Mitambo Dowans bado ya Richmond | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitambo Dowans bado ya Richmond

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 5, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Mitambo Dowans bado ya Richmond

  *Rostam Aziz atajwa hukumu ya ICC

  Na Mwandishi Wetu

  WAKATI serikali ikisubiriwa kutoa msimamo kama ama italipa sh. bilioni 185 kama tuzo kwa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans au la, imebainika kuwa
  moja kati ya mitambo husika katika sakata hilo bado ni mali ya Richmond Development Company (RDEVCO L.L.C).

  Taarifa za uchunguzi zilizolifikia Majira zimethibitisha pasipo shaka kuwa mtambo huo wa kutumia gesi wenye namba TM2500 bado ni mali ya Richmond, na kuna kipindi kampuni hiyo iliyoshindwa kazi na kuhamishia mkataba wake kwa Dowans ililizuia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) lisinunue mtambo huo kwa kuwa ni mali yake.

  Vyanzo mbalimbali vya habari vimelieleza Majira kuwa kulingana na vielelezo vilivyopatikana, wakati wote serikali ilipokuwa inadhani inashughulika na Dowans, kumbe ilikuwa bado inacheza na Richmond ile ile.

  “Nakwambia hawa ni ndugu moja, na hizi taarifa tuinazopata ni pale tu waliposhindwa kuelewana. Kwa hiyo tara serikali ikimlipa Dowans, fedha za walipa kodi zitakuwa zinaingia Richmond, kilisema chanzo chetu kimojawapo.

  Oktoba 14, 2006 kampuni ya RDEVCO L.L.C ya Texas, Marekani ilitiliana saini mkataba na Kampuni ya Dowans Holdings S.A ya Costa Rica ili kuhamisha mkataba kati yake na TANESCO, kuhamisha umiliki wa mitambo hiyo na kuikabidhi mikoba yote kuhusiana na uendeshaji, uzalishaji na uuzaji wa umeme wa dharura.

  Tangu wakati huo, Dowans imeendelea kutambuliwa kuwa ndiyo iliyokuwa inatekeleza majukumu ya Richmond na hata baada ya mkataba wake kusitishwa na serikali, ndiyo ilikwenda Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC-Court) dhidi ya TANESCO na kudai fidia, hatua ambayo imesababisha shirika hilo la umeme kuhukumiwa kulipa sh. bilioni 185.

  Hata hivyo, baadhi ya wanasheria wameshangaa hatua hiyo wakisema kuwa Richmond na Dowans bado ni washirika na kubainisha kuwa licha kuwapo kwa mkataba huo wa kuhamishiana majukumu, uliosainiwa na Dkt. Mohamed S. Huque kwa niaba ya Richmond na HenrySurtee kwa niaba ya Dowans.

  Wanasheria hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe gazetini wamelieleza gazeti hili kuwa miaka miwili baada ya mkataba kati ya kampuni hizo kusainiwa, Richmond iliiandikia barua TANESCO kuitaarifu kuwa isinunue mtambo huo kutoka Dowans (kama ilivyokuwa imesikia uvumi), kwa sababu mtambo huo bado ni mali yake.

  Barua hiyo iliyoandikwa na Kampuni ya Wanasheria ya KLPATRICK STOCKTON LLP Oktoba 18, 2008 kwa niaba ya RDEVCO, L.L.C ilisema: “Lengo la barua hii ni kuifahamisha TANESCO kwamba Dowans si mmiliki wa mtambo mmojawapo katika eneo hilo, GE TM2500 S/n 481-364, 7LM2500-PE-MDW GE Unit. Mtambo huo unamilikiwa na RDEVCO, L.L.C.”

  Barua hiyo iliyosainiwa na Thomas Philip Wilson kama wakili wa RDEVCO, L.L.C ilielekezwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Idris Rashid na kupokewa Oktoba 20, 2008.

  “Kitendo cha Richmond kuzuia kuuzwa kwa mtambo huo, kimetoa mwanga kuwa kampuni hiyo iliyoshindwa kazi na kuhamisha mkataba wake, bado ni mmiliki halali wa mitambo hiyo, jambo ambalo linathibitisha kuwa kampuni hizo bado ni ndugu, na huenda malipo yanayodaiwa kwa serikali yanakwenda kwa Richmond.

  Katika hatua nyingine, wakati swali la ‘Dowans ni nani’ likiulizwa bila majibu, imefahamika kuwa jina la Rostam Aziz limetajwa katika hukumu ya ICC akielezewa kama mtu mwenye ‘ushawishi’ kiasi cha kuhamishia mkataba kwa kampuni hiyo (kutoka Richmond) bila kufuata Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004.

