November 15 2015 tuliandika hayo hapo juu. Tulisema, suala la ZNZ linagusa nchi nzima na tutajikuta tunawatia wananchi shida zisizo na sababu kisa tu kulinda CCM Zanzibar ambayo ni kundi la watu wachache wasiotaka kuona demokrasia, waliojipa haki ya kutawala na wanaodhani ni raia wa daraja la kwanzaTATIZO LA ZANZ NI KUBWA
Tatizo linaloendelea ZNZ ni kubwa kuliko inavyodhaniwa. Ukubwa si tu kwa hali ilivyo, bali muungano kwa ujumla wake.
Viongozi wanalifumbia macho, mbele ya safari litajidhiri kwa namna nyingine kubwa zaidi
Mwaka 2010 ZNZ ilifanya mabadiliko katiba yake ya 1984 kwa kuleta mgongano na katiba ya JMT
Wengi waliliona tatizo hailo, viongozi wakalichukulia kwa wepesi na kwa mazoea tu ya 'ndivyo tunavyofanya'
Majuzi Rais Mstaafu alizungumzia hali ya ZNZ kwa kusema inamgusa
Akiwa Rais wa JMT hali haipaswi kumgusa bali yeye kuwa sehemu ya shauri.
Ni Amir jeshi mkuu na hivyo kutuma wakuu wa vyombo vya usalama kuzungumza na wanasiasa linatia shaka ushiriki wake
Ameondoka na kumwachia Rais aliyepo tatizo. Madhara ya tatizo ni kuigusa JMT kama nchi na si Zanzibar tu
Mwaka 2001 yalipotokea matatizo tunayojua, taifa kwa ujumla lilibeba sura ya tatizo na wala haikuwa ZNZ pekee
Uchaguzi 2015 Rais wa JMT ametangazwa kukiwa na matatizo ZNZ, unazidi kuleta ufa katika muungano. Wanaliona?
Pamoja na hayo, uchaguzi unatufumbulia kitendawili cha rasimu ya Warioba
CCM walikataa rasimu kwa hoja rasimu kuelekea kuvunja muungano badala ya kuuimarisha
Kwa mazingira yaliyopo, mgogoro wa ZNZ unazidi kudhoofisha muungano badala ya kuimarisha.
Nguvu ya Rais wa JMT haionekani na ushiriki wa upande mmoja wa muungano unazua maswali kuliko majibu
Vumbi litakapotulia visiwani, kuna uwezekano ZNZ kuendelea na 'utamaduni' wa mwaka 2010 wa kukiuka katiba ya JMT, kwani kwao katiba ya JMT inapoteza nguvu kila uchao. Yale ya 2010 ya ZNZ kwenda ''solo'' yatajirudia bila kizuizi
Lakini pia, wabunge wa CCM wataelewa kwanini masuala utaifa ni mbele badala ya vyama.
Kile kilichokataliwa na wabunge wa CCM sasa kinaonekana.
Hali iliyopo ni uwepo usio rasimi wa Tanganyika na Zanzibar.
Tunasema hivyo kwasababu, haionekani kama ZNZ imeshirikishwa na tume ya uchaguzi ya JMT
Kama imeshiriki, NEC inapaswa kueleza umma ushiriki wa ZNZ ni upi katika hali ya sintofahamu inayoendelea?
Kuna mambo matatu yanayoweza kujitokeza
Moja, kama uchaguzi utamalizika na CUF kuongoza nchi kama inavyodaiwa, huenda SMZ kupitia BLW kufanyia marekebisho sheria kuepuka matatizo kama yaliyopO.Sura iliyopo inatoa nafasi ZNZ kuamua hatma yao na si JMT
Pili, uchaguzi utakapofutwa kwasababu za ukiukwaji wa taratibu kama inavyosemwa, kura za WZNZ hazitakuwa zimechagua Rais wa JMT. Hivyo , Wznz watakuwa na sababu za kuamini Rais wa JMT ni wa Tanganyika
Haya ni matatizo ambayo CCM inajaribu kuyaficha, mbele ya safari yatajidhihiri pengine kwa mgogoro mkubwa wa kikatiba
FUNZO
Yapo yanayojitokeza na kuleta funzo kubwa kwa Watanzania. Kwamba, kuishi kwa hisia na mazoe ni jambo la hatari
CCM imekumbatia katiba ya 1977 licha ya kuelezwa mapungufu yanayotokana na nyakati.
