Mitandao ya simu mnaibia wateja

Mitandao ya simu mnaibia wateja

Ni dhahiri kwa sasa ukiweka bundle linaisha kwa haraka kwenye data, na sababu ni Makampuni ya simu kuibia wateja Mchezo huu umekithiri sana sasa kuelekea uchaguzi.

Ni kosa makampuni ya simu kifanya wizi wa kidola dhidi ya watumiaji
Hawa voda ndiyo balaaa. Ukiweka 700mb sasa hivi, dakika kumi kuperuzi jf tu ni nyingi kabla hawajakupekekea ujumbe mb zako zimeisha.
 
Nina ufahamu wa kutosha kuhusu speed za internet. Sibahatishi nisemacho. Hakuna ufahari wa kuibiwa na kusema hujali kisa utakuwa na fedha nyingi.
sina pesa ila nina tumia chini ya mb500 pekee kwa wiki nzima na haziishi gentleman,
na niko na wewe humu humu jukwaani kutwa kuchwa 🐒
 
Yamenikuta haya juzi 1.4gb iliisha ndani ya dk 5 na sikuwa nadownload chochote. Yas endeleeni kutumixx.
Hao ovyo sana.
Walinibandika na deni kubwa wakidai nina mkopo wakati hata sijui hicho kitu mkopo kwao.
 
Wakati mwingine tunailaumu mitandao ya simu kwamba wanaiba data kumbe tatizo ni sisi.

Kama unatumia mtandao wa simu kupata huduma za data, fanya yafuatayo ili data yako isiishe upesi:
  1. Zima data taustani (background data) kwa apps ambazo huzitumii mara kwa mara.
  2. Tumia toleo la "lite" la apps kama Facebook Lite, Instagram Lite, nk.
  3. Epuka kuangalia video za HD au kuzipakua bila sababu ya msingi.
  4. Tumia Wi-Fi unapopata nafasi badala ya kutumia data ya simu kila mara.
  5. Zima auto-update ya apps kupitia data; badili iwe Wi-Fi tu.
  6. Funga auto-play ya video kwenye mitandao ya kijamii kama TikTok, Instagram, na Facebook.
  7. Tumia Data Saver Mode ikiwa simu yako inayo.
  8. Fuatilia matumizi ya data kwa kutumia mipangilio ya simu au apps za mtandao wako.
Yote hayo nimefanya. Huwa sichezi clip zozote. Sina app yoyote ambayo sina ufahamu nayo boss wangu.
 
sina pesa ila nina tumia chini ya mb500 pekee kwa wiki nzima na haziishi gentleman,
na niko na wewe humu humu jukwaani kutwa kuchwa 🐒
Usiwe mjinga ww.
 
Yote hayo nimefanya. Huwa sichezi clip zozote. Sina app yoyote ambayo sina ufahamu nayo boss wangu.
Sawa mkuu. Changamoto kubwa inakuja pale unapotaka kupeleka malalamiko ya namna hii kwa mtoa huduma wako wa simu. Ni lazima uwe na ushahidi wa uhakika ili kuthibitisha madai yako kwamba kweli data unazopewa zinatumika kiwivi. Vinginevyo, unapaswa kujiridhisha kwa kufuatilia matumizi halisi ya data kwenye kila aplikesheni. Unaweza kupata ripoti kamili ya matumizi ya data kwenye simu yako itakayokuonyesha kama kweli aplikesheni zako hazitumii data hata kwa nyuma (background), lakini ukikabidhiwa kifurushi, data inaisha ghafla ndani ya muda mfupi.


Njia rahisi zaidi ni kutumia programu maalumu za kusimamia matumizi ya data (mfano: Data Usage Manager au My Data Manager) zinazokupa ripoti sahihi ya matumizi ya kila app. Hata mimi mwanzoni nilikuwa na wasiwasi kuwa mtandao unanipunja, lakini baada ya kufanya ukaguzi wa kina kwenye simu yangu, niligundua tatizo kubwa lilikuwa kwenye apps zinazotumia data kwa siri (background apps). Ukweli ni kwamba hili ndilo tatizo linalowakumba watumiaji wengi zaidi kuliko kufikiri kuwa wanaibiwa na mitandao.


Kumbuka, ukipeleka malalamiko, watahitaji uthibitisho wa madai yako, hivyo ni muhimu kuwa na ushahidi wa kutosha kabla ya kulalamika rasmi.
 
Ni dhahiri kwa sasa ukiweka bundle linaisha kwa haraka kwenye data, na sababu ni Makampuni ya simu kuibia wateja Mchezo huu umekithiri sana sasa kuelekea uchaguzi.

Ni kosa makampuni ya simu kifanya wizi wa kidola dhidi ya watumiaji
Vodafone ni vinara wa huu wizi wakifuatwa na Yaas. Hii Wizara haijapata Waziri wa kueleweka wa kuisimamia. Wangemruhusu Musk aje na Starlink ili tuzike rasmi huu mitandao ya kipigaji.
 
Hii huwezi kusikia inapigiwa kelele na Wakuu wahusika
 
Back
Top Bottom