  Kulingana na vyanzo mbalimbali, ICC ilikubaliana na hoja kuwa Bw. Aziz alikuwa na ‘nguvu’ nyingi na ushawishi mkubwa hadi kubadili mkataba kwenda kwa ‘rafiki yake na yeye mwenyewe’ kupitia kwa mdai (Dowans) na kumlainisha Waziri wa Nishati na Madini ili amlazimishe mwakilishi wa TANESCO, Bw. J. C Lottering kusaini mkataba kati yake na Richmond Juni 23, 2006.

  Taarifa kutoka ndani ya Kampuni ya Uwakili ya Rex Attoneys iliyowakilisha TANESCO katika shauri hilo, zinasema kuwa ICC ilipokea kiapo cha Bw. Lottering aliyekuwa mwajiriwa wa NET Group Solutions, kuwa hata kwa kutumia sheria ya kimataifa ya zabuni, ambayo ni ya wazi, isiyo na ufanisi na ndefu, TANESCO ingeweza kuingiza mitambo hiyo, bila matatizo, na kwa kipindi kifupi kuliko miezi 18 iliyodaiwa na Waziri wa Nishati na Madini.

  Hata hivyo, vyanzo vyetu vimelieleza gazeti hili kuwa pamoja na TANESCO kushindwa katika shauri hilo, kampuni ya Rex Attoneys imeishauri serikali kupinga hukumu hiyo katika mahakama za Tanzania kwa hoja kwamba suala la muda wa kuingiza mitambo na uhalali wa mkataba husika ni kinyume cha sera ya serikali na maslahi ya umma, mambo ambayo hata hivyo hayaelezwi katika vifungu vya sheria.

  Katika ushauri wa kampuni hiyo kwa TANESCO ambayo gazeti hili limeona, wanasheria wa Rex Attoneys wameshauri kuwa hatua hiyo inawezekana kutokana na mazingira yafuatayo:

  “Kwa kuwa ICC iliridhika na ushahidi wa Bw. Lottering aliyedai kutishiwa ‘jambo baya’ endapo asingesaini mkataba kati ya Richmond na TANESCO, na kuwa Bw. Rostam Aziz alitumia nguvu na ushawishi kuhamisha mkataba bila kufuata sheria.

  “Lakini mtazamo huo utategemea na utayari wa mahakama za Tanzania kwa kuwa hakuna sheria nchini inayozungumzia sera ya serikali kama hoja za kubatilisha malipo kwa Dowans.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Kiungo muhimu hapa ni JK kupitia Dr. Idrissa Rashid na Rostam Aziz.............sisi tulishinikize bunge lifute kazi JK na siri zote zitaanikwa kila mahali.....................
   
 3. h

  hoyce JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  *Rostam Aziz atajwa hukumu ya ICC

  Na Mwandishi Wetu

  WAKATI serikali ikisubiriwa kutoa msimamo kama ama italipa sh. bilioni 185 kama tuzo kwa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans au la, imebainika kuwa moja kati ya mitambo husika katika sakata hilo bado ni mali ya Richmond Development Company (RDEVCO L.L.C).

  Taarifa za uchunguzi zilizolifikia Majira zimethibitisha pasipo shaka kuwa mtambo huo wa kutumia gesi wenye namba TM2500 bado ni mali ya Richmond, na kuna kipindi kampuni hiyo iliyoshindwa kazi na kuhamishia mkataba wake kwa Dowans ililizuia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) lisinunue mtambo huo kwa kuwa ni mali yake.

  Vyanzo mbalimbali vya habari vimelieleza Majira kuwa kulingana na vielelezo vilivyopatikana, wakati wote serikali ilipokuwa inadhani inashughulika na Dowans, kumbe ilikuwa bado inacheza na Richmond ile ile.

  “Nakwambia hawa ni ndugu moja, na hizi taarifa tuinazopata ni pale tu waliposhindwa kuelewana. Kwa hiyo tara serikali ikimlipa Dowans, fedha za walipa kodi zitakuwa zinaingia Richmond, kilisema chanzo chetu kimojawapo.

  Oktoba 14, 2006 kampuni ya RDEVCO L.L.C ya Texas, Marekani ilitiliana saini mkataba na Kampuni ya Dowans Holdings S.A ya Costa Rica ili kuhamisha mkataba kati yake na TANESCO, kuhamisha umiliki wa mitambo hiyo na kuikabidhi mikoba yote kuhusiana na uendeshaji, uzalishaji na uuzaji wa umeme wa dharura.

  Tangu wakati huo, Dowans imeendelea kutambuliwa kuwa ndiyo iliyokuwa inatekeleza majukumu ya Richmond na hata baada ya mkataba wake kusitishwa na serikali, ndiyo ilikwenda Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC-Court) dhidi ya TANESCO na kudai fidia, hatua ambayo imesababisha shirika hilo la umeme kuhukumiwa kulipa sh. bilioni 185.

