RAIS MAGUFULI NA BUNGE LA JMT
NINI TUTARAJIE
Awali ya yote kuna video hii inayotoa maelezo ya kina kama tulivyowahi kuyaeleza, kuhoji au kuuliza kuhusiana na sakata la uchaguzi wa visiwani (Kwa hisaini ya Mzalendo.net na Channel 10)
Ukweli unapodhihiri - Mzalendo.net
SUALA LA ZNZ
Hoja zote zimetolewa,ni dhahiri kuwa CCM pamoja na kushiniliza uchaguzi urudiwe, kifundi wamekwama
M/kiti wa ZEC iwe yeye au washauri wake, walifanya makosa ya kifundi katika barua ya madai 9 uchaguzi ZNZ kufutwa
1. Tulieleza hapa duru, uchaguzi haufutwi ni takwa la kikatiba.
Uchaguzi unaarihishwa hata kama ni miaka 3 au 4. M/kiti wa ZEC katika taarifa alisema amefuta .
Taarifa ya msemaji wa serikali imesema tume imefuta matokeo.
Hilo lilikuwa kosa la kwanza kiufundi pengine kutokana na haraka au shinikizo
2. Mwnyekiti wa ZEC alitangaza kama yeye, na hakuna kifungu kinachompa malaka hayo.
Tume ni timu si mtu, yeye ni kiongozi tu wa tume si tume kamili. Kosa la kifundi
3. Mwenyekiti wa ZEC hakuanisha kifungu kinachompa mamlaka ya kufuta uchaguzi.
Hili lilikuwa ni kosa kubwa sana kifundi linalohitimisha tatizo zima la mgogoro wa ZNZ
Madai mengine yaliyotolewa hayakuwa na maana au uhusiano na uchaguzi.
Kwamba, mgombe wa CUF kajitangaza, hilo ni kosa la jinai na tume haina mamlaka ya kumshtaki.
Inachoweza kufanya ni kuwa shahidi upande wa mashtaka.
Kwa maneno mengine ni kosa la kisheria linalohusishwa na uchaguzi lakini si kosa la uchaguzi.
Hivyo mkondo wa sheria ndio unaotumika bila kuathhiri matokeo ya uchaguzi
Hoja za wajumbe wa tume kupigana hazina ushahidi wa maeneo wala wahusika.
Hoja za kuibiwa masanduku hazina ushahidi kwasababu hakuna msimamizi wa jimbo aliyelalamika.
Na hoja kuwa vyama vimelalamika, hakuna isipkuwa CCM bila ushahidi,mashahidi wa CCM ni mawakala walio sain matokeo
Na kosa lingine la kifundi ni kutokuwa na malalamikaji kama tulivyo wahi kueleza.
Yule aliyopo hakulalamika katika kituo au jimbo, na alisubiri masaa zaidi ya 48.
Hoja inayozika suala la ZNZ na kuilazimu ZEC kutangaza matokeo ni moja tu.
Mamlaka ya kufuta uchaguzi yamepatikana wapi na kwa njia gani na sababu zipi ndani ya sheria. Jibu ni hakuna, hivyo hakuna budi kutangaza matokeo.
Hili ndilo kosa kiufundi linalozika hoja ya CCM katika mtindo wa 'technical knockout'
Tumekumbusha haya kwasababu Rais atakapofungua bunge hoja ya ZNZ lazima iwe mezani.
Hakuna namna hilo linaweza kukwepeka. Hivyo, tuna angalia hotuba yake katika mtizamo ufuatao
Inaendelea....