Kwa kuamini tu kuwa itatawala siku zote, hilo haliwashughulishi hata kidogo.
Tumeona uwezekano wa mhimili mmoja kumilikiwa na pande mbili sasa ni mkubwa kuliko ilivyokuwa huko nyuma.
Hatujui hali ingekuwaje kama ingetokea hivyo
Tayari mgogoro wa ZNZ unaonyesha baraza la mawaziri la Serikali ya CCM kuwa na wapinzani.
Ikumbukwe, Rais wa ZNZ ni mjumbe wa baraza la mwaziri la JMT. Je tuna serikali ya umoja wa kitaifa kikatiba?
Lakini funzo kubwa ni lile linalosemwa ''success favors the prepared mind'
kwamba mafanikio ni zao la matayarisho ya kifikra.
Tuliyoyaona mwaka 2010 kutoka Baraza la wawakilishi, mwaka 2015 bunge la katiba na 2015 uchaguzi mkuu lazima tukiri hatujafanya maandilizi ya kifikra, na mafanikio yetu siku za usoni yatategemea majaaliwa na si mipango
Kama Taifa hatuwezi kuishi kwa njia za ramli au kamari. Lazima tuwe na prepared mind.
Tusemezane
Bandiko linalofuata tutapitia hoja tulizozikazia ili kuonyesha namna ambavyo CUF walikosea na namna ambavyo makosa yao yanatumika kubadilisha hoja nzima. Tutaangalia kauli za waziri na jinsi zinavyopingana na za viongozi wengine hata kufikia kukana baadhi ya wahsiriki wa mazungumzoWaziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk.Augustine Mahiga.Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga, amewataka washirika wa maendeleo wakishawishi Chama Cha Wananchi (CUF) kishiriki uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar ili kuwatendea haki wanachama wake.
Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalumu mjini Dodoma, Balozi Mahiga alisema wahisani wanapaswa kuchukua jukumu hilo ili CUF iache kususia uchaguzi uliopangwa kurudiwa Machi 20, mwaka huu na kuendelea kumsimamisha mgombea wao wa urais, Maalim Seif Sharif Hamad, kwa vile wao (wahisani) ndio wanaoonekana kusikilizwa zaidi na chama hicho kuliko serikali.
Alisema CUF ambayo miongoni mwa viongozi wake, Katibu Mkuu Maalim Seif, imekuwa karibu zaidi na wahisani ndiyo maana wameonyesha ghadhabu dhidi ya Serikali ya Tanzania kwa kukatisha misaada, ikiwamo inayotoka Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC).
Zanzibar iko katika mkwamo wa kisiasa baada ya Tume ya Uchaguzi visiwani humo (ZEC) kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015 kutokana na kile kilichoelezwa na mwenyekiti wake, Jecha Salim Jecha, kwamba ulijawa na kasoro nyingi zilizoupotezea sifa ya kuwa ‘huru na wa haki’.
Maalim Seif na wanachama wenzake wametangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio na badala yake kusisitiza ZEC iendelee na majumuisho ya kura ili mshindi ajulikane.
Hata hivyo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichomsimamisha Dk. Ali Mohamed Shein kutetea nafasi yake ya urais, kinaungana na ZEC kuwa uchaguzi ni lazima urudiwe.
Akieleza zaidi kuhusu suala hilo la Zanzibar, Balozi Mahiga alisema pamoja na mvutano uliopo sasa visiwani humo, anaamini bado kuna nafasi ya kutosha kwa pande zote kuzungumza ili kufikia maridhiano, ingawa mojawapo ya changamoto zilizopo ni pamoja na hali ya kutoaminiana.
