beal,Shukrani kwa taarifa! Kumbe ndio maana umeme unakatikakatika! Sijui kitengo cha Tanesco customer care kazi yake ni nini! Manake ukiwauliza wanatoa majibu mepesi eti kuna kazi maalumu ya kukata miti kandokando ya nguzo za umeme!
Mheshimiwa Lowasa alishanawa mikono na kujitoa katika sakata la mitambo hiyo kwa kumtaja swaiba wake kuwa ndiye aliyelazimisha mitambo hiyo mibovu inunuliwe! Ukweli umedhihirika hivi karibu wakati wa ziara ya rais Obama nchini kwa kuitembelea mitambo hiyo mibovu!
Ha haa haaa,mkuu umenifurahisha..nadhani alikuwa ana maanisha moto ulianza 5.45a:m, ila magari yalifika saa 9:00a.m....mawazo yalikuwa kwenye kiswahili,mikono ilikuwa kwenye kiingereza
Mi nadhani wewe ndio umechanganya hapa!
Moto ulianza saa tisa usiku/alfajiri na fire walifika saa kumi na mbili kasoro asubuhi!!
Fire starts 3:00 am na fire brigades arrived 5:45 am.
Ni kitu cha kawaida kwenye storage zap gas moto kutokea.....Wanatakiwa kujipanga tu linapotokea jambo kama hilo wanalikabili mapema bila kuleta madhara......I worked over 20 years on that Field
...Mkuu, Mgawo uliishaanza kitambo kwa kisingizio cha kukata miti inayogusana na Nyaya za Umeme. Kwa tukio hili sasa Mgawo umehalalishwa Rasmi. Poor We.