Hapa sitozungumzia uhalali au mantiki ya kufutwa uchaguzi ule bali nataka kuzungumzia uhalali wa kikatiba. Hata hivyo, ikiwa nitalazimika kuelezea mantiki, sichelei kusema kwamba ule ni uamuzi wa hovyo kabisa kupata kutokea katika kipindi cha miaka 50 ya uwezo wa Zanzibar.Sehemu ya II
HUMPHREYPOLE POLE NA HOJA ZAKE
1) Mwenyekitiwa ZEC
HP amesema,``mwenyekiti wa ZEC akiwa kama alama `symbol` ya tume alikuwa na haki ya kutumiabusara zake kufuta uchaguzi``
Alipoulizwani kifungu gani cha sheria za uchaguzi ZNZ au katiba kinachompa, HPhana jibu.
Kwa manenomengine hakuna kifungu bali ni fikra zake tu zinazomtuma kuaminihivyo
Hapa kinachonipa hofu si WHAT IF vyama tofauti vitashinda bara na visiwani bali WHAT IF muungano ukivunjika! Uwepo wa vyama tofauti sioni kama ni tatizo provided wote wapo tayari kuulinda muungano... tatizo litakuja pale upande mmoja utakapokosa dhamira ya kuulinda muungano na hivyo kuwa sababu ya kwanza ya kupelekea hofu yangu... WHAT IF muungano ukivunjika!HOJA YA SERIKALI 3 INAPATA NGUVU SASA
CCM walipokataa serikali 3 hawakuweza kuona mbali. Hapa duru tumewahi kuhoji sana, hivi ikiwa vyama tofauti vitashinda bara na visiwani nini itakuwa hatma ya taifa?
Nas nina uhakika ni msomaji mzuri tu maana hoja nyingi 'tunashabihiana kwa maelezo''Mkuu Nguruvi3,
Ni kama hoja zako zilitakiwa kujibiwa na Humphrey Polepole lakini ni kama hujam-mention popote kwa namna ya yeye kuweza kupata notification vinginevyo utakuwa hujamtendea haki. Siifahamu ID yake, ngoja nijaribu: Humphrey Polepole
.......Nas nina uhakika ni msomaji mzuri tu maana hoja nyingi 'tunashabihiana kwa maelezo''
Sikumtaja nikijua fika ni mwanachama wa JF na msomaji mzuri hapa duru
Hata hivyo nakushukuru kwa kumualika. Na mwanzoni tumesema anakaribishwa kabisa kutoa maoni, kutufahamisha, kukanusha , kukemea na chochote ilimradi iwe katrika ustaarab na ukweli. 'Tusiongozwe na uongo kama asemavyo HP, ingawa ni mhubiri mkubwa wa uongo anaoukemea''
Humphrey Polepole karibu sana
Mkuu , siku zote tumewaasa CCM kuwa muungano lazima uwe katika hali ya kisheria na maridhiano.Hapa kinachonipa hofu si WHAT IF vyama tofauti vitashinda bara na visiwani bali WHAT IF muungano ukivunjika! Uwepo wa vyama tofauti sioni kama ni tatizo provided wote wapo tayari kuulinda muungano... tatizo litakuja pale upande mmoja utakapokosa dhamira ya kuulinda muungano na hivyo kuwa sababu ya kwanza ya kupelekea hofu yangu... WHAT IF muungano ukivunjika!
Lakini kuvunjika kwa muungano hakuhalalishwi na utawala wa vyama viwili tofauti pekee bali hata chama kile kile kikiwa kinatawala Zanzibar na Muungano, bado hakutoi guarantee ya muungano wetu kutovunjika hasa tukizingatia kulikuwa na "miungano" imara kabisa duniani ambayo ilidumu kwa miongo kadhaa tofauti na huu wa kwetu lakini siku ilipofika, muungano ulivunjika! Suala la Scotland kutaka kujitenga from UK limepitiliza level ya kuita ni red flag kwetu bali ni time bomb!
Now, let's assume LEO muungano unavunjika; je CCM watakuwa tayari kuunda serikali ya mpito instantly kwa kuwa tayari Magufuli atakuwa amepoteza uhalali wa kuongoza kv alipigiwa kura bara na visiwani?! Ni kwa muda gani CHADEMA watavumilia kusubiri uchaguzi mwingine kuitishwa na utaitishwa kwa katiba ipi?
God forbid-- hilo likitokea manake hata katiba iliyopo ita-cease kufanya kazi na taasisi pekee inayoweza kuongoza nchi pasipo na katiba ni jeshi pekee huku "wakisubiri" wanasiasa wa-resolve issues zao!
Mimi bado nina maswali. Hivi mbunge, diwani wanawezaje kuwa wa upande mmoja, Rais akachaguliwa upande mwingine. Je, Watanzania wanachagua sura au seraNasDaz,
..asante kwa mchango wako hapo juu.
..mimi bado naugulia kipigo tulichopata huku Tanganyika.
..kwa kweli siko sawasawa sasa hivi siwezi kuchangia ya Znz.
(6) To ensure equality before the law, the state authority shall make procedures which are appropriate or which take into account the following principles, namely (a) when the rights and duties of any person are being determined by the court or any other agency, that person shall be entitled to a fair
hearing and to the right of appeal or other legal remedy against thedecision of the court or of the other agency concerned;
(6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatiamisingi kwamba -(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitajikufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombokinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa nahaki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, napia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine yakisheria kutokana na maamuzi ya mahakama auchombo hicho kingenecho kinachohusika
Nguruvi3,NasDaz Hapo bandiko 25 umeelezea mambo mawili.