“Naona kwa sababu sisi wenyewe ile inaitwa confidence (kuaminiana) haipo sana. Kati ya sasa na Machi tuendelee na kipindi cha kujenga kuaminiana kwani bado kuna nafasi ya mazungumzo,” alisema Mahiga.Aliongeza kuwa katika kipindi hiki (sasa hadi Machi), kuwe na ushawishi kwa pande zote kuhusiana na uchaguzi huo.
“Kupeana ushawishi wa namna fulani… unataka kuwe na maandalizi ya namna gani, ushiriki wa namna gani, tuna karibu siku 50.
Lakini pia marafiki zao (CUF) wawashawishi,” alisema Balozi Mahiga.
Alipoulizwa ni kwa nini anaona CUF iko karibu zaidi na wahisani hadi kusema ni marafiki zao, alisema; “Ni kwa sababu ya ile ghadhabu wanayoifanyia serikali ya Tanzania. Ni kama vile kwa nini huyu mmemfanyia hivi.”
Kadhalika, Balozi Mahiga alisema leo atakutana na mabalozi wa nchi zote waliopo nchini na kwamba miongoni mwa mambo yatakayopata nafasi ya kuzungumziwa ni pamoja na suala la Zanzibar.
“Kwa nini hivi, mimi tarehe 8 (leo), nakutana na mabalozi wote, kwa niaba ya Rais. Nitazungumza hata na hili, ninavyosema rafiki zao ni kwamba wao si tu wanawasikiliza, wanawafuata… jamani eeh, hivi na hivi, na wale wanawasikiliza. Watu wa upinzani wanawafuata wale (wahisani), inawezekana wana imani zaidi na wale wanaowafuata, na wale wanawasikiliza,” alisema.
Aliongeza kuwa: “Jamani ni hivi na hivi na hivi… sasa sisi wenyewe, imani kati ya sisi kwa sisi imepungua. Lakini wakikimbilia kule wanasikilizwa, ndiyo tunasema mnavyozungumza na hao marafiki, au kama siyo marafiki, basi hao watu wanaokuja, mjaribu kuwashawishi.
“Hebu fikiria, chama ambacho kina wafuasi wengi wasishiriki katika uchaguzi… tutakuwa na miaka mitano ya aina gani? Tutarudi kule nyuma tulipotoka. Siyo sahihi, hatuwatendei haki watu wa Zanzibar, hatuwatendei haki Watanzania wengine ambao wote tunabeba mzigo sasa hivi kwa sababu ya maamuzi tu ya chama kimoja.”
Bila kufafanua, alisema watu wanaadhibiwa kwa kitu ambacho kina majibu, huku akisema kwenye siasa lazima watu wakubali kuwa na machaguo mbalimbali na siyo kung’ang’ania msimamo mmoja.
Alisema amekuwa akiulizwa sana suala la hali ya Zanzibar kila anapokwenda nje, lakini yeye amekuwa akiwaeleza uhalisia wa mambo ulivyokuwa mpaka uchaguzi ukafutwa.Dk. Mahiga alisema jibu ambalo huwapa ni kwamba pamoja na kuwa Tanzania ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Zanzibar ina madaraka tosha ya mambo yake ya ndani, serikali yake, Katiba, Bunge (Baraza la Wawakilishi) na Tume ya Uchaguzi.
Pia alisema huwaeleza kwamba uchaguzi wa Zanzibar ni tofauti na ule wa Tanzania na namna hata walivyomchagua Rais wa Muungano, John Magufuli.
“Serikali ya Zanzibar ina uamuzi wake, utaratibu wake, na utamaduni wake wa kisiasa ambao ni tofauti. Kwa hiyo mtu akisema ni Tanzania lakini Zanzibar haikuwa hivi, Tanzania si mkoa, Tanzania ni serikali… kwa hiyo hilo lazima lijulikane hivyo,” alisema.
Aliongeza kuwa katika mantiki hiyo ya Zanzibar kuwa na aina yake ya serikali na mwelekeo wake, pia wana utamaduni wa kutatua matatizo yao wenyewe.“Tuliona huko nyuma wakati ule kuna matatizo kati ya vyama na serikali, na vyama vya upinzani, hatimaye wakakaa na tukapata muafaka wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Hii ilikuwa wao tu pamoja na kuwa watu walisaidia na kuwaambia jamani zungumzeni,” alisema.
