Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Mitandao ya kijamii imeshinda televisheni kama chombo cha kusambaza habari kwa vijana, kilingana na ripoti.
Vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 walihojiwa, asilimia 28 walisema njia yao ya kupata habari ni kupitia mitandao ya kijamii ikilinganishwa na asilimia 24 kwa runinga.
Chuo cha Taasisi ya Reuters cha Uandishi wa habari, pia kimependekeza kuwa asilimia 51 ya watu wenye uwezo wa kutembelea mitandao hutumia mitandao ya kijamii kupata habari.
Ongezeko la utumizi wa simu za rununu ili kupata habari umekandamiza mfumo wa kibiashara wa hapo awali.
Ripoti hiyo, kwa mwaka wake wa tano sasa, imefanywa na shirika la utafiti la YouGov, ambalo liliwahoji watu elfu 50 kote ulimwenguni, wakiwemo waingereza elfu 2.
Katika ufunguzi wake ripoti hiyo inasema pigo hili la pili imekuwa pigo kwa mashirika ya habari kote ulimwenguni na kuna uwezekano wa athari kubwa kwa wachapishaji na wazalishaji habari katika siku zijazo.