Misukosuko ya maisha tunatoka nayo mbali sana

Misukosuko ya maisha tunatoka nayo mbali sana

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
2,204
Reaction score
2,086
Wakuu, kiukweli maisha yetu tunatoka nayo mbali sana, kuna kipindi unakua unapita katika njia ya maisha mpaka unahisi kama hiyo njia umepotea vile.

Kiukweli siwezi kusahau pindi nikiwa kwenye hekaheka za kutafuta kazi nilipeleka barua yangu ya maombi ya kazi kwenye kampuni moja maarufu hapa mjini.

Wakati nasubiri majibu, siku moja nikaenda kwa mama ntilie kununua maandazi asubuhi akanifungia vizuri, kufika nyumbani hamu yote ya maandazi iliniishia pale nilipogundua karatasi alionifungia nayo maandazi ni ile barua yangu ya kuombea kazi.

Nilifadhaika sana.
 
Duuuh , pole sana mkuu, endelea kupambana one Day yes , mungu hamtupi mja wake anaejituma
 
Back
Top Bottom