Nawasalimia ndugu zangu,
Poleni kwa changamoto ya mvua
Nina shamba langu dogo hapo Chalinze, nataka nilipande miti pembeni kulizunguka.
Je, huu ni msimu mzuri wa kuotesha miti?
Je, ni miti gani mizuri yenye manufaa baadaye?
Je, kwa hapo Chalinze inapatikana au ni bora nitafute kwingine?
NB: Mimi siyo mkazi wa maeneo hayo ndiyo maana sijui chochote ila nina eneo hapo.
Nakaribisha ushauri na mawazo pia.
Asanteni.