Balozi Mahiga alisema Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) iliona kuna tatizo Pemba, ambapo idadi ya wapigakura ilikuwa kubwa kuliko walioandikishwa na pia kulikuwa na matatizo katika kuhesabu kura, hivyo wakaona hata wakitangaza matokeo bado kutakuwa na tatizo.
“Kwa hiyo wakasitisha kuhesabu kura. Zingine zilikamilika pamoja na kuwa zilikuwa na utata, zingine wala hazikuhesabiwa na likatokea tamko kwamba uchaguzi umesitishwa.“
Baadhi ya watu, mashirika, European Union, Marekani, Commonwealth na wote waliona kwamba tume haikutenda haki… kwamba ingemaliza kuhesabu na matangazo yatoke. Lakini tume iliona kabisa kwamba ikifanya hivyo itakuwa imekiuka maadili yake,“ alisema.
“Kwa hiyo kukawa na mvutano. Kwamba kwa upande wa vyama, walivyopewa maamuzi haya ya tume, wakakaa kuona wafanye nini. Na tukadhani katika hivi vyama kuzungumza kule, na sisi bara watatukaribisha, au Serikali ya Muungano watatukaribisha. Lakini wakasema hata, hili mtuachie sisi wenyewe tutalizungumza kuhusu huu uamuzi wa tume,” aliongeza Balozi Mahiga.
Alisema mazungumzo baina ya CUF na CCM yalianza na kufanya takriban vikao sita huku kukiwa hakuna kitu kinachosemwa juu ya kinachoojadiliwa.
“Tukasema jamani eeeh, mbona hatusikii tamko lolote? Na hapo ndipo Rais Dk. John Magufuli akachukua uamuzi wa kuzungumza na pande zote mbili. Akazungumza na Masalim Seif (mgombea urais wa CUF), na Dk. Shein kwamba jamani vipi?
“Na wao walisema wanazungumza wenyewe na wamejumuisha marais wa zamani wa Zanzibar, si marais wa zamani wa Tanzania. Na kila mtu akawa anauliza hivyo, jamani vipi? Sasa wakati wanazungumza hivyo, baadhi ya wadau wetu wa maendeleo na marafiki zetu wakawa wanasema, Jamhuri ya Muungano hawafanyi vya kutosha kusukuma na kutatua suala hili,” alisema.
“Wengine wakasema hata misaada tunasimamisha, kama vile Marekani (MCC) tunasimamisha kwa sababu sisi tunaona haya mazungumzo hayatoi majibu na afadhali tu yatangazwe (matokeo ya uchaguzi) kama yalivyokuwa, lakini katika hilo baadaye tume ikasema jamani, afadhali tuite uchaguzi mwingine.
“Sasa mimi ninaloeleza katika hili kwa marafiki zetu ni kwamba kama upinzani wanadai waliungwa mkono na kushinda, sasa hivi hawana cha kuogopa… wana uchaguzi mwingine. Wale waliowachagua na wanaodai kwamba waliwapa ushindi kwa nini wasiwachague kama walivyowachagua huko (awali),” alisema Balozi Mahiga.
Alisema jambo kubwa hivi sasa ni kuhakikisha uchaguzi huu utapangwa kwa namna ambayo ni ya wazi na utakuwa wa haki na unasimamiwa ipasavyo na watu mbalimbali, ikiwezekana hata wa nje wakaribishwe tena ili watazame.
Alisema anaona kufanya uchaguzi mwingine ni suluhisho kuliko kusema, ‘sisi tumeshinda tutangazwe’, jambo ambalo katikati ya utata uliopo linaweza kuleta fujo.
Alisema kwa sababu inaonekana wahisani na nchi zingine wanazungumza zaidi na CUF na wanawabebea mabango, wawaambie kama kweli wana uhakika kwamba walishinda uchaguzi, hawana cha kuogopa bali waende tena kwenye uchaguzi.
