wengine wananunulia "ngada"pesa za kupewa halikadhalika boom.
upo sahihi kabisa mkuu ila sidhani kama wanafunzi wote wapo hivyo, ni baadhi tu na maranyingi ni wale wasiojitambua vyema
 
Mitihani ya suplimentary hailipiwi,au hata maana ya suplimentary haujui
Inalipiwa mkuu labda kama unaongelea sup za diploma ya ualimu lakin university unalipa tena mfano KIU ni tsh 40,000/= per
 
Kwa case ya MU main campus wanalipia elfu ishirini kwenye kuapeal na pia wameanza kulipia sup mwaka 2015
 
Back
Top Bottom