  Hata hivyo, baadhi ya wanasheria wameshangaa hatua hiyo wakisema kuwa Richmond na Dowans bado ni washirika na kubainisha kuwa licha kuwapo kwa mkataba huo wa kuhamishiana majukumu, uliosainiwa na Dkt. Mohamed S. Huque kwa niaba ya Richmond na HenrySurtee kwa niaba ya Dowans.

  Wanasheria hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe gazetini wamelieleza gazeti hili kuwa miaka miwili baada ya mkataba kati ya kampuni hizo kusainiwa, Richmond iliiandikia barua TANESCO kuitaarifu kuwa isinunue mtambo huo kutoka Dowans (kama ilivyokuwa imesikia uvumi), kwa sababu mtambo huo bado ni mali yake.

  Barua hiyo iliyoandikwa na Kampuni ya Wanasheria ya KLPATRICK STOCKTON LLP Oktoba 18, 2008 kwa niaba ya RDEVCO, L.L.C ilisema: “Lengo la barua hii ni kuifahamisha TANESCO kwamba Dowans si mmiliki wa mtambo mmojawapo katika eneo hilo, GE TM2500 S/n 481-364, 7LM2500-PE-MDW GE Unit. Mtambo huo unamilikiwa na RDEVCO, L.L.C.”

  Barua hiyo iliyosainiwa na Thomas Philip Wilson kama wakili wa RDEVCO, L.L.C ilielekezwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Idris Rashid na kupokewa Oktoba 20, 2008.

  “Kitendo cha Richmond kuzuia kuuzwa kwa mtambo huo, kimetoa mwanga kuwa kampuni hiyo iliyoshindwa kazi na kuhamisha mkataba wake, bado ni mmiliki halali wa mitambo hiyo, jambo ambalo linathibitisha kuwa kampuni hizo bado ni ndugu, na huenda malipo yanayodaiwa kwa serikali yanakwenda kwa Richmond.

  Katika hatua nyingine, wakati swali la ‘Dowans ni nani’ likiulizwa bila majibu, imefahamika kuwa jina la Rostam Aziz limetajwa katika hukumu ya ICC akielezewa kama mtu mwenye ‘ushawishi’ kiasi cha kuhamishia mkataba kwa kampuni hiyo (kutoka Richmond) bila kufuata Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004.

  Kulingana na vyanzo mbalimbali, ICC ilikubaliana na hoja kuwa Bw. Aziz alikuwa na ‘nguvu’ nyingi na ushawishi mkubwa hadi kubadili mkataba kwenda kwa ‘rafiki yake na yeye mwenyewe’ kupitia kwa mdai (Dowans) na kumlainisha Waziri wa Nishati na Madini ili amlazimishe mwakilishi wa TANESCO, Bw. J. C Lottering kusaini mkataba kati yake na Richmond Juni 23, 2006.

  Taarifa kutoka ndani ya Kampuni ya Uwakili ya Rex Attoneys iliyowakilisha TANESCO katika shauri hilo, zinasema kuwa ICC ilipokea kiapo cha Bw. Lottering aliyekuwa mwajiriwa wa NET Group Solutions, kuwa hata kwa kutumia sheria ya kimataifa ya zabuni, ambayo ni ya wazi, isiyo na ufanisi na ndefu, TANESCO ingeweza kuingiza mitambo hiyo, bila matatizo, na kwa kipindi kifupi kuliko miezi 18 iliyodaiwa na Waziri wa Nishati na Madini.

  Hata hivyo, vyanzo vyetu vimelieleza gazeti hili kuwa pamoja na TANESCO kushindwa katika shauri hilo, kampuni ya Rex Attoneys imeishauri serikali kupinga hukumu hiyo katika mahakama za Tanzania kwa hoja kwamba suala la muda wa kuingiza mitambo na uhalali wa mkataba husika ni kinyume cha sera ya serikali na maslahi ya umma, mambo ambayo hata hivyo hayaelezwi katika vifungu vya sheria.

  Katika ushauri wa kampuni hiyo kwa TANESCO ambayo gazeti hili limeona, wanasheria wa Rex Attoneys wameshauri kuwa hatua hiyo inawezekana kutokana na mazingira yafuatayo:

  “Kwa kuwa ICC iliridhika na ushahidi wa Bw. Lottering aliyedai kutishiwa ‘jambo baya’ endapo asingesaini mkataba kati ya Richmond na TANESCO, na kuwa Bw. Rostam Aziz alitumia nguvu na ushawishi kuhamisha mkataba bila kufuata sheria.

  “Lakini mtazamo huo utategemea na utayari wa mahakama za Tanzania kwa kuwa hakuna sheria nchini inayozungumzia sera ya serikali kama hoja za kubatilisha malipo kwa Dowans.

  Source" Majira
   
 4. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45

  source: majira
   
Loading...