Mita ya TANESCO na ununuaji wa Luku

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
Ukifunga mita ya TANESCO hii ya Luku kwa mfano mita nimefunga mbezi, alafu nikahama Mbezi na mita yangu nikahamia labda magomeni na hiyo mita, nimesikie eti ni hadi nikahamishe location ya mita ili niweze kununulia umeme sehemu niliohamia bila hivyo siwezi pata hiyo huduma kwa hapo nitakapohamia.

Sasa swali ni hili. Je, inakuwaje kuna nyumba iko mkoani tena kijijini ina mita alafu luku tukinunulia huku Dar es Salaam tunapata na kutuma namba za hiyo luku mkoani na inaingia? Hivi kwani nini mtu kuhamisha kwa hapa Dar inaleta usumbufu eti ukajiandikishe upya kupata nyingine kwa nini isiwe hiyo hiyo mtu unahama nayo tuu kama tunavyohama na saa ya ukutani?

Naomba kufafanuliwa zaidi.
 
Nafikiri kila location ina no zake za mita ili iwe rahisi kugundua udanganyifu na hata kutatua hitkafu za umeme kirahisi. Sasa utoe kimgamuzi cha luku sehem nyingine ulete apo haiwezi kukubalika hata siku moja.
 
mhh
 
Hujaelewa hoja mlamu, jipe utulivu na ufikiri tena.
 
Ukifunga mita ya TANESCO hii ya luku kwa mfano mita nimefunga mbezi, alafu nikahama mbezi na mita yangu nikahamia labda magomeni na hiyo mita,nimesikie eti ni hadi nikahamishe location ya mita ili niweze kununulia umeme sehemu niliohamia bila hivyo siwezi pata hiyo huduma kwa hapo nitakapohamia.
Kununua umeme, unanunua popote. Tena kwa kutumia simu, utanunua kupitia mitandao yote.

Ila, tujue kuwa, umeme wa Tanesco, huwa umegawanywa kwa kanda. We mteja, unaweza kuhama au kuhamisha hiyo mita kwenda kwenye nyumba yoyote, ndani ya kanda husika. Ukihama kwenye kanda uliopo, huruhusiwi kuihamisha hiyo mita!

Nami ni mteja tu, nimechangia ninachokijua, kwani nishafanya hivyo, yaani kuhamisha mita, na pia kukataliwa kwani nilikuwa nahamia Kanda tofauti, na kushauriwa niombe upya kuunganishiwa.
 
Nafikiri kila location ina no zake za mita ili iwe rahisi kugundua udanganyifu na hata kutatua hitkafu za umeme kirahisi. Sasa utoe kimgamuzi cha luku sehem nyingine ulete apo haiwezi kukubalika hata siku moja.
Mbona mita iko mkoani tunanunua luku mkoa mwingine inakubali lakini hapa hapa mkommoja wilaya tofauti inaktaa inakuwaje
 
Amna kitu kama icho, unaingia kama kawaida. Ila fuata taratibu za kuamisha mita yako vinginevyo ni kosa kuamisha kienyeji
Sijahamisha nimeuliza nikaambiwa nikitaka nifuate hivyo ndo nauliza kwa nini.
 
Kununua umeme, unanunua popote. Tena kwa kutumia simu, utanunua kupitia mitandao yote.

Ila, tujue kuwa, umeme wa Tanesco, huwa umegawanywa kwa kanda. We mteja, unaweza kuhama au kuhamisha hiyo mita kwenda kwenye nyumba yoyote, ndani ya kanda husika. Ukihama kwenye kanda uliopo, huruhusiwi kuihamisha hiyo mita!

Nami ni mteja tu, nimechangia ninachokijua, kwani nishafanya hivyo, yaani kuhamisha mita, na pia kukataliwa kwani nilikuwa nahamia Kanda tofauti, na kushauriwa niombe upya kuunganishiwa.
Eheee wee ndio umenielewa sana kwa nini ukihamisha kununua luku kanda uliohamia inagoma.wakati kuna mita ziko mikoani huko luku tunanunulia huku inakubali ndio nataka nijue kwani kama ina2ezekana mita za mikoani tununue umeme mkoa mwingine lakini za hapa kwa hapa zikatae.
 
Mkuu Wa stendi umekuwa na mfululizo wa maswali kuhusu tanesco tena ambayo hayana mrengo mzuri, Unataka kuhujumu Shirika nini? We are watching your steps
 
Wakuu habari' iko hivi Tanesco wana mikoa yao ya kazi yaani kanda na kila kanda ina mfumo sawa kwa utendaji wa meter ndio maana meter hata iwe wapi inasoma ukiweka ktk system na ndio maana unaweza kununua umeme popote ndani ya inchi husika.

Inapokuja kwann meter iliyokua kinondoni mkwajuni ukipeleka Mbagala hauwezi kununua umeme ni kwa sababu hizo meter zinakua locked kwa mfumo maalum wa kanda husika ktk matumizi yake ukiihamisha ktk kanda nyingine lazima iwe locked kwa mfumo wa kanda husika ilipo na ndio sababu huwezi kuhamisha meter kienyeji toka kanda moja kwenda nyingine mpaka Tanesco wahusike ktk uhamishaji.
 
Ndugu mteja, mita ya TANESCO ikifungwa haiwezi kuhama kutoa eneo moja kwenda eneo jingine. Hii inatokana kuwa mita zote za Shirika zinafungwa kutokana na location ya mita hivyo kuhama ni sawa na mita kuwa imeibwa kutoka sehemu halisi kufungwa sehemu nyingine.

Kuhusu kununua umeme unaweza kununua sehemu yoyote
 
Vipi hakuna namna naweza kuingiza token nikiwa nimekaa sebuleni/ofisini bila kugusu mita?
 
Unalazimisha kutolea maelezo kitu ambacho hukijui.
Acha kujitutumua bhana.
Nafikiri kila location ina no zake za mita ili iwe rahisi kugundua udanganyifu na hata kutatua hitkafu za umeme kirahisi. Sasa utoe kimgamuzi cha luku sehem nyingine ulete apo haiwezi kukubalika hata siku moja.
 
Ndugu mteja, mita ya TANESCO ikifungwa haiwezi kuhama kutoa eneo moja kwenda eneo jingine. Hii inatokana kuwa mita zote za Shirika zinafungwa kutokana na location ya mita hivyo kuhama ni sawa na mita kuwa imeibwa kutoka sehemu halisi kufungwa sehemu nyingine.

Kuhusu kununua umeme unaweza kununua sehemu yoyote
Mbona kuna mfanyakazi wenu wa shirika alituambia hivyo lazma tuhamishe location ili tuweze nunua umeme hapo tulipohamia tena akasisitiza kuwa tusipofanya hieti jina linakuwa halipo eneo tùlipo hivyo luku hai tukanunulie tulikohama
 
Ihame kutoka wapi kwenda wapi
 
Back
Top Bottom