Kwanza mantiki ya suala la ZNZ na pili, uhalali wa kikatiba
Nichangie tena kidogo
Kimantiki:
Watu waelewe uchaguzi ni takwa la kikatiba iwe ya JMT au ZNZ. Imeanishwa kikatiba na ndivyo ilivyo
Uchaguzi hauwezi kufutwa kwasababu tayari ni takwa la kikatiba.
Ili uchaguzi ufutwe ni lazima kifungu kinachosema ' kutakuwepo na uchaguzi...' katika katiba zetu kifutwe kwanza
Vinginevyo midhali kifungu hicho kipo intact , uchaguzi haufutwi. Kinachofanyika ni Uchaguzi kuahirishwa
Kwa mfano, ikibainika taratibu za uchaguzi zimekiukwa na uchaguzi hauwezi kufanyika siku hiyo kabla ya kupiga kura, uchaguzi unaahirishwa hata kama ni miaka 5, haufutwi kwasababu tayari ni takwa la kikatiba na lazima lifanyike ili katiba iwe hai
Ikitokea asilimia 95 ya maeneo yana matatizo baada ya kupiga kura, uchaguzi haufutwi bali unaahirishwa katika maeneo husika. Ndio mantiki ya neno kuahirishwa na si kufutwa na ndio maana wasimimazi wa vitu na majimbo wamepewa nguvu hiyo.
Sasa kama ZNZ kuna matatizo majimbo kadhaa na imegundulika baada ya kupiga kura, kinachofuata ni kuahirisha uchaguzi wa maeneo hayo husika na si kufuta uchaguzi mzima.
Tukiendeleza dhana inayotawala ya kufuta uchaguzi ambayo kikatiba haionekani, tutaingia katika matatizo makubwa.
Ipo siku mkoa wa Tanga au Mtwara kutakuwa na matatizo, na italazimu uchaguzi mzima ufutwe.
Hili kimantiki halipo, kilichopo ni uchaguzi kuahrishwa maeneo husika
Kisheria
Kama ulivyoonyesha hapo, mwenyekiti alifuta uchaguzi kama yeye. Humphrey Poleppole anasema ni symbo ya tume na hivyo ana uwezo wa kutumia busara zake kufuta uchaguzi. Ukisoma sheria ulizoweka, mwenyekiti hakupewa nguvu hiyo
Ukisoma barua aliyotumia kufuta uchaguzi, hakusema kwa mamlaka ya tume, alisema kwa mamlaka kama mwenyekiti
Hapa ndipo tunamuuliza Humphrey Polepole, kama ametumia neno mamlaka ina maana kuna kifungu cha sheria kinachompa mtu mamalka hayo.
Ni kipi hicho? Humphrey hakukionyesha alichosema ni kuwa mwenyekiti kama symbol ametumia busara
Kama ametumia busara, ilipaswa aandike kuwa 'kwa busara zake' amefuta uchaguzi.
Hata hivyo, tungemuuliza busara zinazotokana na kifungu gani cha sheria?
Kuna kitu kinaitwa 'Prerogative' yaani mamlaka au nguvu maalumu anazopewa kiongozi katika kutekeleza majukumu yake
Kwa mfano, nchi kwenda vitani inahitaji kupata kibali cha Rais kufanya hivyo.
Hata hivyo Rais ana prerogative ya kuamua kupeleka jeshi kabla ya hapo kwa kutumia busara, si mamlaka ya busara
Hii maana yake ni kuwa Rais anapewa nguvu fulani ya kumwezesha kutekeleza majukumu yake. Nguvu hizo zipo kisheria
Anpofanya hivyo anatumia prerogative akiongozwa na busara, si busara zake tu kwakuwa ameamua hivyo kama Humphrey anavyouaminisha ulimwengu
Sasa, swali linakuja, kufuatana na vifungu alivyonukuu NasDaz hapo bandijo 25, ni wapi mwenyekiti wa tume amekaa hata na wajumbe wake 3 tu na kufikia hitimisho la kufuta uchaguzi?
Hapa ieleweke kufuta tu si sahihi, bali usahihi ni kuahirisha. Hata kama uchaguzi mzima wa ZNZ ungekuwa na matatizo na tume kwa ujumla wake wakaamua urudiwe, haiwezi kusemwa umefutwa, bali umeahirishwa kwasababu ni takwa la kikatiba kwamba siku moja lazima ufanyike
Tusemezane
Hili la mbunge kuangukia chama kingine na rais chama kingine ni jambo la kawaida kabisa! Binafsi, sikumpigia Lowassa kwa sababu ambazo tayari nilishazieleza hapa jamvini lakini hata hivyo ubunge na udiwani nilipigia upinzani! Kuna bro wangu yeye ni mtu wa kawaida kabisa... I hope unanielewa namaanisha nini! Yeye nilipomuhoji akasema wazi kwamba Urais amempigia Magufuri lakini ubunge na udiwani akampigia mtu wa UKAWA!Mimi bado nina maswali. Hivi mbunge, diwani wanawezaje kuwa wa upande mmoja, Rais akachaguliwa upande mwingine. Je, Watanzania wanachagua sura au sera
Hivi Jiji linawezaje kuangukia upande mmoja, halafu Urais uka angukia upande wa pili