Balozi Mahiga alisema jambo la msingi ni kuhakikisha mazingira ya uchaguzi yanakuwa huru na haki.Chanzo: Nipashe
Waziri wa SMZ alisema 'ZNZ wapo tayari kufa njaa'' kauli hiyo tulisema si njema. Leo tunaona tatizo linavyozidi kuwa kubwaMAONI
KAULI YA WAZIRI WA SMZ NI HATARI
INACHOCHEA HASIRA KWA WZNZ NA WATANGANYIKA
Waziri SMZ amekaririwa 'Znz ipo tayari kufa njaa kuliko kuwanyenyekea wazungu'
Kauli imekuja baada ya ''marudio ya kura' yaliyoacha makovu katika jamii ya WZNZ
Kwa miezi mitano hali ya kisiasa na kiuchumi ZNZ imeathiri maisha ya wananchi
Waathirika ni wa kipato cha chini ambao shughuli za kipato ziliathiriwa na siasa.
Biashara na shughuli za utalii zikakwama na kufanya maisha kuwa magumu
Waathirika ni wale wasio na account Uswiss, Ujerumani au kwingineko.
Ni wasioweza kununua aspirin kwani kwao ni bidhaa inayohitaji kutafuta kpato
Ni wale wasioweza kujiuguza India au Uingereza, kwao mardhi ni 'Tangazo la kifo'
Ungewauliza wanataka nini, kwao Amani ndicho kitu cha kwanza.
Wanajua kupitia Amani, heshima ,utu na ubinadamu wao unatimia kwa kiwango kikubwa.
Hawana habari nani anakaa hekalu gani, anakula biryani au anasaza makaimati. Wanachojua ni jua litoke na kuzama wakiwa salama
Uchumi wa ZNZ unategemea huduma za jamii kama Utalii na biashara.
Kuathirika kwa biashara na kuzorota huduma za jamii ni pigo kwa wananchi
Kauli ya kuwabeza wazungu inatia shaka. Lau kana mataifa hayo yasingekuwa na nguvu, waziri hakUwa na sababu za kuyaongelea.
Na wala mataifa ya Magharibi hayana sababu za kukaa kikao cha kujadili ZNZ.
Wanaweza kutafuta Kamba fupi na rahisi kufikia wanachokitaka.
Kwa mfano, wakitoa tahadhari ya usalama wa visiwani, biashara ya Utalii ambayo ni uti wa uchumi wa ZNZ itaathirika kikamilifu. Kauli kuhusu ZNZ inatosha kuumiza ZNZ
Kuanguka kwa utalii kuna athari katika kipato cha mwananchi na athari katika biashara
SMZ itakujikuta katika wakati mgumu katika kutoa huduma, kujiendesha na kutimiza malengo ya maendeleo. Kukiwa na mgawanyiko uliopo, hali itazidi kuwa mbaya
Mwisho wa siku atakayebeba mzigo ni mwananchi wa kawaida.
Mwananchi asiyeweza kukubaliana na waziri kuhusu ZNZ kufa njaa.
Hakukuwa na sababu ya ZNZ kufa njaa, kwanini wawekewe maneno ya kufa njaa?
Ni kikao gani cha wznz kimeazimia hayo?
Na mznz gani wa kufa njaa, mwenye account Uswiss au mfuma madema?
Athari za kipato kwa SMZ zitaathiri Tanganyika. Kwamba, huenda tukalazimika kuendesha serikali tatu kwa gharama za wananchi wa serikali moja.
Tunasema tatu kwa mantiki ya serikali ya ''Tanganyika'' kama ilivyo kwa miezi 5, serikali ya muungano baada ya mazingaombwe na SMZ
Mwananchi wa Iramba, Mtimbira, Isevya, Nakapanya, Najilinji,Magila, Kicheba na Katoma watalazimika kulipia gharama za SMZ ambayo viongozi wake wameamua ife njaa
Hili litachochea hasira pande mbili.
Upande wa Zanzibar kwenye moshi unaofuka na Tanganyika unaoona hauhusiki
Waznz walidharua Tanganyika katika marekebisho ya katiba ya 1984 marekebisho 2010
Ipo siku Watanganyika watakuwa na haki ya kuuliza, kwanini wabebe mzigo usiowahusu
Watahoji kama si ujinga kugharamia Zanzibar iliyoamua kufa njaa yenyewe
Watahoji kwanini walipe kodi kwa watu walio tayari kufa njaa
Tayari mgogoro umeppoteza pesa za millennium, waendelee kufa njaa kama wale walioamua kufa njaa kwa mapenzi yao? Kosa la Mtanganyika ni lipi hadi alipe gharama?
