Miswaada ya sheria inayokwenda kwa hati ya dharura na mahitaji ya wakati husika!

Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,989
2,000
Serikali imekua ikipeleka miswaada mbalimbali bungeni kwa hati ya dharura ili kufanya marekebisho au kuweka sheria mpya!

Imekua ikizua maswali mengi kwa wadau mbalimbali juu ya umuhimu wa dharura hizo kwa mazingira ya wakati husika, nyingi za sheria hizo zinazokwenda kwa dharura zinaonekana kutokuwa na umuhimu wa uharaka huo nikitolea mfano miswaada ya sheria za makosa ya mtandao!

Lakini serikali imekuwa haipeleki miswaada kwa dharura kwa mambo ambayo pengine yanaonekana wazi kuwa yanahitaji marekebisho ya haraka!

Katika hilo natolea mfano sheria ya manunuzi ya umma imekuwa na kasoro nyingi sana hasa kwenye urasimu na mgogano wa maslahi! Ndio maana sio ajabu leo Mh Rais kuvunja sheria hizo kwa kufanya manunuzi na kutoa tenda kama apendavyo, rejea ununuzi wa ndege, ujenzi wa hostel UDSM na makazi ya askari magereza!

Suluhusho la sheria mbovu sio kuvunja sheria na kufanya unachoamini ni sahihi,hilo halitoi ufumbuzi wa kudumu!Suluhisho ni kupeleka miswaada bungeni kwa hati ya dharura ili sasa tuwe tumepata ufumbuzi wa kudumu!
Kiongozi kama Rais hakutakiwa kuwa mfano kwa kuvunja sheria za nchi, hata kama huzipendi na ni mbaya!

Ni zaidi ya mwaka uko madarakani,kasoro hizi umeziona muda mrefu hasa kwakuwa umekaa serikalini miaka mingi!Ndani ya mwaka huo ungeshakuwa umeshapeleka mswaada ya mabadiliko ya sheria ya manunuzi tena kwa hati ya dharura! Cha ajabu ni kwamba miswaada ya dharura inaenda ambayo haina uharaka zaidi ya kutengeneza mazingira ya kutawala nchi kiulaini!

Swali:
Akitokea waziri akatoa tenda kwa style kama yako utamuwajibisha?
 

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,404
2,000
Kwa spidi hii ya kuvunja sheria na katiba ni bora mswada usipelekwe bungeni kwani hata baada ya mabadiliko zitavunjwa tena.

Wasiwasi wangu ni kuwa mtu akivunja sheria nyingi upo uwezekano wa kiongozi atakayefuata baada ya yeye kuamua kumshtaki mahakamani na kumfunga, kwa hofu ya kuumizwa italazimika kubadili katiba abaki madarakani milele.

Wengi walianza hivi hivi kuvunja sheria ndogo ndogo kama za manunuzi ya umma na wakafikia kuvunja sheria kubwa kwa kuhamisha hela benki kuu na kuweka kwenye akaunti binafsi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom