Mitafaruku bungeni

Mitafaruku bungeni

The Conspire

Member
Joined
Nov 15, 2012
Posts
6
Reaction score
3
Kwa wale wanaofuatilia shughuli za Bunge, nadhani watakubaliana na ukweli kuwa wazee wa miongozo ni chanzo cha mitafaruku ndani ya Bunge.
 
Kwa wale wanaofuatilia shughuli za Bunge, nadhani watakubaliana na ukweli kuwa wazee wa miongozo ni chanzo cha mitafaruku ndani ya Bunge.
Kwa sisi ambao tupo mbali na TV/Redio kwa ni ni usituwekee kilichojili?
 
Kwani ni vipi mleta mada?

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Maelezo hayajakamilika bado toa yanayojiri ndo uhabarishaji mzuri co wote wanafuatilia wengine tupo kimtandao zaidi!
 
Kwa wale wanaofuatilia shughuli za Bunge, nadhani watakubaliana na ukweli kuwa wazee wa miongozo ni chanzo cha mitafaruku ndani ya Bunge.
wewe kajipange upya, vurugu bungeni zinachangiwa na spika na naibu spika kutotenda haki. Miongozo ina umuhimu wake, ndo maana iliwekwa kwenye kanuni za bunge!
 
Jinsi maelezo yasivyojitosheleza, ndivyo na akili ya mleta mada isivyomtosheleza
 
Kwa wale wanaofuatilia shughuli za Bunge, nadhani watakubaliana na ukweli kuwa wazee wa miongozo ni chanzo cha mitafaruku ndani ya Bunge.

Wewe wa wapi wewe?? UNafuatilia na mabunge mengine? Huo ndo upinzani na maana ya kukua kwa demokrasia na uelewa wa watu, hakuna mambo ya ndiyo mzee. Kumbuka kauli ya Kangi Lugola, kuwa kila silu wanaunga mkono bajeti asilimia 100 lakini hakuna kinachofanyika, funguka mkuu.
 
Kuhusiana na kuwa husishahao unao waita wazee wa mingozo na kile kilicho tokea bunge hebu jaribu kuona kauli ya spika na hoja yako na utuhakikishie kuwa ni wapi hao waliomba muongozo kwa wewe umeona ni tatizo wakati mwingine tukubaliane na ukweli hata kama haupendi ilimradi ni ukweni meza kama dawa kwa kuwa sababu ya kumeza dawa ni ili upone kwa hiyo kwenye bunge letu kuna wanao paswa kumeza dozi hizi wanao pewa ili waweze kupona.
Pitia hili la spika hapa chini.
Tumeona Spika akisema kuwa angeshangaa kuona kama wabunge wasingeuliza maswali hayo ya msingi. Pia amekubaliana nao. Lakini wasingeuliza ili kutimiza mshangao wake basi hatujui ingekuwaje na huenda ingekuwa kama ilivyoelekea kuwa.

Sasa, kama Spika alijua kuwa haya ni maswali ya msingi na ya kikanuni, hebu angalia walioyauliza (Zitto, Tundu, Mnyika). Wote ni Chadema.

Utaachaje kusema kwamba alichotarajia hoja yamsingi kama ile isiulizwe na wabunge kwa kweli kwa namna moja ni sawa na yeye kujua kwamba haiwezekani hoja ya msingi ipite kimya mle bila Chadema kuuliza.

Hakuna CCM hata mmoja aliyeinuka kusema lolote katika haya ambapo yasingesemwa yangepita hivi hivi tu kama ilivyoelekea.
 
Tumekuwa na bunge tulivu kwa takriban miaka 50.....limetusaidia nini....tumefanikiwa kuzidi kuwa masikini wakati wachache wakiwa matajiri wa kutupwa. So hiyo miongozo na fujo za bungeni zilikosekana ndo maana tumegeuzwa matahira....sasa kwa bahati mbaya vurugu sio bungeni tu....hata mitaani...na sio Arusha tu, hata kusini.....watanzania taratibu tunazinduka usingizini.....
 
kwa wale wanaofuatilia shughuli za bunge, nadhani watakubaliana na ukweli kuwa wazee wa miongozo ni chanzo cha mitafaruku ndani ya bunge.
kwa wale mnaofuatilia mijadala ya jf mtakubaliana na mimi mtoa mada ni kilaza na thread yake haina hadhi ya kukaaa jf!!!!!!!! Apeleke facebook waliko watoto wenzie au kama sivyo mambo ya buku 7 kutoka lumumba ccm ofisi ndogo.
 
Kwa wale wanaofuatilia shughuli za Bunge, nadhani watakubaliana na ukweli kuwa wazee wa miongozo ni chanzo cha mitafaruku ndani ya Bunge.

Ninapata wasi wasi na ufahamu wako, sijawahi ona bunge lolote duniani lisilokuwa na Miongozi. Ungependekeza sheria na taratibu za bunge zivunjwe ili kuondoa mitafaruku.
 
Back
Top Bottom