Hapo tutakuwa na tatizo jingine jipya
Tusemezane
Wahafidhina wachache wametuweka 'rehani'MGOGORO WA ZNZ WALIATHIRI TAIFA
TULIONYA MAPEMA, HILI NI SUALA LA TAIFA SI ZNZ
MIRADI ILITAFUTWA KWA GHARAMA KUBWA, KUKWAMA NI HASARA KWETU
Kama mtakumbuka, mapema sana katika jamvi la duru tulionya kuhusu mgogoro wa ZNZ na athari zake kitaifa
Tulisema, kwa muundo wa muungano, Rais wa JMT ndiye mwenye dhamana ya ulinzi na usalama na ni taswira ya nchi
Bodi ya MCC imesitisha msaada kwa Tanzania. Ikumbukwe, awamu ya 4 ilitumia muda mwingi kutafuta msaada huo
Aidha,serikali ya CCM imesifia safari za nje kwa kuonyesha MCC kama sehemu ya mafanikio ya ziara hizo
Inapotokea Taifa likakosa misaada likiwa limekeza muda na rasilimali, ni upotevu wa nguvu na rasilimali bila sababu
Awamu ya 5 nayo ilisema mgogoro utapatiwa ufumbuzi, kitu kinachoonekana hakikuwa na uhalisia
Mgogoro wa ZNZ ni wa sehemu ndogo sana ya Taifa. Madhara yake yanawagusa watu wasiohusika, inasikitisha
Hatuoni sababu za Watanganyika kubeba mzigo wa matatizo yanayosababishwa na mgogoro wa ZNZ
Hili ni sawa na kutoa 'kafara' ya watu takribani milioni 44 kwasababu tu ya wapiga kura laki 3
Lakini pia mgogoro huu hautokani na wapiga kura wa ZNZ.
Kazi yao ilikamilika, na wengi wakiwemo wa CCM walikubali matokeo.
Tatizo linatokana na wahafidhina wasiozidi 20 wa CCM waliogomea matokeo hayo kwasababu tu za kihistoria
Hivyo Taifa limewekwa rehani na kikundi cha watu ambao wanaungwa mkono na CCM. Hili linasikitisha sana
Swali la kujiuliza, kikundi hiki cha wahafidhina kina umuhimu gani katika Taifa hili kiasi cha kuliweka Taifa njia panda
Hoja ya kwamba, hatutaki misaada haina mashiko. Kama tulijua hivyo, kwanini tuliwekeza sana katika MCC siku za nyuma?
Kuna umuhimu wa kurudi katika katiba, tuandike utaratibu utakaolinusuru Taifa na majanga kama haya
Wakati Tanganyika ikibeba mzigo mzito wa kuhudumia muungano na sehemu ya SMZ , sasa inajikuta inalipa gharama zaidi kutokana na mgogoro wa ZNZ ambao kiuhalisia hauna masilahi na mwananchi wa Tanganyika
Kilichotokea ni kuwatwisha Watanganyika mzigo zaidi licha ya ukweli kuwa wamebeba muungano mzito tayari
Watanganyika wanabebeshwa mzigo huu na CCM iliyoshindwa kukabaliana na wahafidhinaa pengine hawazidi 20
CCM inaweza kuwekwa rehani na wahafidhina kama chama, lakini ni makosa makubwa wahafidhina kuvuka mipaka na kuliweka Taifa rehani.
Haya ni matokeo ya kutumia maguvu na wingi wa CCM kuliko maarifa katika masuala yanayowagusa wananchi.
Tutaendelea hivi hadi lini?
Tusemezane
Inahitaji ustahamilivu kuwa Mtanzania au Mzanzibar mkaazi!Wahafidhina wachache wametuweka 'rehani'
Tulionya, yanatokea sasa.