Tanzania haina mitaala, period. Si primary, secondary wala university. Kwa elimu kama hii, na kwa mitaala kama hii, ni vigumu kuwa na taifa linalojitegemea. Hivi ni nani katuloga? Hawa wanaoitwa wataalamu, si wataalam kitu, watakuwa feki. Professor wa chuo kikuu na mwanasiasa huwezi tofautisha ufikiri wao. Maprofessor wetu kwa namna walivyojitengenezea ka-himaya ambako si rahisi kwa hali ya kawaida mtu mwingine kuwa kama wao, fikra zao sasa ni kudumisha mila badala ya kufikiria mahitaji ya dunia. Dunia inabadilika haraka sana, kwa hiyo bila kufikiria na kutenda haraka sana ipasavyo, ni vigumu sana kwenda na dunia, ndio maana mtu akija Tanzania au nchi nyingi za Kiafrika, utaona kila kitu cha zamani sana.
Mimi nashauri tu kwamba, wote wanaojiita wataalam wajifanyie tathmini ya dhati kwanza halafu wakae wfanye tathmini juu ya mifumo kongwe ya elimu kisha waone namna ambavyo twawezapata mfumo wetu wa elimu utaotuwezesha kumudu changamoto za karne ya 21. Kwa hali ilivyo, ni vigumu kuendelea kutegemea fikra na mtazamo wa miaka ya 1960 wakati dunia iko mbali sana.
Ninayo mengi lakini naomba niishie hapa, hii mada ni nyeti nadhani mjadala uendeleee