Mita za kwenye nguzo tabu tupu

Mita za kwenye nguzo tabu tupu

samakinchanga

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2014
Posts
2,024
Reaction score
1,237
Tanesco kupitia REA wametuwekea Umeme huku vijijin lakin mita zimewekwa juuu kwenye nguzo sijui sababu nini lakini kukatika umeme ndio balaa yaweza tokea Mara kumi hivi ni nini hii tanesco.inakera inaudhi.
 
Hujapewa mashine ya kusomea umeme na kuwekea ?
 
hzo mita ni chenga hazifai hata kidogo sio kwamba unakatika bali umeme ukiwa mdogo zinakata umeme mala nyingi inatokea wakati wa usiku. iyo ondoa tupa mkuu
 
Mimi natumia ziko poa. Uswazi ndo shida. Sehemu zenye population kubwa ni shida
 
Kuwekwa mita juu ya nguzo wanakwepa watu wanachakachua mita, halafu suala lla kukatika katika umeme kama unakatika nyumba zote Hilo Ni tatizo la tanesco, lakini kama Ni nyumba yako Tu ndio inayokatika hiyo inatokana umeme kuwa low voltage hii inatokea Sana kwa mita hizi mpya, au nyumba yako Ina matumizi makubwa kiasi inahitaji kufungwa mita ya 3phase.
 
Mita za hivi zipo pia maeneo yaliyokuwa na umeme toka kitambo kama moshi mjini, nilikwenda home decemba nikashangaa Mita imewekwa juu ya nguzo wenyewe wanasema wanazuia uchakachuaji.
 
Tanesco kupitia REA wametuwekea Umeme huku vijijin lakin mita zimewekwa juuu kwenye nguzo sijui sababu nini lakini kukatika umeme ndio balaa yaweza tokea Mara kumi hivi ni nini hii tanesco.inakera inaudhi.

Mkuu huku Mbeya ndiyo yametapakaa mamita hayo. Umeme ni full kukatika utafikiri kuna mgao. TANESCO tunajua kuwa hili tatizo mnalitambua, chukueni hatua madhubuti kutuondolea adha hii!! Watoto wanashindwa hata kujisomea!!
 
Labda Kwa kuwa ni msaada toka kwa watu wa marekani.inaudhi jamani sie huku vijijini kuna simba kakiwaka kaumeme inakuwa nafuu .hebu badilisheni mita zenu
 
tanesco badilisheni hizi mita zina kata umeme bila mpango!!!
 
Wakuu hizi mita za kwenye nguzo ndio zipoje?
ni kama za luku au? na kama ni za luku ......
nisaidieni kwanza kabla sijauliza la pili..
 
Back
Top Bottom