Mkuu
GalaxyS3
Umetoa hoja nyingi , naomba nizipitie katika mabandiko tofauti
Hoja ya kwanza, kwamba nipo katika uchaguzi na napinga 'ramani' na nataka ichorwe out of thin air nikiwa na lawama
Nakuhakikishia kuwa uchaguzi kwa upande wangu uliisha kabla ya kuanza.
Matokeo yaklikuwepo kabla ya mtu mwingine hajaona.
Nilisema uchaguzi si sanduku la kura ni zaidi ya hapo. Niliandika kwa undani kwanini CCM 'itashinda'
Pili, nahitaji kuona ramani halisi katika blue print, si ramani katika karatasi ya kufungia sigara.
Kinachoendelea si ramani ni mhemuko tu ambao nimesema wazi ATAFELI
Kufanikiwa kwa Rais ni kufanikiwa kwa nchi na kufeli kwake ni kufeli kwa nchi.
Sisi tunaosema ukweli tunamsaidia sana kuona picha kwa ukubwa wake, kuliko wanaomtia matumaini feki kwa kushangilia bila kuona umbali mrefu
Tatizo si nia wala maadili ya kiroho ya watu. Nchi za wenzetu masuala ya kiroho yapo katika nyumba za ibada.
Nchi zao zinaongozwa na sheria kuhakikisha maadili yanafuatwa kisheria na si kumsingizia mungu.
Hakuna nchi iliyo perfect , hata hivyo suala si perfection bali striving for excellence
Nikuonyeshe tatizo la mfumo na jinsi linavyoanza kumkwaza mheshimiwa
1. Suala la Muhimbili :
Kumuondoa mkurugenzi kwasababu MRI hazikufanya kazi miezi zaidi ya 3 si suluhu.
Hakuna ushahidi kama mkurugenzi alizembea kutoomba pesa.
Hakuna ushahidi kama pesa zilitoka akazitumia tofauti
kwa maoni yetu at least, kama upo ushahidi hilo ni suala lingine
Kuna ushahidi kuwa pesa hazikuwepo. Siku alipomteua mkurgenzi mpya aliagiza pesa zitolewe haraka siku hiyo.
Maana yake ni kuwa somewhere somewhat kuna uzembe. Je, uzembe ni wa mkurugenzi peke yake?
Kama aliomba pesa hazina na hakupewa angefanya nini zaidi?
Na kama kuna uzembe hazina, mbona hatua hazikuchuliwa dhidi ya wazembea?
Kama mfumo ungekuwa sahihi, tungekuwa na majibu bila kupepesa.
Kila mmoja angetoka na kuweka wazi wapi tatizo lilipo
Inawezekana pesa zilitumika kununua magari kwa mamia ya jeshi la Polisi. Je, hilo ni tatizo la mkurugenzi?
Iweje mabailioni yatumike kununua magari na zisiwepo pesa za MRI? Je, ni tatizo la mkurugenzi kutoa vipaumbele
Lakini pia, iweje tatizo liwe la mkurugenzi na si katibu mkuu au waziri au uongozi wa juu wa nchi.
Ilikuwaje utawala uliopita haukuona tatizo. Maana yake ni rahisi, mambo yanaamuliwa na watu na si mfumo.
Mkurugenzi ni mtu aliyewajibika kwasababu ya mazingira tu. Kwa undani zaidi mfumo mzima ulifeli
Ilikuwaj bunge la katiba lilitumia mabailioni katika shughuli zake, wakati huo huo zikizkosekana bilioni 2 au 3 za kufanyia marekebisho ya MRI.
Ni mfumo gani ulioruhusu kiasi kikubwa kutumika katika allowance na si MRI ya wananchi
Utaona hadi hapo suala si mtu bali system nzima ilifeli
Huu ni mfano wa kwanza, inafuata mingine