Mitego 5 ya Kifedha Inayoua Vijana Kiuchumi

Mitego 5 ya Kifedha Inayoua Vijana Kiuchumi

Tuwapumzishe madogo. Kwani sisi wakati tupo kwenye age yao tulikua tumefanikisha kipi cha maana
 
Ukiwa kijana, kushika mshiko wa kwanza maishani ni kama kupata uchawi fulani hivi unaokufanya uhisi una uwezo wa kununua mtaa mzima. Lakini bila kujitambua, unajikuta unafanya makosa ya kijinga sana ya kifedha yanayokuhakikishia umaskini wa kudumu ukifika umri wa miaka 30. Usikubali kuwa "bosi wa sekunde tano" huku mfuko wako ukiwa unafuata ruti ya maji ya bomba yaani yanayoingia yanatoka hapo hapo.

Huu hapa ni mchanganuo wa mitego ya kifedha unayotakiwa kukaa nayo mbali mapema kabisa: 👇
Sifa: Huu ndio mtego mkuu wa kizazi hiki. Unakuta kijana ananunua simu ya milioni 2 huku analala kwenye godoro lililowekwa chini sakafuni bila kitanda, na asubuhi anaamka anakula kiporo cha wali wa jana. Unajaribu kuwatega wadada wa Instagram au washikaji wa vijiweni ambao kiuhalisia hawajali hata ukila mawe. Nunua kitu unachokiweza kiuchumi, sio unachokitaka ili "uonekane" una mshiko.

Kutegemea Chanzo Kimoja tu cha Pesa : Kutegemea mshahara pekee au mchongo mmoja wa mtaani ni hatari kuliko kutembea juu ya kamba ya manila huku umefumba macho. Siku mchongo ukizingua au bosi akiamka vibaya asubuhi na kukufukuza kazi, unarudi kuwa ombaomba ndani ya masaa mawili. Kuwa na "Side Hustle"—iwe ni biashara ndogo, kilimo, au ujuzi wowote unaoingiza hata buku mbili ya ziada kwa siku.

Mtindo wa Maisha Kupanda Kisa Kipato Kimeongezeka: Jana ulikuwa unapata laki mbili kwa mwezi, unakula kwa mama ntilie na maisha yanaenda safi kabisa. Leo umepata mchongo wa laki tano, ghafla umeanza kuona chakula cha mama ntilie kina wadudu, unahamia migahawa ya kishua na kuanza kununua maji ya chupa kila saa. Ukipata pesa zaidi, ongeza kiwango cha kuweka akiba (savings), sio kiwango cha matumizi ya anasa.

Kutegemea "Aviator" na Upatu kama Ajira: hakuna muujiza wa kupata utajiri wa haraka bila kufanya kazi ya maana. Vijana wengi sasa hivi wameweka akili zote kwenye kucheza kamari mtandaoni au kuweka pesa kwenye kampuni za kitapeli zinazoahidi mara dufu ya pesa ndani ya wiki moja. Mwisho wa siku unaishia kuuza hadi redio au feni ya ndani kisa umeliwa mtaji wote. Pesa halisi inajengwa kwa jasho, muda, na maarifa.

Kuishi Bila Mfuko wa Dharura: Unaishi kwa mtindo wa "pesa ikija, inatumika yote kwani kesho nina uhakika wa kuishi?" Siku simu yako ya kazi ikidondoka kwenye maji au ukipata dharura ya ghafla ya ugonjwa, ndio unaanza kutuma meseji za mizinga kwa kila mtu kwenye WhatsApp yako: "Mwanetu niazime buku tano nitakurudishia kesho jioni." Hakikisha una kiwango cha pesa kilichofichwa sehemu ambacho hakitandikiwi hadi dharura ya kweli itokee.

Pesa haina adabu wala adui; ukiichezea ukiwa kijana, itakuja kukutesa vibaya sana ukiwa mzee. Badili mwelekeo sasa hivi, anza kuheshimu kila shilingi inayoingia mkononi mwako ili ujenge kesho yenye heshima.
Mfuko wa dharula ndo pagumu
 
Umetisha sana
Nataka niweke Uzi kuhusu kamari vijana hawaelewi yaani mtu anashindana na programmable machine alafu anasema anapata pesa kila siku Lakini hasemi anazopoteza kila siku na mwenye kamari hapati hasara.
 

Attachments

  • 20260621_125448.jpg
    20260621_125448.jpg
    625.9 KB · Views: 10
Punguza ushauri mzee!!!
Shida zako usituletee sisi 😂😂😂
 
Mmewekewa na bango kabisa huko

Ova
loose Nut
Wapo sahihi huu mchezo watu wanapiga sana hela ukijua timing tu na kuucheza kama haujui utaishia kuliwa hela kila round kikubwa ni kucheza kwa kuhesabu round tu na zile patten za namba basi
 
Back
Top Bottom